Wawekezaji wanaangalia kona tofauti, kwa mfano wewe ukisema huwekezi nchi yenye vita, wengine kwao ni opportunity ndio maana hata Kongo kuna wawekezaji, Sudan kuna wawekezaji, kwa hiyo wakati mwingine siasa, vita, thamani ya fedha, matamshi ya rais, sio vikwazo kwa mwekezaji yeye anaangalia atapata nini akiwekeza. Afrika ya Kusini iliwekewa vikwazo wakati wa utawala wa kibaguzi lakini wako waliowekeza pamoja na vikwazo hivyo. Kwa hiyo neno "hela ya madafu" sio kikwazo kwa mwekezaji makini na inawezekana ikawa ni opportunity iliyosababishwa na weakness ya upande wa pili. Unaweza kulinganisha Yen na $? au Yuan na $? au Stg na $? au na UG.Shs? KSh. nk? Mbona nchi hizo zina wawekezaji?