Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Acha uongo tunaposema hela Ya madafu ni hela ndogo ndogo isiyokuwa na thaman

mzeelapa utakuwa mzazi wa ajabu sana kubariki jina la kebehi kwa mwanao, eti kwa sababu mitaan wanamwita fara na ww mzazi unamwita fara,shame upon u. Kama kiongozi alitakiwa kutotumia neno hilo ukizingatia alikuwa anasikilizwa ndani na nje ya tz, kiuchumi si afya wabunge wanapigania malipo yote yafanyike kwa Tsh halafu yeye publically anaita hela ya madafu.mzazi anabariki jina lisilorasmi kwa mwanae. kwa sababu hamjui athari zake kiuchumi mnaona sawa tu.msumbiji,malawi,uganda,zimbabwe etc wana hela haina thamani kabisa lkn huji kusikia kiongozi wao anaita hela yake kwa majina anayotumia kiongoz wenu wa kijiweni.
 
Kuepuka informality mzee wa ukweli na uwazi alikuwa anasoma hotuba zake. Hotuba inatakiwa iwe formal bwana! !
 
Mh Rais pamoja na yoote uliyo yaeleza ktk mkutano wako na wazee wa dar, mimi sikukuelewa ulipo iita pesa ya nchi yako kuwa ni fedha za madafu... Duuh.
 
Mh Rais pamoja na yoote uliyo yaeleza ktk mkutano wako na wazee wa dar, mimi sikukuelewa ulipo iita pesa ya nchi yako kuwa ni fedha za madafu... Duuh.

Anamaanisha kwamba wao huwa wakipiga deal kama ya Escrow huwa hela inakuwa in terms of $ not Tshs a.k.a madafu
 
waswahili wana madharau sana na sisi tutaendelea kuwadharau
 
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.

Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?

Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
Hela ya madafu ni hela inaayonunua vitu vya hapa hapa tz haivuki mpaka. Maana pana si chochote mbele ya hela zingine kama dola.
mtoa hoja anaobainisha kuwa si vizuri kwa rais wa nchi kuidharau fedha yake mwenyewe na pia kimsingi kabla mtu hajapato dola ni lazima kwanza apate shilingi kutokana na mali aliyopata kisha shilingi hizo zitabadilishwa kuwa dola au nyingine yoyote ili mtu huyo anunue bidhaa kutoka nje.
sasa wakenya, wachina wasauz n.k wanaweza kuziita hela zao hela za madafu?
 
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.

Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?

Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.

Zamani nilikua najua watu walioko ng'ambo au waliowahi kuishi au kusoma ng'ambo wana akili sana, nilipogundua kua hata wewe ulaya unakufahamu huko, nikabadiri mawazo yangu fasta.
 
Watanzania acheni fikra potofu. Ki msingi Wakenya ndio walioanza kuiita hela ya Tanzania ya madafu kwa sababu thamani yake ilikuwa chini kupita yao tena enzi za Nyerere, Na kipindi hicho hata pesa ya Uganda ilikuwa juu kabla ya vita ya Kabera ndio ikaporomoka. Kama umeishi Kenya hilo ni jina maarufu tu kwa ela ya Tanzania
 
Nimemsikiliza rais Jakaya Kikwete (JK) jana na hotuba yake ya kujibaraguza mbele ya Watanzania. Sikutegemea jipya kwenye story zake za jana na wale Wazee wa vijiwe vya CCM ila hili la yeye kama rais wa nchi kudharau sarafu ya nchi yake mwenyewe hadharani limenisikitisha sana.

Ni ajabu sana kwa rais wa nchi kwenda mbele ya vyombo vya habari kukiwa na halaiki ya watu na kuiita bila haya wala aibu sarafu ya nchi kwa jina la kebehi kuwa eti ni "hela ya madafu" halafu anaachwa tu hakuna kitakachompata. Hii ni fedheha na dharau ya hali ya juu kwa sisi ambao hela hiyo ya 'madafu' ndio mshahara wetu na fedha yetu ya kufanya biashara kila siku.

Tunajua mmeiba sana na tena mkishaiba chap chap mnazibadilisha kuwa dollar hivyo haya "madafu" hata yawe sawa na toilet paper (karatasi za kuchambia) kwenu sio issue. Itakuwa ajabu sana kama nikimsikia tena waziri wa fedha na uchumi akisisitiza wafanyabiashara hasa Wahindi ambao wanajua sana umuhimu wa dhamani ya fedha wasiuze bidhaa zao kwa dollar maana hela wanayoambiwa watumie hata mkuu wa nchi anaiona haina maana yoyote zaidi ya kuwaweza kununulia tunda la bei duni la aina ya madafu.

Rais anatakiwa aelewe kuwa kauli zake za namna hii tena anazozitoa hadharani zina madhara ya moja kwa moja kwa uchumi wetu na achunge sana kauli zake anapozungumza masuala muhimu ya nchi hadharani. Kama ni kutudharau kesha fanya hivo sana lakini atuache basi na hii sarafu yetu ambayo kila kukicha anafanya mbinu za kuishusha dhamani. Kudharau sarafu ya nchi hadharani tena mchana kweupe na mtoa dharau akiwa ndie rais wa nchi inatakiwa liwe kosa la uhujumu uchumi na JK anapaswa kushitakiwa kwa hili.

Tumekuvumilia kwa mengi JK lakini kwa kuifananisha sarafu yetu na madafu umevuka mipaka. Bora ungeiita hivyo ukiwa chumbani kwako au ukisha acha nafasi yako ya urais. Ni kwa sababu unaongoza nchi yenye mifumo mibovu ya sheria inayokulinda laiti ingelikuwa nchi nyingine kauli yako hiyo ingetosha wewe kujiuzulu ukachunge mbuzi wako kule Msoga.

Mwana JF hebu piga picha nini kitampata rais Baraka Obama wa Marekani kama siku atakwenda hadharani kukiwa na vyomba vya habari na kutamka maneno ya dhihaka kwa dollar kama alivyofanya rais Jakaya Kikwete jana pale ukumbi wa Diamond Jubilee. Jibu nadhani unalo mwenyewe mwana Jf.

Wasalaam,
Kinyungu.

Kwani Bwashee hujui kuwa strength ya pesa yoyote duniani ni internal purchasing power? Je ungesemaje endapo rais angeiita hela ya sukari?
 
Watanzania tukome kuwapa watu wa pwani Urais, hawa watu asili yao ni uvivu na kukaa vijiweni, hata jana pale Diamond kilikuwa ni kijiwe cha wazee/waswahili wa Dar wasiojitambua. Mambo kama hayo mimi sikuona kulikuwa na haja gani ya kuweka kijiwe, ilikuwa ni kuchukua hatua basi

Hiyo ni kashfa, we unawajua waliomnunulua JK Nyerere Baiskeli ili imsadie kufanya kazi za Chama? Unawajua waliompinga mkoloni kwa kutumia maji maji !unamkumbuka Chifu mkwawa wa Iringa ,punguza Zarau.unadhani wavaa mlegezo wangeweza kupigana na mkoloni?.

Wakati wr wa bara unawakumbatia hawa wazungu wapwani walikuwa wanapambana nao japo kwa zana duni.
 
Ulitaka Rais aseme kitu gani zaidi ya hivyo alivyosema? Shilingi ya Ki-Tanzania ni pesa ya Madafu Au Pesa ya Machungwa haina thamani kokote pale duniani. Wewe Fananisha Shilingi ya Ki-Tanzania na Shilingi ya Ki-Kenya ipi Pesa yenye Thamani? Mkuu SoNotorious Amka acha mapenzi ya kupenda kitu kwako hakina thamani ili mradi unakipenda utapenda umasikini eti ukiulizwa mzee wangu pia alikuwa ni masikini changamka kuondo wa umasikini nyumbani kwako .

hapo kwenye nyekundu si kweli mbona KILA SIKU tunaitumia kufanya manunuzi kama haina thamani kokote duniani ? mwambie a-phase out tzs tutumie US dola kama Zimbabwe yeye si ndiye Rais.
 
hapo kwenye nyekundu si kweli mbona KILA SIKU tunaitumia kufanya manunuzi kama haina thamani kokote duniani ? mwambie a-phase out tzs tutumie US dola kama Zimbabwe yeye si ndiye Rais.
Nikisema Pesa ya Ki-Tanzania Shilingi Haina Thamani popote pale Duniani nina maanisha inatumika nchini mwetu lakini nje ya

Tanzania Shilingi haina thamani wewe jaribu kufananisha Shilingi Kenya na shilingi ya Tanzania ipi pesa yenye Thamani?

Ukweli mara nyingi huwa unauma Ndio Maana Mheshimiwa Rais JK Amesema kuwa Pesa ya Tanzania yaani

Shilingi ni Pesa ya Madafu mimi huwa ninaita Pesa ya Shilingi ya Ki-Tanzania ni Pesa ya Machungwa.

Thamani yake ni Pesa ya Ki-Tanzania ni kununuwa Machungwa na Madafu tu. Mkuu SoNotorious Amka Wa-

Danganyika amkeni jamani. acheni usingizi. Ninatabiri- Baada ya Miaka 10 ijayo Tanzania shilingi itakuwa

kama Pesa ya Zimbabwe Dollar.

  1. [TABLE="width: 515"]
    [TR]
    [TD][TABLE="width: 254"]
    [TR]
    [TD]1 Kenyan Shilling equals
    19.05 Tanzanian Shilling
    Disclaimer

    [TABLE="width: 515"]
    [TR]
    [TD]
    chart
    [/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]
    [/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]
    [/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]

Chanzo.Convert Kenyan Shillings (KES) and Tanzanian Shillings (TZS): Currency Exchange Rate Conversion Calculator
 
Samahani kama nitakuwa nimekukosea MziziMkavu naomba kujua elimu yako ya kidunia ni ya kiwango gani ? Je umesoma uchumi na masuala ya kifedha ? Ni kwa nini thamani ya shilingi inashuka ? na JK kama Rais amefanya jitihada gani za makusudi za kupandisha thamani ya shilingi ? Je unajua ufisadi wa EPA na ESCROW amabao JK ndiye sterling wake umeshusha thamani ya shilingi yetu kwa asilimia ngapi ?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo ni kama wewe uambiwe "una degree ya chupi" - yani ni tusi na dharau inayoonyesha kwamba kisomo chako hakina thamani! Hivyo ndio kusema kwamba: "Pesa za madafu" maana yake ni pesa zisizo na thamani!

Kwa hiyo anaongoza nchi ambayo fedha yake haina thamani? Anailingajisha fedha ya nchi yake na.nchi gani? Na je, ni kwa nini fedha ya nchi yake haina.thamani? Dah! Rais wetu kiboko.
 
Wadau nimewaza sana kwamba, Kwa nini Shilingi ya Tanzania inaporomoka thamani yake kila kukicha mwaka hadi mwaka, ukilinganisha na Fedha za kigeni kama USD, Euro, Pound n.k.
Pamoja na sababu nyingine nimejikuta nashangazwa sana na Kauli za Mkuu wa nchi,
Kauli zenyewe ni kama:-
1. Shilingi ya Tanzania ni Fedha ya Madafu (JK)
2. Tusipoomba misaada nje tutagawana Mihogo tu! (JK).
Kwa kauli hizi mbili tu, tunapata Picha kwamba Mhimili Mkuu yaani Serikali yenyewe haina Utashi Imara wa kisiasa na dhamira ya kweli ya kukuza Uchumi wa nchi, ambavyo vyote viwili ni muhimu katika kujenga thamani halisi ya Fedha!
Nawasirisha!
 
Mkuu nakuunga mkono, kwa wasiojua madhara ya kauli hizi kiuchumi watabeza wakidhani ni kauli za kawaida tu. Hili ni tatizo tena kubwa la kiongozi wetu kuingiza utani kwenye mambo ya msingi.

Ingawa fedha yetu imekuwa ikiporomoka hasa kwa mwaka huu, kwa siku mbili tu tangu siku Jk aliposema pesa yetu ni ya madafu shilingi ilishuka kwa sh. 26 ambayo ni sawa na asilimia 1.5, kiwango hiki cha kushuka ni kikubwa sana kwa nchi changa kama yetu.
 
Samahani kama nitakuwa nimekukosea MziziMkavu naomba kujua elimu yako ya kidunia ni ya kiwango gani ? Je umesoma uchumi na masuala ya kifedha ? Ni kwa nini thamani ya shilingi inashuka ? na JK kama Rais amefanya jitihada gani za makusudi za kupandisha thamani ya shilingi ? Je unajua ufisadi wa EPA na ESCROW amabao JK ndiye sterling wake umeshusha thamani ya shilingi yetu kwa asilimia ngapi ?

Aisee we jamaa una akili kishenzi. Mimi nilianzisha uzi kama huu nikasema Rais amekosea kusema kwa status yake kama kiongozi wa inchi na mtu anaepaswa kusimamia uchumi wa inchi hii. Yeye ndie anaepaswa kuongoza juhudi za kupandisha uchumi wa inchi hii na kama Rais anatakiwa kuongea vitu ambavyo ni formal sio kuchukua maneno ya mtaani na kutuwekea kwenye hotuba yenye maswala nyeti ya inchi kama ile. Ngoja nikuletee hoja zangu kwenye thread hiyo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom