The mountain lion
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 1,153
- 418
Fedha ya nchi yako unaidharau halafu ukizingatia yeye ndo President hajui kwamba hiyo aibu ni yake na inaonyesha wazi kwamba kuna jambo halipo sawa kwenye uchumi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
aisee kama nimeandika vibaya samahani sana, huwa sipendi lugha za kebehikama aliteleza mbona hakuanguka na wewe acha tabia za kutumiwa kama toilet paper
Rais kwa maneno yako inaonyesha ni jinsi gani usivyopenda nchi na watu wake huna hata chembe ya uzalendo kwa kejeli.
Mimi sioni tatizo lolote kwa sababu haliondoi ukweli na halileti athari yoyote katika uchumi.
Mbona maneno ya utani au wakati hata UK wanaita utawasikia wanaita pesa yao majina kama quid, nicker, bin lid, vile vile hata Wamarekani wanaita pesa yao majina kama bucks.
Kwanza tujue chanzo cha jina hili "fedha ya madafu". Haya ni maneno ya mtaani. Kwa mfano jina "daladala" sasa
hivi ni jina la kawaida kwa mabasi madogo na imehamia mpaka magari makubwa yanayosafirisha abiria wa mjini na vitongoji vyake. Nakumbuka chanzo chake ni miaka ya 80 kulikuwa na vibasi vidogo hiace, town ace na namna yake ambavyo vilikuwa vikichukua abiria kwa kuiba (sio rasmi) kutoka Magomeni mpaka Posta na kwa kutumia njia zisizo rasmi na nauli ilikuwa ni Sh.5/= ambayo ndio ilikuwa ni sawa na Dola moja, na wakati huo UDA nadhani nauli ilikuwa ni Shs. 2/=. kwa hiyo wapiga debe wake walikuwa wakisema daladala badala ya Shs. tanotano kuzuga vyombo vya sheria. Kuna neno "Bodaboda" nalo asili yake ni maeneo ya mipakani ambapo pikipiki zilikuwa zikitumika kuvusha watu toka nchi moja kwenda nyingine kwa njia zisizo rasmi ambazo pia zimepachikwa jina" njia za panya". Yako maneno mengi ya aina hiyo mengine yanadumu na mengine yanapotea hizi ndio tabia za lugha. "Fedha ya madafu" chanzo chake ni fedha yetu (Shilingi) iliitwa hivyo miaka hiyo ambapo ilikuwa inaweza kutumika nchini tu ikimaanisha utaitumia kununua madafu ambayo yanapatikana hapa hapa na huhitaji fedha ya kigeni kuyapata. Watu walikuwa wanataka sana kumiliki fedha za kigeni km $ au Stg. ikawa ni sababu ya kushuka kwa thamani ya fedha yetu na hali ya uchumi ikichangia.
Je rais hawezi kutumia neno bodaboda? au daladala? au njia za panya? au Lumbesa? Ninachoweza kusema ni kwamba Raisi ametumia neno lililoanza kupitwa na wakati kwani kwa sasa unaweza kupata fedha za nje kwa manunuzi halali bila matatizo, na ndio maana mwekezaji aliweza kuwekewa malipo yake kwa fedha za Kitanzania. ALIKUWA SAHIHI KUTUMIA NENO HILO.
Nilimwandikia Mh. Rais waraka wa kuleta maadili mema nchini ambapo ingekuwa mwanzo mpya kama utasoma kwa ukamili attachment katika habari zangu ndani ya JF yenye kichwa MH. KIKWETE MTIKISIKO WA 4 KULIKUMBA TAIFA.
Ndani ya waraka huo wa tarehe 27/10/2012 ushauri nilioshauri utangazwe na rais ni: (Nanukuu hapa chini)
1. NJIA YA KULETA AMANI NA UTENGAMANO WA TAIFA
Mungu wa Kweli Yehova anaagiza kuwa: Ukiwa Rais na kabineti yako ya utawala na ushauri; kwa pamoja mpitishe azimio la kusamehe na kufuta kesi zote ambazo zinahusikana na migogoro ya kidini, kisiasa, uhujumu uchumi, ufisadi, migomo ya wafanyakazi, wanafunzi na hata kesi ambazo zinakabili watu ambao wamehusika katika migogoro ya kikabila na ardhi. Mungu akimaanisha watu watakao husika katika zoezi hili la kusamehewa ni katika kesi ambazo zinasimamiwa na Jamhuri siyo katika kesi zinazohusisha mtu na mtu. Pia, msamaha utahusika kwa wale wote ambao tayari wanatumikia vifungo kwa sababu ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu, wanapaswa kufunguliwa na kuwekwa huru. Kisha, utoe tamko kwamba serikali itapitisha sheria kali hivi karibuni kwa wote watakaotenda au kusababisha matatizo mapya yaliyotajwa hapo juu.
MWAROBAINI WA KUKOMESHA MATATIZO HAYO HAPO JUU UNATOLEWA NA MIFANO MIWILI INAYOPATIKANA KATIKA BIBLIA:
i). Andiko la Luka 19:2-10 linalosema: Sasa kulikuwa na mwanaume anayeitwa Zakayo; naye alikuwa mkuu wa wakusanya kodi, na alikuwa tajiri. Basi, alikuwa akitafuta kuona Yesu huyu ni nani, lakini hangeweza kwa sababu ya umati, kwa sababu alikuwa mfupi. Kwa hiyo akakimbia mbele na kupanda mforsadi-tini kusudi amwone, kwa sababu alikuwa karibu kupitia njia hiyo. Sasa Yesu alipofika hapo, akatizama juu na kumwambia: Zakayo, shuka haraka, kwa maana leo lazima nikae katika nyumba yako. Ndipo akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa shangwe. Lakini walipoona hilo, wote wakaanza kunungunika, wakisema: Ameingia apate kukaa pamoja na mwanamume mtenda-dhambi. Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana: Tazama! Nusu ya mali zangu, Bwana mimi nitawapa masikini, na chochote nilichomnyanganya mtu yeyote kwa shitaka la uwongo nitarudisha mara nne. Ndipo Yesu akamwambia: Leo wokovu umekuja kwenye nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Abrahamu. Kwa maana Mwana wa Binadamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.
ii). Pia, andiko la 2Wafalme 6:15-23 linasema: Wakati mhudumu wa yule mtu wa Mungu wa kweli (Elisha) alipoamka asubuhi na mapema, akaenda nje, na, tazama, hapo jeshi lilikuwa limelizunguka jiji kwa majeshi na magari ya vita. Mara moja mtumishi wake akamwambia: Ole, bwana wangu! Tutafanya nini? Lakini yeye akasema: usiogope, kwa maana wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Na Elisha akaanza kusali na kusema: Ee Yehova, tafadhari fungua macho yake, ili aone. Mara moja Yehova akafungua macho ya yule mtumishi, hivi kwamba akaona; na, tazama! Lile eneo lenye milima lilikuwa limejaa farasi na magari ya vita ya moto kumzunguka Elisha pande zote.
Walipoanza kushuka kumwendea, Elisha akaendelea kusali kwa Yehova na kusema: Tafadhali, lipige taifa hili kwa upofu. Basi yeye akawapiga kwa upofu kulingana na neno la Elisha. Sasa Elisha akawaambia: Hii siyo njia, na hili silo lile jiji. Nifuateni, na acheni niwaongoze kwa yule mtu mnayemtafuta. Hata hivyo akawaongoza kwenda Samaria.
Na ikawa kwamba mara walipofika Samaria, ndipo Elisha akasema: Ee Yehova, fungua macho yao waone. Yehova akafungua macho yao mara moja, nao wakaona; na, tazama, walikuwa katikati ya Samaria. Sasa mfalme wa Israeli akamwambia Elisha mara alipowaona: Je, niwapige, je, niwapige, baba yangu? Lakini akasema usiwapige. Je, unawapiga wale ambao wewe umewachukua mateka kwa upanga wako na upinde wako? Weka mkate mbele yao ili wale na kunywa, waende kwa bwana wao. Basi akawaandalia karamu kubwa; nao wakaanza kula na kunywa, kisha akawaacha, wakaenda zao kwa bwana wao. Na vikundi vya waporaji vya Wasiria havikurudi tena hata mara moja katika nchi ya Israeli.
Kwa hiyo maandiko yote mawili yana maana kubwa au mfano mkubwa kwa makundi yote ambayo yametajwa hapo juu ambayo yatapata msamaha wa serikali. Ni kwamba Yehova ametoa agizo la msamaha kwa sababu msamaha huo utawahukumu wahusika katika nafsi zao; kwa sababu watakapokuwa wakifikiria rehema walizotendewa, hawatarudia makosa yao ya zamani. Ndivyo alivyofanya Zakayo baada ya kumkaribisha Yesu alijisikia hatia juu ya ufisadi na rushwa alizokuwa akipokea naye akaahidi kuwalipa aliowadhurumu, kusaidia masikini n.k. Vivyo hivyo msamaha ambao serikali imetoa kwa watuhumiwa utawafanya wahusika kuwa watu wazuri katika jamii ili kulipia matendo waliyosababisha na itachochea jamii kuchukia matendo hayo. Na katika mfano wa pili, tunaona Wasiria waporaji baada ya kufanyiwa matendo mema badala ya mabaya; walipata somo kubwa sana na hawakurudi tena kuwasumbua Waisraeli, hii, ikiwa ni sehemu ya kulipia matendo mema waliyotendewa badala ya mabaya.
HITIMISHO: Ushauri huu ungefuatwa 2012 kusingekuwa na ufisadi wa Escrow au ufisadi mwingine