Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.
Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?
Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
Mkuu,Soma vizuri kilichoandikwa na mtoa hoja, siyo kukurupuka!
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.
Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?
Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
Mkuu hapo ni kama wewe uambiwe "una degree ya chupi" - yani ni tusi na dharau inayoonyesha kwamba kisomo chako hakina thamani! Hivyo ndio kusema kwamba: "Pesa za madafu" maana yake ni pesa zisizo na thamani!
Mimi sijaona tatizo lolote, kukosa hoja za msingi za kujadili mambo muhimu
tunakaa kushupalia neno 'pesa ya madafu'. Labda hili linaweza kuwa tatizo
kwa watu wa shamba na si mjini. Neno hilo halina athari yoyote iwe kisiasa
kiuchumi nk. Tutafute kukosoa hotuba yake katika mambo mengine
kujadili hili ni upuuzi zaidi.
Unadhani Nyerere alikuwa mjinga kumkataa huyu mswahili wa M.so.g.a?Nyinyi mkajifanya kiherehere kumtaka awe rais wenu eti atawaletea maisha bora,Haya mvumilie sasa maana haya matatizo mliyataka wenyewe!Nimemsikiliza rais Jakaya Kikwete (JK) jana na hotuba yake ya kujibaraguza mbele ya Watanzania. Sikutegemea jipya kwenye story zake za jana na wale Wazee wa vijiwe vya CCM ila hili la yeye kama rais wa nchi kudharau sarafu ya nchi yake mwenyewe hadharani limenisikitisha sana.
Ni ajabu sana kwa rais wa nchi kwenda mbele ya vyombo vya habari kukiwa na halaiki ya watu na kuiita bila haya wala aibu sarafu ya nchi kwa jina la kebehi kuwa eti ni "hela ya madafu" halafu anaachwa tu hakuna kitakachompata. Hii ni fedheha na dharau ya hali ya juu kwa sisi ambao hela hiyo ya 'madafu' ndio mshahara wetu na fedha yetu ya kufanya biashara kila siku.
Tunajua mmeiba sana na tena mkishaiba chap chap mnazibadilisha kuwa dollar hivyo haya "madafu" hata yawe sawa na toilet paper (karatasi za kuchambia) kwenu sio issue. Itakuwa ajabu sana kama nikimsikia tena waziri wa fedha na uchumi akisisitiza wafanyabiashara hasa Wahindi ambao wanajua sana umuhimu wa dhamani ya fedha wasiuze bidhaa zao kwa dollar maana hela wanayoambiwa watumie hata mkuu wa nchi anaiona haina maana yoyote zaidi ya kuwaweza kununulia tunda la bei duni la aina ya madafu.
Rais anatakiwa aelewe kuwa kauli zake za namna hii tena anazozitoa hadharani zina madhara ya moja kwa moja kwa uchumi wetu na achunge sana kauli zake anapozungumza masuala muhimu ya nchi hadharani. Kama ni kutudharau kesha fanya hivo sana lakini atuache basi na hii sarafu yetu ambayo kila kukicha anafanya mbinu za kuishusha dhamani. Kudharau sarafu ya nchi hadharani tena mchana kweupe na mtoa dharau akiwa ndie rais wa nchi inatakiwa liwe kosa la uhujumu uchumi na JK anapaswa kushitakiwa kwa hili.
Tumekuvumilia kwa mengi JK lakini kwa kuifananisha sarafu yetu na madafu umevuka mipaka. Bora ungeiita hivyo ukiwa chumbani kwako au ukisha acha nafasi yako ya urais. Ni kwa sababu unaongoza nchi yenye mifumo mibovu ya sheria inayokulinda laiti ingelikuwa nchi nyingine kauli yako hiyo ingetosha wewe kujiuzulu ukachunge mbuzi wako kule Msoga.
Mwana JF hebu piga picha nini kitampata rais Baraka Obama wa Marekani kama siku atakwenda hadharani kukiwa na vyomba vya habari na kutamka maneno ya dhihaka kwa dollar kama alivyofanya rais Jakaya Kikwete jana pale ukumbi wa Diamond Jubilee. Jibu nadhani unalo mwenyewe mwana Jf.
Wasalaam,
Kinyungu.
Mimi sioni tatizo lolote kwa sababu haliondoi ukweli na halileti athari yoyote katika uchumi.
Mbona maneno ya utani au wakati hata UK wanaita utawasikia wanaita pesa yao majina kama quid, nicker, bin lid, vile vile hata Wamarekani wanaita pesa yao majina kama bucks.
'Hela ya madafu' ni fedha yenye thamani ndogo,na kweli fedha yetu imeshuka sana thamani kwasababu ya sera zake mbovu za kiuchumi na kifedha pamoja na ufisadi mkubwa unaoendelea kwenye fedha za umma.Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.
Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.
Raisi hapaswi kamwe kuikejeli sarafu ambayo yeye ndo alipaswa aisimamie ili thamani yake iwe juu,kwa nchi nyingine zenye uwajibikaji hii ni skandali kubwa yenye uwezo wa kumjambisha mpaka atengue kauli.
Kutokuona kasoro pana ya raisi kutoa kauli kama hiyo ni upuuzi mwingine baada ya huo ulioutaja.
Nawasilisha!
Mkuu,Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.
Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.
Mimi sioni tatizo lolote kwa sababu haliondoi ukweli na halileti athari yoyote katika uchumi.
Mbona maneno ya utani au wakati hata UK wanaita utawasikia wanaita pesa yao majina kama quid, nicker, bin lid, vile vile hata Wamarekani wanaita pesa yao majina kama bucks.
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.
Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?
Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
Mkuu,Hata sisi tunaita pesa mkwanja,mapene,mpunga,dinyilu,kisu nk hzo ni nicknames za pesa lakini "madafu" ni kejeli kwa pesa yetu kutokana na kutokuwa na thamani.
Inakuaje raisi anafurahishwa na kubariki kejeli hyo badala ya kusikitika?