Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Ni Kweli alichosema Rais wetu kuwa Pesa ya Tanzania ni Pesa ya Madafu mimi huwa ninaita Shilingi ya Tanzania ni Pesa ya machungwa sasa angalia machungwa na madafu ipi zaidi Mkuu Kinyungu Pesa ya Tanzania ingelikuwa na thamani mbona tungelikuwa tumekwisha kuendelea kimaendeleo.Lakini pesa yetu ya Machungwa haina thamani tutaendelea kivipi? Viongozi wetu wengi wao ni Mafisadi na Wala Rushwa tutaweza kweli kuwa na maendeleo? Rais ana haki kusema Pesa ya nchi yake ni pesa ya Madafu haina thamani ndani na nje ya nchi mimi pia nina muunga mkono Mheshimiwa Rais JK..

Hata kwenye huu ujinga uko na JK, hii ni zaidi ya mahaba niue.
 
Jaji Warioba aliongelea kumheshimu rais kwa sababu urais ni alama ya taifa.

Fedha za taifa ni alama nyingine ya taifa.

Inapotokea alama moja ya taifa (rais) inaidhalilisha alama nyingine ya taifa (fedha), inabidi tujiulize kama wanaomdhalilisha rais wanafanya makosa kweli au wamechoshwa na ukosefu wa nidhamu, staha na ujuzi unaoonyeshwa na rais kiasi cha kufanya watu waweke pembeni habari za Jaji Warioba za "rais ni alama ya taifa" na kumnanga JK tu.

Waingereza wanasema "Respect is earned", Waswahili wanasema "Jiheshimu uheshimike".

Rais anayeiita fedha ya nchi yake "hela ya madafu", anategemeaje kuheshimiwa?

Ni mtanzania mjinga tu anaeweza kumheshimu huyu muhuni
 
Pamoja na madhaifu yote ye JK kuhusu sakata la Escrow, mwenzenu natatizwa na upeo na uzalendo wa mkuu huyu jamani.

Kuiita fedha halali ya nchi yako "madafu" ni kuidhalilisha nchi yako mwenyewe. Hivi nani aanze kuithamini fedha yake kama mkuu wa nchi? Na je mgeni akija akachukua fedha ambayo mkuu anaiita madafu akaenda chooni na kuchambia atakuwa ametenda kosa?

Tunaimbishwa kupenda vya kwetu, but unapoanza kutumia lugha ya ku-dunisha kilichochako nani akipende? Tumeimbishwa methali ya kuwa "ziwa la mama ni tamu hata kama ni la mbwa". Misemo kama hii kaka yetu amesahau kabisa.

Najuta kumfahamu...
 
Jaji Warioba aliongelea kumheshimu rais kwa sababu urais ni alama ya taifa.

Fedha za taifa ni alama nyingine ya taifa.

Inapotokea alama moja ya taifa (rais) inaidhalilisha alama nyingine ya taifa (fedha), inabidi tujiulize kama wanaomdhalilisha rais wanafanya makosa kweli au wamechoshwa na ukosefu wa nidhamu, staha na ujuzi unaoonyeshwa na rais kiasi cha kufanya watu waweke pembeni habari za Jaji Warioba za "rais ni alama ya taifa" na kumnanga JK tu.

Waingereza wanasema "Respect is earned", Waswahili wanasema "Jiheshimu uheshimike".

Rais anayeiita fedha ya nchi yake "hela ya madafu", anategemeaje kuheshimiwa?
Thank you Sir!
 
Mimi naogopa sana! Ipo siku Rais ataita State house kama Guest house

Watetezi watakuja na kusema hiyo ni tafsida.
 
Pamoja na madhaifu yote ye JK kuhusu sakata la Escrow, mwenzenu natatizwa na upeo na uzalendo wa mkuu huyu jamani. Kui ita fedha halali ya nchi yako "madafu" ni kuidhalilisha nchi yako mwenyewe. hivi nani aanze kuithamini fedha yake kama mkuu wa nchi? na je mgeni akija akachukua fedha ambayo mkuu anaiita madafu akaenda chooni na kuchambia atakuwa ametenda kosa? tunaimbishwa kupenda vya kwetu, but unapoanza kutumia lugha ya ku-dunisha kilichochako nani akipende?. tumeimbishwa methali ya kuwa "ziwa la mama ni tamu hata kama ni la mbwa". misemo kama hii kaka yetu amesahau kabisa. najuta kumfahamu...
Shedaaa,,,,,,,,
 
Attachments

  • IMG-20141222-WA0012.jpg
    IMG-20141222-WA0012.jpg
    64.9 KB · Views: 187
Mwenye nyumba anaidharau nyumba yake,sijui majirani wanamuonaje?
 
Ashike adabu yake. Pumbaaf kabisa! Rais mzima runnin' his mouth in state kwa style hii ya kijiweni ni aibu.
 
kwa mkuu wa nchi kusema neno kama hili whether anasema akichekacheka ama la inathali kiuchumi na katika ulimwengu wa roho! ni kuishusha dhamani ni kuilaani shilling yetu!
 
Mimi naogopa sana! Ipo siku Rais ataita State house kama Guest house

Watetezi watakuja na kusema hiyo ni tafsida.

MKULU alipoana wazee wa darisalama(dar es salaam),hawacheki hawatabasamu,wanamuangalia tu,akaona labda akisema ela za madafu watapiga vigeregere,kumbe ndo anaharibu zaidi
 
MKULU alipoana wazee wa darisalama(dar es salaam),hawacheki hawatabasamu,wanamuangalia tu,akaona labda akisema ela za madafu watapiga vigeregere,kumbe ndo anaharibu zaidi

Unaweza kusema kama utani, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ana tabia ya kupepesa macho sana akijiona ana audience fulani hivi.

Ukitaka kuhakikisha tafuta hotuba aliyomjibu George Bush kumkaribisha, sehemu ya majibu na maswali umuone anavyojifaragua mpaka kusema anakuwa kama anashindwa hivi.
 
kwa mkuu wa nchi kusema neno kama hili whether anasema akichekacheka ama la inathali kiuchumi na katika ulimwengu wa roho! ni kuishusha dhamani ni kuilaani shilling yetu!

Katika nchi zinazoangaliwa uchumi duniani, rais kuiita hela yake hela ya madafu inaweza kuishusha hiyo hela thamani kiukweli kwenye money markets huko kutokana na speculators wanachoweza kusema "a display of lack of confidence from the very president of the country".
 
Mkuu aliteleza kidogo jamani hakuwa na maana mbaya
 
Ukitaka kuhakikisha tafuta hotuba aliyomjibu George Bush kumkaribisha, sehemu ya majibu na maswali umuone anavyojifaragua mpaka kusema anakuwa kama anashindwa hivi.

Hii?

Halafu cheki 10:11....Bush alikuwa ananifurahisha sana.

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom