POTOSHI Rais wa Haiti anywa maji kwa kutumia jagi kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, 2026?

POTOSHI Rais wa Haiti anywa maji kwa kutumia jagi kwenye mkutano wa umoja wa mataifa, 2026?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kumekuwepo na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa Kiongozi wa Baraza la Urais la Mpito la Haiti, Edgard Leblanc Fils, hivi karibuni amezua gumzo wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), baada ya kunywa maji kwa kutumia jagi na kaucha kutumia glass kama ilivyo kawaida

Kwa kutumia njia ya ufuatiliji wa google reverse image search imeanisha kuwa video hiyo ni tukio la mwaka 2024 ambalo lolitokea wakati wa mkuu wa UNGA

Video hiyo ilimuonyesha Edgard Leblanc Fils, ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Urais la Mpito la Haiti, akihutubia Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79) mjini New York, Marekani, tarehe 26 Septemba 2024.

Katika tukio hilo, Leblanc Fils alionekana kunywa maji moja kwa moja kutoka kwenye jagi kubwa lililokuwa mbele yake, badala ya kutumia glasi iliyokuwepo. Sehemu ya maji hayo ilimwagika kwenye mavazi yake wakati akiendelea kunywa.

Hvyo video hiyo sio tukio la sasa ni tukio la zamani katika muendelezo wa matukio ya umoja wa mataifa
Sambamba na hilo video halisi ilichapishwa kwenye ukurasa wa umoja wa mataifa

Video hiyo inazid kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku mkutano mkuu wa UNGA ukiwa unaendelea marekani kwenye jiji la New york.
HAITI.jpg
 
Back
Top Bottom