Rais wa FIFA anashambuliwa sana mda huu, mashabiki wa timu za Afrika wamepigwa komeo kuingia Marekani

stakehigh

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
40,702
Reaction score
41,213
Mwaka ujao kutakua na kombe la dunia na watu wengi mtandaoni wapo kwenye sintofaham ya kuingia marekan, mpaka sasa raisi hajatoa kauli yoyote lakini hali sio nzuri
 
Trump mbaguzi sana hataki wageni Nchini kwake anataka kombe la Dunia na pia hataki wageni si bora hilo kombe liende Nchi nyingine wao wabaki na sheria zao ngumu za kuishi USA.
 
Sasa wengine kama hata uchaguzi tu hamuwezi kufanya watu wako radhi kuua kwa ajili ya madaraka hata mimi ningekuwa rais wa Marekani siwezi kukubali kila mtu akae kwake.
 
Nizamie wapi mkuu nilitumia passport ya kaburu kutafuta maisha tu naishi Arusha na nipo na Usafirishaji na ununuzi wa magari makubwa huku kama sasa nipo huku nategemea kutoka wiki hii tukijaaliwa.
Huyo ni wewe mmoja, ila wengi wanazamia wanaanza kusumbua mamlaka za huko kuwarudisha makwao tena.
 
Hao hao wanaodai demokrasia sio muhimu kwa ustawi wa taifa ndio walewale wanaomba wapewe viza ili waende Marekani na kuzamia kabisa huko.
 
Mkienda hamrudi makwenu mnazamia.
πŸ˜„πŸ˜„.unachekesha hivi unajua nauli ya marekani ni bei gani? Gharama ya visa ya marekani ni bei gani?tiketi ya kuingia uwanjani ni bei gani? gharama za Marathi ni bei gani?
Mwafrika anayekwenda huko SIO MASIKINI KAMA UNAVYODHANI
 
πŸ˜„πŸ˜„.unachekesha hivi unajua nauli ya marekani ni bei gani? Gharama ya visa ya marekani ni bei gani?tiketi ya kuingia uwanjani ni bei gani? gharama za Marathi ni bei gani?
Mwafrika anayekwenda huko SIO MASIKINI KAMA UNAVYODHANI
Huwajui wazamiaji wewe.
 
Mwaka ujao kutakua na kombe la dunia na watu wengi mtandaoni wapo kwenye sintofaham ya kuingia marekan, mpaka sasa raisi hajatoa kauli yoyote lakini hali sio nzuri
Dunia ni ya Muumba. Tumezaliwa, tunaishi, na tutakufa. Trump aachwe na nchi yake; wananchi wake ndio waliomchagua. Sisi ni nani hata tumshinikize aendeshe nchi yake kwa matakwa yetu?

Mpira ni mchezo na pia ni biashara. Mbona Kombe la Dunia lilifanyika Qatar, wakaweka wazi marufuku dhidi ya ushoga, na FIFA haikuchukua hatua yoyote?

Basi na Trump aachwe na sheria zake. Kama kuna nchi hazitaki kushiriki chini ya sheria hizo, zisipeleke timu zao. Hakuna anayelazimishwa.
 
sasa ushoga na kuingia njini vitu mbili tafauti
 
Aisee, sawa tukubaline kutokubaliana tu.
Hivi unajua kuna watu wakifoji ukimbizi kigoma huko ili waende ng'ambo??
Watu wanafosi ni mapunga ili waende ng'ambo??
Sawaa ila Kwa point Yako ya kusema kuwa watu wanakwenda marekani kuangalia mpira Ili wazamie mimi nakukatalia .Kwa sababu mtu huyo sio masikini.landa aende Kwa ofa ya taifa lake mtu kama huyo anaweza akazamia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…