Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Tukijiheshimu tutaheshimika..... Duuuh !
Tukijitukuza tutatukuzwa na kutukuka...
Tukijistiri tutastirika.... Kinyungu
 
Last edited by a moderator:
Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.

Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.

Fedha ya Madafu kwa muktadha wa watumiaji wa mitaani ni fedha ambayo haina thamani. Fedha ambayo thamani yake inabadirika badirika mintarafu kushuka mara kwa mara. Ni nini kinachoshusha thamani ya fedha ya nchi? Ni hali ya uchumi wa nchi pamoja na sera za kiuchumi za serikali inayokuwa madarakani (fiscal policy).

Rais ndo msimamiaji mkuu wa fiscal policies na ndiyo msimizi mkuu wa sera za uchumi wa nchi. Fedha ya madafu mara nyingi inatumika kwa ajili ya kuonesha kuwa wale wanaosimamia uchumi wetu hawawezi - kutokana na kuwa hawawezi fedha yetu thamani yake inashuka kila wakati.

Rais ndo msimamiaji mkuu wa sera za uchumi na sera za fedha. Anapotumia slang ile ile ya mitaani, inaonesha ukosefu wa kuwajibika. Yaani rais haoni kuwa matendo yake kama rais ndo yanayosababisha fedha ya nchi iwe inayumba kila siku.

Kwa mfano; kwenye escrow tuliambiwa na Takukuru kuwa zilitolewa bilioni 73 taslimu. Matukio kama haya sera za kifedha haziyaruhusu yafanyike kwa maana kuwa hii ndo inasababisha kujaa kwa shilling kwenye mzunguko kunakofanya mfumko wa bei (inflation). Matukio kama EPA, ESCROW, n.k. ndo mambo yanayofanya fedha ya nchi ikose stability kwenye soko na kushuka haraka haraka.

Kauli kama ile kutoka kwa rais (kuita shillingi madafu) kunafanya vile vile wawekezaji wanaotoka nje ya nchi kukosa imani na fedha ya nchi na hivyo kusisitiza matumizi ya fedha za nje hata kwenye miamala (transactions) ambayo ingehitaji shillingi. Hii maana yake ni kuwa tunalazimika kutumia dola nyingi kwenye mfumo wa uchumi, wakati dola zinazoingia nchini ni kidogo. Hili huchangia kushusha thamani ya shilingi zaidi na kuifanya iendelee kuwa madafu zaidi na zaidi.

Kwa ujumla kauli hiyo ina madhara makubwa sana kwa uchumi wa nchi. Inawezekana wewe huwa huchukulii kwa uzito kauli za viongozi wako. Lakini ukae ukijua kuwa tuko kwenye mfumo wa kidunia ambapo kauli za viongozi zina thamani kama fedha. Kauli kama ile imeisababishia nchi ya Tanzania hasara ya mabilioni na rais kama mchumi jambo hilo ilitakiwa awe analijua sana. Wanaofanya speculation ambao ndo wanaoendesha uchumi wa dunia huangalia sana mwenendo wa uongozi wa nchi na viongozi wake.

Yaani kauli kama ile kuna hata wawekezaji walioisikia kauli ile wanaahirisha kabisa kuja kuwekeza Tanzania. Au mabenki yanayotoa mikopo kwa wanaowekeza Tanzania wakaongeza riba kutokana na kuongezeka kwa "risk profile" ya nchi. Haya ni mambo mazito kweli kweli, si mchezo mchezo na yana madhara ya moja kwa moja kwa nchi.

Kiongozi kama huyu, hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi kwa sababu haelewi ni kwa namna gani kauli zake zinaiathiri nchi.
 
Nyerere alisema Kikwete hafai, ninyi mkampa, mnategemea nini?
 
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.

Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?

Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.

Kama unalipwa mshahara kwa hela ya tanzania alafu hujui ubaya wa kuitwa hela ya madafu. Basi hata ukitukaniwa mama yako ni malaya hata kama ni ukweli utachekelea kwasababu ni uhalisia.
 
Mkuu, lazima awe dharau maana zile wanazokwapua zipp kwa dollar.
Ndio zile kauli za akina Chenge- vijisenti

Sibonike;
Hilo ndo jibu mahususi kwa hilo neno au usemi wa rais. Hawa watu hawanaga hizi pesa zetu. Tangu wamekataa hata kuweka picha zao humo wameamua kutozitumia kabisaa. Noti inapakwa rangi ya unga ka ile dawa ya cbd?? Umeona wapi??
Wao wanazijua dollar wala si haya makaratasi. Wanashangaa wezi wanaoiba hizo hela za madafu mpaka hata kuutoa uhai wa mtu. Shs 150 million juzi watu wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa. Wakati Chenge kajichukulia 1.6 Bilion mara zaidi ya 3, EPA, RADA, ESCROW bado kapewa nafasi ya kutuandikia katiba kama mwandishi mkuuu. Hela za madafu, zisitutoe roho, tusiwakemee wezi wa madafu. Pongezi rais wetu kwa kuwa muwazi na mkweli daima.
 
Mkuu,
Kwa nini unaita pesa yetu mkwanja, mapene, mpunga, dinyilu na kisu?. Huoni kama hii ni dharau kwa sababu kuna jina lake kisheria ambalo ni shilingi.

Kama hiyo siyo dharau, kwa nini kuita madafu ndiyo iwe dharau?

Hayo majina yote niliyoyataja tunayatumia katika mtazamo chanya nadhan ni kama hao uliowataja wanavyotumia hayo majina,tatizo ni neno "madafu" ambalo linaakisi mtazamo hasi mbele ya sarafu yetu.
Hivi unaweza sikia mwanao ana nickname ya kikojozi afu babake ukasimama mbele ya kadamnasi ukamuita hvyo?
 
Watanzania tukome kuwapa watu wa pwani Urais, hawa watu asili yao ni uvivu na kukaa vijiweni, hata jana pale Diamond kilikuwa ni kijiwe cha wazee/waswahili wa Dar wasiojitambua. Mambo kama hayo mimi sikuona kulikuwa na haja gani ya kuweka kijiwe, ilikuwa ni kuchukua hatua basi
 
Kauli ya Kiongozi wa nchi ni sawa sawa na fedha. Inaweza ikawa fedha kuingia au fedha kutoka. Kauli mbaya inaongeza risk ya watu kuwekeza kwenye nchi. Risk maana yake ni riba kuongezeka. Riba ni gharama kwa uchumi kwani huongeza cost of doing business katika nchi husika. Cost of doing business huongeza gharama ya bidhaa na huduma na kuyafanya maisha katika nchi yawe magumu.

Muulizeni mchumi yeyote atawaambia hivyo!
 
Fedha ya Madafu kwa muktadha wa watumiaji wa mitaani ni fedha ambayo haina thamani. Fedha ambayo thamani yake inabadirika badirika mintarafu kushuka mara kwa mara. Ni nini kinachoshusha thamani ya fedha ya nchi? Ni hali ya uchumi wa nchi pamoja na sera za kiuchumi za serikali inayokuwa madarakani (fiscal policy).

Rais ndo msimamiaji mkuu wa fiscal policies na ndiyo msimizi mkuu wa sera za uchumi wa nchi. Fedha ya madafu mara nyingi inatumika kwa ajili ya kuonesha kuwa wale wanaosimamia uchumi wetu hawawezi - kutokana na kuwa hawawezi fedha yetu thamani yake inashuka kila wakati.

Rais ndo msimamiaji mkuu wa sera za uchumi na sera za fedha. Anapotumia slang ile ile ya mitaani, inaonesha ukosefu wa kuwajibika. Yaani rais haoni kuwa matendo yake kama rais ndo yanayosababisha fedha ya nchi iwe inayumba kila siku.

Kwa mfano; kwenye escrow tuliambiwa na Takukuru kuwa zilitolewa bilioni 73 taslimu. Matukio kama haya sera za kifedha haziyaruhusu yafanyike kwa maana kuwa hii ndo inasababisha kujaa kwa shilling kwenye mzunguko kunakofanya mfumko wa bei (inflation). Matukio kama EPA, ESCROW, n.k. ndo mambo yanayofanya fedha ya nchi ikose stability kwenye soko na kushuka haraka haraka.

Kauli kama ile kutoka kwa rais (kuita shillingi madafu) kunafanya vile vile wawekezaji wanaotoka nje ya nchi kukosa imani na fedha ya nchi na hivyo kusisitiza matumizi ya fedha za nje hata kwenye miamala (transactions) ambayo ingehitaji shillingi. Hii maana yake ni kuwa tunalazimika kutumia dola nyingi kwenye mfumo wa uchumi, wakati dola zinazoingia nchini ni kidogo. Hili huchangia kushusha thamani ya shilingi zaidi na kuifanya iendelee kuwa madafu zaidi na zaidi.

Kwa ujumla kauli hiyo ina madhara makubwa sana kwa uchumi wa nchi. Inawezekana wewe huwa huchukulii kwa uzito kauli za viongozi wako. Lakini ukae ukijua kuwa tuko kwenye mfumo wa kidunia ambapo kauli za viongozi zina thamani kama fedha. Kauli kama ile imeisababishia nchi ya Tanzania hasara ya mabilioni na rais kama mchumi jambo hilo ilitakiwa awe analijua sana. Wanaofanya speculation ambao ndo wanaoendesha uchumi wa dunia huangalia sana mwenendo wa uongozi wa nchi na viongozi wake.

Yaani kauli kama ile kuna hata wawekezaji walioisikia kauli ile wanaahirisha kabisa kuja kuwekeza Tanzania. Au mabenki yanayotoa mikopo kwa wanaowekeza Tanzania wakaongeza riba kutokana na kuongezeka kwa "risk profile" ya nchi. Haya ni mambo mazito kweli kweli, si mchezo mchezo na yana madhara ya moja kwa moja kwa nchi.

Kiongozi kama huyu, hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi kwa sababu haelewi ni kwa namna gani kauli zake zinaiathiri nchi.
You're spot on Mkuu,Tatizo Watanzania wengi hatufuatilii mienendo ya kisiasa nje ya mipaka ya nchi yetu,Tungekuwa tunafuatilia masuala ya kisiasa katika nchi nyingine let's say America basi viongozi wazembe kama JK na wengineo si tu wangetawala katika mazingira magumu kwasababu ya Wananchi kupenda kuchambua na kupima kauli na mienendo yake ya kiutawala bali pia asingekuwa madarakani hii leo.Wenzetu kule kila kinachozungumzwa au kutendwa na kiongozi kinachukuliwa kwa umakini mkubwa na kina athari za aidha moja kwa moja au siyo moja kwa moja Kwenye mienendo ya masoko ya fedha,uwekezaji na kadhalika.Ila hapa Tanzania tunafanya mambo kwa mazowea tu,hii ndilo tatizo letu kubwa,Ndiyo maana Jumuiya ya Afrika Mashariki yaelekea kutushinda kwasababu wenzetu majirani wamejiwekea vision za maendeleo na standard za kiwango cha juu cha uwajibikaji wakati sisi tunafanya mambo yetu kiswahili Swahili.Tabu kweli kweli.
 
Kwahili hats mimi sijaona shida kuiita pesa yetu no madafu sababu neno pesa ya madafu inamaanisha dafu halijawahi au muuza dafu hawezi kupanga being ya dafu kwa gharama za kigeni. Name dafu laliwa lachokolewa sana hapa kwetu mpaka twapata tezi Duke Yakheeee
 
'Hela ya madafu' ni fedha yenye thamani ndogo,na kweli fedha yetu imeshuka sana thamani kwa sababu ya sera zake mbovu za kiuchumi na kifedha pamoja na ufisadi mkubwa unaoendelea kwenye fedha za umma.

TShs. 1 = Japannese Yen 0.071
TShs. 1 = Chinese Yuan 0.00366520
 
Kwa waliosoma na kufaulu lugha ya kiswahili, madafu ni "sifa". Japo kwa wengine wanaona ni dharau, lakini ni sifa tu. Kuna mwingine anaweza kuiita hela ya ugolo, embe, mchicha, mkaa, n.k. Hata hiyo dollar ina majina kibao km dough, bill kutegemeana na wingi au uchache wake.

Kwa kifupi, ACHENI JAZBA NA CHUKI.detichi
 
Iddi Amini alimshikisha adabu Gavana wa Benki Kuu ya Uganda alipo iita Uganda Shiling Worthless paper! Wakati huo uganda kilo ya sukari ilikuwa inauzwa UShs. 100/-. Leo Rais wetu anaita Tshs. "Hela ya Madafu" wananchi tunachekelea. Wakati yeye mwenyewe kasababisha sarafu yetu kukosa thamani kiasi hiki. Hivi tumelogwa! :frusty:
 
TShs. 1 = Japannese Yen 0.071
TShs. 1 = Chinese Yuan 0.00366520

Nenda pale samora ukachungulie tena kwenye bureau de change. Hizi namba zako si sahihi. Hata hivyo thamani halisi ya fedha iko kwenye "stability" sana sana si kwenye exchange rate. Pamoja na kuwa umekosea mno na hesabu zako si sahihi, angalia kwa mwaka thamani ya yen au yuan inapungua kiasi gani? Hicho ndo kipimo cha fedha. Hard currency si fedha yenye exchange rate kubwa, bali ni fedha ambayo thamani yake haiyumbi!! Hizo Namba zako ni uongo ulioshiba!
 
Hakuna maana kuwa na benki kuu ya Tanzania...So dollar ihalalishwe kwa matumizi ya kawaida ya wananchi kama ilivyo kwa nchi kama Zimbabwe ambayo inatumia pound na dollar kama fedha za nchi hiyo...IMENIFEDHEHESHA NA KUNISONONESHA SANA...
 
Fedha ya Madafu kwa muktadha wa watumiaji wa mitaani ni fedha ambayo haina thamani. Fedha ambayo thamani yake inabadirika badirika mintarafu kushuka mara kwa mara. Ni nini kinachoshusha thamani ya fedha ya nchi? Ni hali ya uchumi wa nchi pamoja na sera za kiuchumi za serikali inayokuwa madarakani (fiscal policy).

Rais ndo msimamiaji mkuu wa fiscal policies na ndiyo msimizi mkuu wa sera za uchumi wa nchi. Fedha ya madafu mara nyingi inatumika kwa ajili ya kuonesha kuwa wale wanaosimamia uchumi wetu hawawezi - kutokana na kuwa hawawezi fedha yetu thamani yake inashuka kila wakati.

Rais ndo msimamiaji mkuu wa sera za uchumi na sera za fedha. Anapotumia slang ile ile ya mitaani, inaonesha ukosefu wa kuwajibika. Yaani rais haoni kuwa matendo yake kama rais ndo yanayosababisha fedha ya nchi iwe inayumba kila siku.

Kwa mfano; kwenye escrow tuliambiwa na Takukuru kuwa zilitolewa bilioni 73 taslimu. Matukio kama haya sera za kifedha haziyaruhusu yafanyike kwa maana kuwa hii ndo inasababisha kujaa kwa shilling kwenye mzunguko kunakofanya mfumko wa bei (inflation). Matukio kama EPA, ESCROW, n.k. ndo mambo yanayofanya fedha ya nchi ikose stability kwenye soko na kushuka haraka haraka.

Kauli kama ile kutoka kwa rais (kuita shillingi madafu) kunafanya vile vile wawekezaji wanaotoka nje ya nchi kukosa imani na fedha ya nchi na hivyo kusisitiza matumizi ya fedha za nje hata kwenye miamala (transactions) ambayo ingehitaji shillingi. Hii maana yake ni kuwa tunalazimika kutumia dola nyingi kwenye mfumo wa uchumi, wakati dola zinazoingia nchini ni kidogo. Hili huchangia kushusha thamani ya shilingi zaidi na kuifanya iendelee kuwa madafu zaidi na zaidi.

Kwa ujumla kauli hiyo ina madhara makubwa sana kwa uchumi wa nchi. Inawezekana wewe huwa huchukulii kwa uzito kauli za viongozi wako. Lakini ukae ukijua kuwa tuko kwenye mfumo wa kidunia ambapo kauli za viongozi zina thamani kama fedha. Kauli kama ile imeisababishia nchi ya Tanzania hasara ya mabilioni na rais kama mchumi jambo hilo ilitakiwa awe analijua sana. Wanaofanya speculation ambao ndo wanaoendesha uchumi wa dunia huangalia sana mwenendo wa uongozi wa nchi na viongozi wake.

Yaani kauli kama ile kuna hata wawekezaji walioisikia kauli ile wanaahirisha kabisa kuja kuwekeza Tanzania. Au mabenki yanayotoa mikopo kwa wanaowekeza Tanzania wakaongeza riba kutokana na kuongezeka kwa "risk profile" ya nchi. Haya ni mambo mazito kweli kweli, si mchezo mchezo na yana madhara ya moja kwa moja kwa nchi.

Kiongozi kama huyu, hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi kwa sababu haelewi ni kwa namna gani kauli zake zinaiathiri nchi.

Wawekezaji wanaangalia kona tofauti, kwa mfano wewe ukisema huwekezi nchi yenye vita, wengine kwao ni opportunity ndio maana hata Kongo kuna wawekezaji, Sudan kuna wawekezaji, kwa hiyo wakati mwingine siasa, vita, thamani ya fedha, matamshi ya rais, sio vikwazo kwa mwekezaji yeye anaangalia atapata nini akiwekeza. Afrika ya Kusini iliwekewa vikwazo wakati wa utawala wa kibaguzi lakini wako waliowekeza pamoja na vikwazo hivyo. Kwa hiyo neno "hela ya madafu" sio kikwazo kwa mwekezaji makini na inawezekana ikawa ni opportunity iliyosababishwa na weakness ya upande wa pili. Unaweza kulinganisha Yen na $? au Yuan na $? au Stg na $? au na UG.Shs? KSh. nk? Mbona nchi hizo zina wawekezaji?
 
Back
Top Bottom