Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?


Uwezo wa Rais wetu unatia mashaka. Lugha za mitaani na sokoni Kariakoo huwezi kuziweka katika hotuba ya kitaifa kama ile ambayo unajua nchi nzima na mashirika wahisani wanasubiri kusikia utasema nini.
Kama kiongozi wa nchi anajua wazi kuwa utawala wake umeshindwa kuimarisha uchumi na pesa yetu inadondoka kwa kasi na wananchi kwa hasira waaiita pesa hiyo ya MADAFU. Hakupaswa naye kama Rais kulibariki jina hilo la kejeli la pesa yetu hadharani. Hii nisawa na mwenye mke ambaye anashindwa kumtunza kiasi anaonekana mchafu na mtaani ana jina la utani " Masulupwete".
Sasa mume awe ana address kikao cha mtaani kisha anamtambulisha mkewe kama Masulupwete huo sii utakuwa ujinga?
 
kama raisi anajukumu la kusimamia ukuaji wa uchumi na thamani ya fedha ya nchi yake,kinyum cha hapo ni umasikini uliotopea kwa wananchi wake
 
Kuwa mzalendo ww!! Kushuka kwa thaman ya tsh kwa dola kumeifanya wanasiasa kama chenge, na jk kuita pesa yetu kwa maneno ya kejeri na dharau. Kuwa na rais mswahl ndo tabu yake hyo
 

100% na watu wazima humu JF eti hawaoni tatizo? Yule ni mkuu wa nchi na alikuwa anaongelea hatima ya maisha yetu. Wengi wetu sasa tunashindwa hata kupanga bajeti kwasababu ya mfumuko wa bei. Mada yenyewe aliyokuwa anaongelea sio ya utani kwani wafadhili wamezuia hela na watu wanakufa kwa kukosa dawa
 

Nilipata ukakasi
 

Maneno yanabeba maana kubwa. Ni kielelezo tosha jinsi mtu anavyoelewa au kulichukulia au kulipa uzito jambo. AMECHEMKA!
 

Sawa mtoto wa mtaani
 
Mkuu,
Hujajibu swali langu lililoko ndani ya hoja yangu.

Kwani pesa ya madafu ni nini au ina maana gani?

Je, hiyo maana inaondoa ukweli wake?

Nadhani hoja yako ina harufu ya political correctness!
 

Mkuu msingi wa kuiita fedha yetu madafu wakati ule ilikuwa ni kumaanisha kuwa ina thamani ndogo kiasi cha kununua madafu hata kama ni noti kubwa.

Anachimaanisha mleta thread ni kuwa kwa mkuu wa Nchi kutumia kejeli hiyo ni dharau kwa fedha yetu.
 
Moja kwa moja akiachia madaraka ni mahakamani, sasa hivi nahitaji msaada wa kisheria maana hata shilingi ni tunu ya taifa.
 

unajiita "dos santos", ningeshangaa kama ungekuwa na mawazo tofauti na haya
 
Mtoto kama ni mbumbumbu kiasi gani hauwezi kumchana laiv vile2 tena mbele ya wanafunzi ama watoto wenzie kua hana akili, mpumbavuu au la mchafuuu!!!
Especially ukiwa kama mwalimu au mzazi au mlezi!!
JK hana elimu ya kisaikolojia, naamini hata IQ yke ya kuforce sana coz ana uwezo mdogo sana ktk kufikiri!!!!
 
Mkuu msingi wa kuiita fedha yetu madafu wakati ule ilikuwa ni kumaanisha kuwa ina thamani ndogo kiasi cha kununua madafu hata kama ni noti kubwa.

Anachimaanisha mleta thread ni kuwa kwa mkuu wa Nchi kutumia kejeli hiyo ni dharau kwa fedha yetu.
Mimi sioni tatizo lolote kwa sababu haliondoi ukweli na halileti athari yoyote katika uchumi.

Mbona maneno ya utani au wakati hata UK wanaita utawasikia wanaita pesa yao majina kama quid, nicker, bin lid, vile vile hata Wamarekani wanaita pesa yao majina kama bucks.
 

Hiv kwann wengi wetu huonekana tunapenda ukweli lakin ukweli unapowekwa waz kwa baadhi ya mambo tunaanza kukosoa ,tatizo nchi yetu saiz kila mtu anajua , anataka kuonekana anajua zaid ya wengine ( muchknow), sasa ndugu kwann unakataa ukweli alioungea rais kuwa ni fedha za madafu? Hebu nenda kaulize elf 1 ya tanzania ni sawa na dola ngapi za kimarekan hapo ni mwanzo mzuri wa kujua kuwa rais hajakosa kusema alichosema, tatizo ukweli unauma sana lakin ndo ukweli hata ukisema utukane au umshambulie rais , ukweli utabaki palepale na hauwezi kufunikwa na kauli mbiu za kujifariji
 
Aliikuta Tsh 600 kwa USD 1;Sasa ni Tsh 1800 kwa USD 1:anahaki ya kuidharau naamini Ana nia ya dhati kuiua nchi hii.
 
Sasa wewe ulitaka iitwe pesa gani kama si ya madafu, ina thamani gani? mtu anaongea lugha ambae yule msikilizaje ataelewa pia ndiyo jina tulioipa sarafu yetu na tunalitumia katika maongezi yetu ya kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…