Rais wa Malawi akubali kushindwa kabla ya matokeo rasmi kutangazwa

Rais wa Malawi akubali kushindwa kabla ya matokeo rasmi kutangazwa

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameweka historia baada ya kukubali kushindwa kwenye uchaguzi wa urais saa chache tu kabla ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo rasmi. Akihutubia taifa Septemba 24, 2025 Chakwera alisema: “Ni haki nikubali matokeo haya kwa heshima ya maamuzi ya wananchi na kwa kuheshimu katiba ya nchi. Nimejipanga kikamilifu kushirikiana katika mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani.”​

1758717616506.png
​

Taarifa za awali kutoka kwa Tume ya Uchaguzi zilionyesha aliyewahi kuwa rais, Peter Mutharika, akiwa na uongozi mkubwa kwenye uchaguzi uliofanyika Septemba 16. Muda mfupi baada ya taarifa za Chakwera, wafuasi wa Mutharika walisherehekea kwa shangwe katika kituo cha kitaifa cha kutangaza matokeo.

Huu ulikuwa ni uchaguzi wa nne kati ya Mutharika (85) na Chakwera (70). Mutharika aliwahi kushinda mwaka 2014 na 2019, ingawa ushindi wa 2019 ulifutwa na Mahakama ya Katiba kwa sababu ya udanganyifu mkubwa, ikiwemo kutumia correction fluid kwenye fomu za matokeo. Chakwera aliibuka mshindi katika marudio ya uchaguzi huo mwaka 2020.

Wachambuzi wa siasa walitarajia mapambano makali mwaka huu kutokana na hali ngumu ya kiuchumi iliyoikumba Malawi. Nchi imeathirika na kimbunga kikubwa na ukame wa kikanda unaohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, hali iliyoharibu mashamba na kuongeza umasikini.

Kwa zaidi ya miaka mitatu, mfumuko wa bei umekuwa zaidi ya asilimia 20. Takribani robo tatu ya Wamalawi wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa Benki ya Dunia wa dola 3 kwa siku, huku nusu ya wananchi wakikosa hata kiwango cha chini cha lishe bora kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia.​

================For English Audience================
​
Malawi president concedes election defeat hours before result announcement

LILONGWE, Sept 24 (Reuters) - Malawi's President Lazarus Chakwera on Wednesday conceded defeat in the Southern African country's presidential election, less than two hours before the final result was due to be announced. Official results released so far show ex-president Peter Mutharika, Chakwera's predecessor, has built a commanding lead in the September 16 election.

The Reuters Daily Briefing newsletter provides all the news you need to start your day. Sign up here.
"It is only right that I concede defeat out of respect for your will as citizens and out of respect for the constitution," Chakwera said in an address to the nation.

"I am fully committed to ... a peaceful transfer of power."
Malawi's electoral commission is due to release the presidential election result later on Wednesday.
Mutharika's supporters celebrated at the national results centre when they heard Chakwera had conceded.
This month's election was the fourth showdown between Mutharika, 85, and Chakwera, 70. Mutharika won in the 2014 and 2019 elections, though his 2019 victory was annulled by the constitutional court because of widespread irregularities including the use of correction fluid on results sheets. Chakwera won the re-run of that election in 2020.

Political analysts had predicted that Mutharika would mount a strong challenge to Chakwera's re-election bid, as the economy has worsened since the last election. A devastating cyclone and a regional drought, both linked to climate change, have wiped out crops and worsened hardship.

Inflation has been above 20% for more than three years. Nearly three-quarters of Malawians live below the World Bank's poverty line of $3 a day. Around half the population does not get the minimum number of calories for adequate nutrition, according to the bank's estimates.

SOURCE: REUTTERS​
 
Huyu sasa ndo Rais anaefaa kutumika kama mifano kwenye historia za nchi ya Africa kwenye vitabu vya mashuleni.
 
Ni haki nikubali matokeo haya kwa heshima ya maamuzi ya wananchi na kwa kuheshimu katiba ya nchi. Nimejipanga kikamilifu kushirikiana katika mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani.”
Na hii ndio demokrasia ya kweli. Nmemkubali sana
 
Back
Top Bottom