Shida vijana wengi humu wanaushabiki tu, hawapendi kukiri ukweli wa mambo. Wakati tunakuwa , tuliambiwa Tanzania ni moja ya nchi inayoheshimika duniani kwa maswala ya upelelezi. Ila ni nchi isiyo na makuu. Ufanya mambo yake kimya kimya.
Sasa siasa hizi za leo ambazo watu wanadhani kudhalilisha au kutukana viongozi wakuu wa nchi na kukashifu Taifa lako na vyombo vya ulinzi ati ndo siasa za kukufanya uonekane wewe ni mjuvi wa mambo.
Kufa kwa kiongozi wa nchi ni sawa na kifo cha mzazi nyumbani, awe mama au baba. Familia utetereka kwa miaka. Hivyo tusikimbilie kusema nchi imesimama vizuri na kuanza kuropoka maneno tusiyojua.
Kitu kimoja kilinishangaza mama utadhani hii awamu ni tofauti na iliyopita, anasema alipoingia alikuta sijui shule kadhaa sasa anajenga kadhaa. Anajiweka kama vile hakuwepo kwenye serikali hilo pita. Anasahau yeye ni mwendelezo wa kumalizia awamu ya serikali iliyopita. Kwani alikuwa makamu wa Rais na ilani ni ileile inayotumika hakuna nyingine.
Mama anaanza kuona utamu wa madaraka, anajitangaza kuwa mgombea kabla ya wakati. Awe makini asipotoshwe. Hawezi achwa agombee tu bila kupimwa kuwa je ndo alikuwa chaguo baada ya Magufuli kama angemaliza muhula wake.
Nchi bado haijatulia, Rais wetu hasijione kafika. Na kuanza kujiona ana haki ya kufanya lolote!