Rais wa Nchi anapofariki akiwa madarakani Nchi huwa katika nyakati za hatari zaidi kuliko wakati wowote ule

Kusema kweli tulipaswa kusimamisha Katiba... Nchi ikawa kwenye Baraza maalum, she is the mess
Kwani katiba haielezi kipi kinatakiwa kufuatwa baada ya Rais kufa?!!! Hivi umekwenda shule kweli ?!!!

Yaani uifanye katiba null and void simply tu kufurahisha nafsi ?!!! 😳😳
 
Metal mada una lako Jambo, umetudhihirishia uko like Kundi lisilomtaka Samia , na hamkuridhishwa na nia yake ya kuendelea.

Poleni sana zama zenu zishapita
Kama taifa anatutaka tuziishi ndoto na matakwa yake...
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi kutangaza nia...tatizo la chama kikubwa Kama CCM wangeanza kupambania nafasi za kugombea na kuacha kufanya kazi.....ili kuwakatisha tamaa na kazi ziendelee mujarabu huo ni KUTANGAZA TU HUKO....
 
Shida vijana wengi humu wanaushabiki tu, hawapendi kukiri ukweli wa mambo. Wakati tunakuwa , tuliambiwa Tanzania ni moja ya nchi inayoheshimika duniani kwa maswala ya upelelezi. Ila ni nchi isiyo na makuu. Ufanya mambo yake kimya kimya.
Sasa siasa hizi za leo ambazo watu wanadhani kudhalilisha au kutukana viongozi wakuu wa nchi na kukashifu Taifa lako na vyombo vya ulinzi ati ndo siasa za kukufanya uonekane wewe ni mjuvi wa mambo.
Kufa kwa kiongozi wa nchi ni sawa na kifo cha mzazi nyumbani, awe mama au baba. Familia utetereka kwa miaka. Hivyo tusikimbilie kusema nchi imesimama vizuri na kuanza kuropoka maneno tusiyojua.
Kitu kimoja kilinishangaza mama utadhani hii awamu ni tofauti na iliyopita, anasema alipoingia alikuta sijui shule kadhaa sasa anajenga kadhaa. Anajiweka kama vile hakuwepo kwenye serikali hilo pita. Anasahau yeye ni mwendelezo wa kumalizia awamu ya serikali iliyopita. Kwani alikuwa makamu wa Rais na ilani ni ileile inayotumika hakuna nyingine.
Mama anaanza kuona utamu wa madaraka, anajitangaza kuwa mgombea kabla ya wakati. Awe makini asipotoshwe. Hawezi achwa agombee tu bila kupimwa kuwa je ndo alikuwa chaguo baada ya Magufuli kama angemaliza muhula wake.
Nchi bado haijatulia, Rais wetu hasijione kafika. Na kuanza kujiona ana haki ya kufanya lolote!
 
Msukule wa Ngosha, rubbish
 
Kwani kikatiba mh.SSH ni rais nusu ?!!!
Kama sivyo unatanguliza hisia na matakwa binafsi ?!!!

Unaposema nchi haijatulia ina maana hakuna Rais.....hakuna mawaziri....hakuna UTULIVU katika mihimili ya JUDICIAL and LEGISLATIVE.....
 
Kwani kikatiba mh.SSH ni rais nusu ?!!!
Kama sivyo unatanguliza hisia na matakwa binafsi ?!!!

Unaposema nchi haijatulia ina maana hakuna Rais.....hakuna mawaziri....hakuna UTULIVU katika mihimili ya JUDICIAL and LEGISLATIVE.....
Hivi nchi kutotulia mpaka hao uliowataja wasiwepo? Au usanifu wa lugha ndo tatizo kwako? Pia usikurupuke soma uelewe kwanza si kukimbilia kujibu hoja bila kujua nini kimeongelewa.
Eti SSH ni Rais nusu? Wapi nimesema hivyo? Kweli mada za Kiswahili na Kiingereza zile za "Ufahamu" ni tatizo. Yaani mtu anasoma mada lakni atakachokuja andika kwa ufahamu wake ni aibu.
 
Waziri mkuu wa Israel aliyeuwawa anaitwa Yitzak Rabin

Kijana aliyemuua yes aliandaliwa na alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu. Alikuja kufungwa miaka 2 na sasa yupo huru.

Wale jamaa hovyo sana

Jina lake huyo kijana ni Dunisan wa ukoo wa Benjamini kati ya yale makabila 12 ya mbari za'wana wa Yakobo/Israel.
 
Sawa.....

Nchi kutotulia ni kipindi cha kufiwa na "incumbent president" na kabla hajaapishwa mpya....

Hujumuisha pia na uwepo wa "uasi" baada ya kifo hicho ama hata baada ya kupata rais mpya....sasa huo ukosefu wa UTULIVU unaupata wapi kipindi hiki?!!!
 
Mh.Rais SSH yuko sahihi kutangaza nia...tatizo la chama kikubwa Kama CCM wangeanza kupambania nafasi za kugombea na kuacha kufanya kazi.....ili kuwakatisha tamaa na kazi ziendelee mujarabu huo ni KUTANGAZA TU HUKO....
Huoni yeye kutangaza nia ili hali amekataza wengine wasiinue vichwa inaleta mkanganyiko kwamba kawekwa hapo kwa maslahi ya watu fulani?
 

TumainiEl🙏
 
Kwa mujibu wa maelezo yako mengi unataka kuniambia Idala ya Usalama wa Uganda iko kwa maslahi ya Taifa la Uganda??😅😅😅😅
 
Ukosefu wa utulivu si vurugu mtaani au nn, bali unakuwa hasa kwa system nzima na wananchi. Inaweza kuwa kisaikolojia. Mfano, wananchi watakuwa hawajaelewa, direction ipi wataenda. Kuna kuwa na lugha ambazo mfano kukitokea jambo watu wanakimbilia kusema heri fulani angekuwepo? Haya mambo ni kisaikolojia inaitajika muda mpaka hapo watu watazoea na utulivu utaendelea.

Pia kutokuwepo utulivu ktk maswala mazima ya kiutawala. Hii mfano kuna makundi yatatokea yaweza kuwa ya siri au uwazi. Kuna ambao watakuwa bado wanamlengo wa kiongozi alopita, na ambao watakuwa ktk mlengo wa kiongozi aliopo madarakani. Hii haileti utulivu, hata Rais aliopo itakuwa inamsumbua kichwani. Ni mambo yanayohitaji muda. Tazama hata katuni ya kipaya, utajua nachoongelea.

Utulivu usiokuwepo ni wakisakolojia hasa kwa wananchi. Na pia utulivu usiokuwepo ni wakitawala. Rejea sasa Swala la machinga. Inaonesha viongozi wa mikoa kadhaa wanawatimua machinga. Viongozi wengine wanasema hapana Magufuli alikataa wasitimuliwe. Mama hataki toa maamuzi ya wazi kama Magufuli alivyofanya, alimwita SSH wakati huo akiwa makamu na waziri wa Tamisemi akasema Machinga wasibughuziwe, Mkuu wa Mkoa anae ona hataki kufuata maagizo ajiuzuru. Hii ilikuwa kauli ya JPM haikuwa na unafiki.

Mama yeye anasema wapangeni, lakn viongozi hawajali wameendelea kufanya watakavyo. Je hapa mama Rais wetu anaogopa kuchukua hatua? Make machinga hawapangwi bali wanafukuzwa. Hii ndo kutokuwepo kwa utulivu kiutawala, na mengine mengi.
 
Asante sana mkuu kwa hii elimu. Hakika nimeshausoma sasa mchezo. Na kwa ulivyoelimisha nadhani 1 na 3 kazi iko kubwa mbele yao. Hakika Kifo cha Dkt Magufuli ni dhihaka kubwa sana kwa idara nyeti, maana eti wapinzani walifanya sherehe? Yaani baadhi ya viongozi wa juu wa serikali walishukuru na kushangilia kifo. Nadhani wengi hatukufahamu madhara yake. Ni muhimu Mungu amlinde Mama Samia. Tulimuombea sana Dkt Magufuli, na tulikuwa na nafasi ya kumuombea zaidi kama tungejulishwa anaumwa. Mungu hakika sijui ilikuwaje kuugua kwa Dkt Magufuli kuwe siri mpaka kifo chake. Kumbe kuna huo utaratibu tena wa vyombo vya ulinzi na usalama, hakika huu uzi ni muhimu sana kwa viongozi wote waandamizi, hasa waliojitokeza na kuonesha kuwa Wateule wa Dkt Magufuli hawafai kumbe wanaingia 18 za watu.
 
Mkuki kwa nguruwe. Lesson learned
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…