Zamiluni Zamiluni
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 13,997
- 15,112
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/281346-kikwete-sijui-kwa-nini-nchi-yangu-ni-maskini.html..., pili hata Kikwete mwenyewe hajui kwanini hela yetu inashuka thamani kila uchwao. Kweli shule ni tatizo
Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.
Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.
Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?
Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
Mkuu, lazima awe dharau maana zile wanazokwapua zipp kwa dollar.
Ndio zile kauli za akina Chenge- vijisenti
= uhalisia
Mkuu,
Kwa nini unaita pesa yetu mkwanja, mapene, mpunga, dinyilu na kisu?. Huoni kama hii ni dharau kwa sababu kuna jina lake kisheria ambalo ni shilingi.
Kama hiyo siyo dharau, kwa nini kuita madafu ndiyo iwe dharau?
You're spot on Mkuu,Tatizo Watanzania wengi hatufuatilii mienendo ya kisiasa nje ya mipaka ya nchi yetu,Tungekuwa tunafuatilia masuala ya kisiasa katika nchi nyingine let's say America basi viongozi wazembe kama JK na wengineo si tu wangetawala katika mazingira magumu kwasababu ya Wananchi kupenda kuchambua na kupima kauli na mienendo yake ya kiutawala bali pia asingekuwa madarakani hii leo.Wenzetu kule kila kinachozungumzwa au kutendwa na kiongozi kinachukuliwa kwa umakini mkubwa na kina athari za aidha moja kwa moja au siyo moja kwa moja Kwenye mienendo ya masoko ya fedha,uwekezaji na kadhalika.Ila hapa Tanzania tunafanya mambo kwa mazowea tu,hii ndilo tatizo letu kubwa,Ndiyo maana Jumuiya ya Afrika Mashariki yaelekea kutushinda kwasababu wenzetu majirani wamejiwekea vision za maendeleo na standard za kiwango cha juu cha uwajibikaji wakati sisi tunafanya mambo yetu kiswahili Swahili.Tabu kweli kweli.Fedha ya Madafu kwa muktadha wa watumiaji wa mitaani ni fedha ambayo haina thamani. Fedha ambayo thamani yake inabadirika badirika mintarafu kushuka mara kwa mara. Ni nini kinachoshusha thamani ya fedha ya nchi? Ni hali ya uchumi wa nchi pamoja na sera za kiuchumi za serikali inayokuwa madarakani (fiscal policy).
Rais ndo msimamiaji mkuu wa fiscal policies na ndiyo msimizi mkuu wa sera za uchumi wa nchi. Fedha ya madafu mara nyingi inatumika kwa ajili ya kuonesha kuwa wale wanaosimamia uchumi wetu hawawezi - kutokana na kuwa hawawezi fedha yetu thamani yake inashuka kila wakati.
Rais ndo msimamiaji mkuu wa sera za uchumi na sera za fedha. Anapotumia slang ile ile ya mitaani, inaonesha ukosefu wa kuwajibika. Yaani rais haoni kuwa matendo yake kama rais ndo yanayosababisha fedha ya nchi iwe inayumba kila siku.
Kwa mfano; kwenye escrow tuliambiwa na Takukuru kuwa zilitolewa bilioni 73 taslimu. Matukio kama haya sera za kifedha haziyaruhusu yafanyike kwa maana kuwa hii ndo inasababisha kujaa kwa shilling kwenye mzunguko kunakofanya mfumko wa bei (inflation). Matukio kama EPA, ESCROW, n.k. ndo mambo yanayofanya fedha ya nchi ikose stability kwenye soko na kushuka haraka haraka.
Kauli kama ile kutoka kwa rais (kuita shillingi madafu) kunafanya vile vile wawekezaji wanaotoka nje ya nchi kukosa imani na fedha ya nchi na hivyo kusisitiza matumizi ya fedha za nje hata kwenye miamala (transactions) ambayo ingehitaji shillingi. Hii maana yake ni kuwa tunalazimika kutumia dola nyingi kwenye mfumo wa uchumi, wakati dola zinazoingia nchini ni kidogo. Hili huchangia kushusha thamani ya shilingi zaidi na kuifanya iendelee kuwa madafu zaidi na zaidi.
Kwa ujumla kauli hiyo ina madhara makubwa sana kwa uchumi wa nchi. Inawezekana wewe huwa huchukulii kwa uzito kauli za viongozi wako. Lakini ukae ukijua kuwa tuko kwenye mfumo wa kidunia ambapo kauli za viongozi zina thamani kama fedha. Kauli kama ile imeisababishia nchi ya Tanzania hasara ya mabilioni na rais kama mchumi jambo hilo ilitakiwa awe analijua sana. Wanaofanya speculation ambao ndo wanaoendesha uchumi wa dunia huangalia sana mwenendo wa uongozi wa nchi na viongozi wake.
Yaani kauli kama ile kuna hata wawekezaji walioisikia kauli ile wanaahirisha kabisa kuja kuwekeza Tanzania. Au mabenki yanayotoa mikopo kwa wanaowekeza Tanzania wakaongeza riba kutokana na kuongezeka kwa "risk profile" ya nchi. Haya ni mambo mazito kweli kweli, si mchezo mchezo na yana madhara ya moja kwa moja kwa nchi.
Kiongozi kama huyu, hafai kuendelea kuwa kiongozi wa nchi kwa sababu haelewi ni kwa namna gani kauli zake zinaiathiri nchi.
'Hela ya madafu' ni fedha yenye thamani ndogo,na kweli fedha yetu imeshuka sana thamani kwa sababu ya sera zake mbovu za kiuchumi na kifedha pamoja na ufisadi mkubwa unaoendelea kwenye fedha za umma.
TShs. 1 = Japannese Yen 0.071
TShs. 1 = Chinese Yuan 0.00366520
Fedha ya Madafu kwa muktadha wa watumiaji wa mitaani ni fedha ambayo haina thamani. Fedha ambayo thamani yake inabadirika badirika mintarafu kushuka mara kwa mara. Ni nini kinachoshusha thamani ya fedha ya nchi? Ni hali ya uchumi wa nchi pamoja na sera za kiuchumi za serikali inayokuwa madarakani (fiscal policy).