Rais wa Mahakama ya Afrika: Nchi wanachama ziheshimu Hukumu za Mahakama ya Afrika bila Visingizio

Rais wa Mahakama ya Afrika: Nchi wanachama ziheshimu Hukumu za Mahakama ya Afrika bila Visingizio

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
20 February 2023
Arusha, Tanzania

Jaji Imani Daudi Aboud Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu yenye makao yake Arusha.

Leo ameziasa nchi wanachama kutekeleza hukumu zinazotolewa na mahakama hiyo ya Afrika bila visingizio kuwa hukumu hizo haziendani na sera za nchi zao husika.

Wito huo mzito umetolewa leo wakati wa ufunguzi wa mwaka mpya wa kazi ya korti hiyo ya juu ya Afrika the 2023 Judicial Year mjini Arusha Tanzania yalipo makao ya Mahakama ya Afrika.

Wabobezi wa sheria, wanataaluma nguli walichangia mada mbalimbali kuhusu katika siku hii ya ufunguzi wa mwaka wa kazi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu iliyoanzishwa na azimio la Umoja wa Afrika AU - African Union




ENGLISH :
20 February 2023
Arusha, Tanzania

Opening of the Judicial Year of The African Court - The Intergenerational Dialogue

Theme: Integrating the jurisprudence of regional and international human rights mechanisms into national systems The specific objectives of the inaugural opening of the judicial year were:

a. To provide a forum for interaction and discussion with Member States, inter-governmental, semi-governmental and non-state actors, to brainstorm, exchange and reflect on the work of the African Court for the year;

b. To enhance the visibility of the African Court among key human rights stakeholders on the continent;

c. To update the stakeholders on some of the specific activities that the African Court will conduct in realising the theme;

d. To reflect on the challenges facing the African Court and the African justice system and measures to tackle the challenges; and

e. To share lessons and experiences with key judicial officials and relevant stakeholders on the continent on the key thematic issues.

Source: African Court
 
Aende zake huko,ale mshahara atulie

USSR
 
20 February 2023
Arusha, Tanzania

Dkt. Mpango atoa wito kwa Mahakama ya Afrika kuzingatia mamlaka (jurisprudence / mandate) yake ili kuepukana na malalamiko ya nchi wanachama ya kuingilia uhuru wa ndani



Makamu wa rais mheshimiwa Dr. Philip Isdor Mpango alikuwa mgeni rasmi katika siku ya leo ya ufunguzi wa mwaka mpya wa kazi 2023 wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu ambapo hotuba yake ...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa wito kwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuzingatia Mamlaka yake ili kuepukana na malalamiko ya nchi wanachama ya kuingilia uhuru wa ndani wa nchi hali inayopelekea baadhi ya Nchi Wanachama kuondoa matamko ya kujiweka chini ya mamlaka ya Mahakama hiyo huku baadhi zikisita kuridhia Mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe 20 Februari 2023, wakati wa Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu, uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo Mkoani Arusha.

Dr. Philip Mpango amesema changamoto zinazopaswa kufanyiwa kazi ni pamoja na zile za kusikiliza na kutolea hukumu mashauri ambayo yako nje ya mamlaka ya mahakama hiyo, Mahakama kutoa hukumu dhidi ya nchi wanachama bila kuzingatia mazingira na mifumo ya kisheria ya nchi za Afrika na kupelekea hukumu hizo kutotekelezeka.

Dr. Philip Mpango meongeza kwamba njia ya mazungumzo kati ya Mahakama na Nchi Wanachama inapaswa kutumika ili malengo yaliyokusudiwa ya Mahakama hiyo yaweze kufikiwa.

Makamu wa Rais amempongeza Rais wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Jaji Imani Aboud, kwa hatua anazochukua kuimarisha mahusiano kati ya Mahakama hiyo na Nchi Wanachama na kumsihi kuendeleza jitihada hizo.
 
TOKA MAKTABA:

4 November 2021

Dkt. MPANGO - TANZANIA HAIJAJITOA KATIKA MAHAKAMA YA AFRIKA, BALI INPINGA SERIKALI KUSHITAKIWA

4 Nov 2021
— SERIKALI imesema, Tanzania haijajitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu bali imejiondoa katika sehemu ya tamko la itifaki linayoruhusu NGOs na watu binafsi kuishitaki serikali .

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameongeza kwamba Tanzania haijajitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu bali imejiondoa katika tamko lililofanywa chini ya ibara ya 34 (6) ya itifaki ya uanzishwaji wa Mahakama hiyo inayoruhusu mashirika yasio ya kiserikali pamoja na watu binafsi kuishitaki serikali katika mahakama hiyo.

Amesema Tanzania itaendelea kushirikiana vema na mahakama za Afrika kwa kutambua kwamba Afrika inahitaji vyombo vyake vya utoaji haki katika kutatua changamoto za waafrika.

Kwa upande wake Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud amesema kuongezwa kwa ufanisi katika utaoaji haki katika mahakama za ndani kwa nchi wanachama wa mahakama ya Afrika kutapunguza mrundikano wa kesi katika mahakama hiyo na kuongeza kwamba mjadala huo wa siku mbili unaofanyika hapa nchini utakua na maana zaidi kama utaongeza ufanisi wa utaoaji haki pamoja na kulinda haki za binadamu katika mahakama za ndani ya nchi.
 
4 April 2022

"HII ni MAHAKAMA PEKEE INAYOSIKILIZA KESI za HAKI za BINADAMU AFRIKA" - RAIS wa MAHAKAMA ya AFRIKA JAJI IMANI ABOUD


Jaji Imani Daud Aboud rais wa Mahakama ya Afrika anafafanua suala la haki za binadamu na watu, lina uwigo mtambuka mpana sana .

Jaji Imani Aboud anasema kwa mfano hata wafanyabiashara wakifilisiwa na mamlaka za serikali kupitia amri za kufungiwa biashara, masuala ya kodi n.k wanaweza kwenda katika Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu na watu, kwani suala hilo linahusu haki za binadamu kuvunjwa kupitia wenye biashara kukosa kipato na kukabiliwa na madeni ..

 
4 April 2022

"HII ni MAHAKAMA PEKEE INAYOSIKILIZA KESI za HAKI za BINADAMU AFRIKA" - RAIS wa MAHAKAMA ya AFRIKA JAJI IMANI ABOUD


Jaji Imani Daud Aboud rais wa Mahakama ya Afrika anafafanua suala la haki za binadamu na watu, lina uwigo mtambuka mpana sana .

Jaji Imani Aboud anasema kwa mfano hata wafanyabiashara wakifilisiwa na mamlaka za serikali kupitia amri za kufungiwa biashara, masuala ya kodi n.k wanaweza kwenda katika Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu na watu, kwani suala hilo linahusu haki za binadamu kuvunjwa kupitia wenye biashara kukosa kipato na kukabiliwa na madeni ..

Tz wanahofia nn!? Kama hawana mpango wa kuzivunja hizo haki, nn tatizo?! Au tayari wameshazivunja? alafu mahakama yenyewe iko hapa kwetu. itashangaza ikiwa serikali ilokubali mahakama iwepo hapa, haitatekeleza hukumu zinazohusu haki za binadamu! uoga wa nini?!
 
Tz wanahofia nn!? Kama hawana mpango wa kuzivunja hizo haki, nn tatizo?! Au tayari wameshazivunja? alafu mahakama yenyewe iko hapa kwetu. itashangaza ikiwa serikali ilokubali mahakama iwepo hapa, haitatekeleza hukumu zinazohusu haki za binadamu! uoga wa nini?!

Sovereignty aliyosema mwana CCM prof. Palamagamba Kabudi alidai inahusu kupinga ubeberu, sasa hii mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu sijui wanaiogopa nini hii serikali ya CCM

Toka maktaba:


TheCitizen.co.tz
https://www.thecitizen.co.tz › national
Kabudi: Tanzania won't succumb to pressure from donors

9 Apr 2021 — Our independence and sovereignty are worth more than money,” said Prof Kabudi. He said, China is Tanzania's trusted friend, hoping that the ...

The East African
https://www.theeastafrican.co.ke › tea
Respect our judicial, sovereign boundaries, Tanzania tells Arusha ...

6 Jan 2021 — At the time of filing Tanzania's withdrawal notice back in November 2019, Foreign Affairs Minister Palamagamba Kabudi said the
 
22 February 2023

JAJI CHANDE - MSITUPANGIE WATU WA KUONANA NA TUME YA KUBORESHA MFUMO WA HAKI JINAI, TUME INATAKA KUJUA UKWELI



Jaji Chande amesema ingawa hawawezi kuvamia wadau waliopo ktk mfumo wa haki jamii kama magereza, vituo vya polisi, Kamati ya Bunge ya sheria na katiba, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ,Usalama na Ulinzi, askari wa ngazi za chini yaani Rank and file n.k lakini inasisitiza Tume isipangiwe watu watakaokuja mbele ya tume. Hii ni kwa ajili ili Tume kujua ukweli wa malalamiki jinsi mfumo wa haki jinai unavyoendeshwa kiasi Mh. Rais Samia Hassan kuamua kuunda tume hiyo kuchunguza malalamiko.

Sasa Tume hiyo imemaliza kazi mkoani Dar es Salaam na sasa inakwenda mikoani na wilayani kufanya kazi mikoa 13 kayi ya 26 na wilaya 26 kati ya wilaya 139 zilizopo Tanzania bara, Zanzibar na Pemba.

Jaji Chande awataka wananchi kujitokeza kwa wingi mbele ya vikao vya tume hiyo pia katika anuani za mitandao ya tume iliyopo twitter, FB, Instagram, barua pepe / email na WhatsApp..
 

Ijumaa, 3 Februari 2023​

MAHAKAMA YAWEKA HISTORIA MPYA KATIKA MFUMO WA UTOAJI HAKI NCHINI​

Na Faustine Kapama-Mahakama
Mahakama ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa mfumo wa kunukuu na kutafsiri mienendo na hukumu, hatua inayokwenda kuongeza kasi na uwazi wakati wa usikilizaji wa mashauri na kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama.

Hayo yamebainishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma katika hotuba yake aliyoitoa kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma hivi karibuni.

Mhe. Prof. Juma ameeleza kwenye hotuba hiyo kuwa Mahakama ya Tanzania imekuwa ikitafuta mfumo (software) unaotumia akili bandia (Artificial Intelligence) kutafsiri mienendo ya mashauri na hukumu za Mahakama kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.

“Tuligundua kuwa Mahakama ya Juu ya India tayari ilikuwa inatumia software hiyo kutafsiri lugha kubwa tisa za India na kubaini kuwa India walipata ujuzi huo kutoka Italia, nchi yenye utaalamu na uzoefu mkubwa wa kutengeneza programu au softaware za kutafsiri na kuweka sauti katika maandishi (translation and transcription),” ameeleza.

Jaji Mkuu amesema kuwa wataalamu wa Mahakama ya Tanzania, Mahakama Kuu Zanzibar, wakishirikiana na wale wa Serikali Mtandao (eGA) walikwenda Italia kutafuta na kufanikiwa kutengeza mfumo na kuufundisha lugha ya Kiswahili kwa lafudhi na sauti mbalimbali za Kitanzania.

Ameeleza mfumo huo umejengwa kwa pamoja kati ya Mahakama ya Tanzania na Mkandarasi Almawave S.P.A wa Italia kwa kutumia fedha za ndani.

“Utakapoanza kutumika mfumo huu utawaondolea Majaji na Mahakimu jukumu zito la kunukuu na kutafsiri mienendo ya mashauri, hivyo kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri, uwazi na kuimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama. Tanzania pia itapata mrahaba wa asilimia 20 kwa mauzo yoyote ya mfumo huu kwa mtu mwingine,” Jaji Mkuu amesema.

Jaji Mkuu pia alitumia fursa hiyo kutambua uwezeshwaji mkubwa kwa Mahakama uliofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa mwaka 2022 aliendelea kuiongezea nguvu kazi Mahakama kwa kuteua Majaji 22 wa Mahakama Kuu.

Mhe. Prof. Juma ameeleza kuwa uteuzi huo uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2022 uliongeza idadi ya Majaji wa Mahakama Kuu kutoka 78 hadi 100 na hivyo kupunguza mzigo wa mashauri kwa ngazi hiyo kutoka mashauri 340 hadi 265 kwa wakati huo.

Amebainisha pia kuwa kwa mwaka 2022, watumishi 292 wapya waliajiriwa, wakiwemo Mahakimu Wakazi 48, ongezeko lambalo limesaidia pia Mahakama kutimiza mpango wake wa kusogeza huduma zake karibu na wananchi kwa kuanzishwa kwa huduma ya Mahakama Kuu katika Mkoa wa Manyara na huduma za Mahakama katika Wilaya 12 kufuatia kukamilika kwa mradi wa majengo ya Mahakama za Wilaya.

“Uwezeshaji mkubwa ulifanyika katika miundombinu ya majengo. Katika kipindi cha mwaka jana 2022 Mahakama ya Tanzania imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa majengo mapya 32 yakijumuisha majengo 24 ya Mahakama za Wilaya na matano ya Mahakama za Mwanzo. Aidha, majengo mengine matatu ya Mahakama yamefanyiwa ukarabati mkubwa,” alisema.

Jaji Mkuu ameeleza pia kuwa ili kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi, kupitia mradi wa maboresho 2020/21- 2024/25, Mahakama inatarajia kufikisha huduma ya Mahakama Kuu katika mikoa nane isiyo na huduma hiyo ambayo ni Singida, Pwani, Songwe, Katavi, Geita, Njombe, Simiyu na Lindi.

Aidha, alisema, Mahakama inatarajia kujenga Mahakama za Mwanzo 60 na Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki 10, kikiwemo Kituo kimoja kitakachojengwa huko Pemba na kupitia fedha za ndani kutajengwa jumla ya majengo 24, kati ya hayo 14 ni ya Mahakama za Wilaya na 10 ni ya Mahakama za Mwanzo.

Mhe. Prof. Juma kipekee amemshukuru Rais Samia pamoja na Serikali yote anayoiongoza kwa kuridhia na kufanikisha Serikali kuingia katika makubaliano na Benki ya Dunia mwishoni mwa Februari 2022 ya kuongeza fedha na muda wa utekelezaji wa mradi huo wa maboresho.

“Kukamilika kwa majengo hayo kutaongeza pia mahitaji ya watumishi. Ni matumaini yangu kwamba Serikali itaendelea kuiwezesha Mahakama kwa kutoa vibali vya ajira ili kusaidia wananchi kupata huduma za Mahakama karibu na maeneo yao kwa gharama nafuu na kwa wakati,” amesema.

Watanzania waliadhimisha Siku ya Sheria tarehe 1 Februari, 2023 kama ishara ya kuanza mwaka mpya wa shughuli za kimahakama kote nchini. Maadhimisho ya kitaifa yalifanyika jijini Dodoma, ambayo ni Makao Makuu ya nchi na mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

1677137463921.png

Picha: Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wananchi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria.

1677137502862.png

Photo: Viongozi Waandamizi wa Mahakama wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma Siku ya Sheria nchini

Source: MAHAKAMA YAWEKA HISTORIA MPYA KATIKA MFUMO WA UTOAJI HAKI NCHINI
 
Back
Top Bottom