Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?



Mimi Pia nina muunga mkono Rais Jk Kuita Shilingi taTZ ni Pesa ya Madafu kwa sababu Tanzania hakuna Viongozi wa Serikali wanaojali Maslahi ya Wananchi Viongozi karibu wote ni wabinafsi wanaojali Maslahi yao na Familia yao hawajali walala hoi. mimi pia ninaita Shilingi ya Tz ni Pesa ya Machungwa sio Madafu tu.


Yeye mwenyewe ndiye anaeifanya kuwa dafu kila siku anamwaga biillions of easy money mtaani kupitia ufisadi unaomfaidisha yeye na familia yake. Taifa limekuwa la kichuuzi mwingine anauza bidhaa za forever mwingine bidhaa za china. Wapi shilinhi itaimarika kwa Rais kama huyu ?
 
Last edited by a moderator:
Kwa masikio yangu wakati Jk anaongea na wazee wa dar, alipokuwa anaitetea IPTL, alisema zile fedha zilikuwa katika dollar, lakini zilipobadilishwa katika madafu....hela za tanzania ndo zikawa hizo billioni.

Kwa akili yangu ndogo nikuwa Rais inabidi aitetee fedha ya nchi yake kadri awezavyo. Lakini president mwenyewe akaziita madafu. Inakuwaje.
 
Mkuu alipitiwa, pengine baada ya kuona ngoma imekuwa ngumu na hivyo akapoteza focus. Kweli hata mimi siwezi kuiita pesa yetu tena mbele ya jamii ya kitaifa na kimataifa kama Rais alivyofanya.
 
Alikosea kwa kweli hata mumtete vipi......kati ya viapo vyake ni kuilinda nchi hii kadri anavyoweza
 
Wadau Nimekua Nikijiuliza Hili Neno Lina Maana Gani?Maana Ni Mara Kadhaa Nawasikia Wanasiasa Wakilitumia. Wengi Wetu Hua Tunafikiria Kama Si Neno La Kawaida Ivi. Pengine Kama Ni La Kibiashara Wachumi Mtatuambia, Kama Ni La Kisiasa Tulifahamu, Ama Wataalam Wa Kiswahili Mtusaidie.
 
Hili ni neno la dharau na dhihaka kwa pesa ya nchi kwamba haina thamani ya kufanyia biashara ya maana zaidi ya kununulia madafu. Kwa wenzetu ni sawa na kusema useless paper au toilet paper. Sasa kama kiongozi ambaye matendo yake yamechangia kuikosesha thamani pesa hiyo kisha anaidharau, huyo anatakiwa ajitathmini kisha achukue hatua zinazostahili.

Kumbuka pesa ni moja ya vitambulisho vya taifa lolote lile, vitambulisho vingine vya taifa ni kama Wimbo wa Taifa na Bendera. Sasa mtu akidharau vitu hivi na ni kiongozi wa nchi bado anafanya nini kwenye ofisi ya umma?
 
Ni hela za madafu maana walibeba kwa Magunia, viroba, sandarusi na mafuso siku nzima. Ingelikuwa ni US dollars hata gunia moja lisingejaa
 
Ni hela za madafu maana walibeba kwa Magunia, viroba, sandarusi na mafuso siku nzima. Ingelikuwa ni US dollars hata gunia moja lisingejaa

Taratibu Mkuu! Usijibu Kwa Jazba, Tunahitaji Kujua Maana.
 
Mara kadha tulimsikia rais mstaafu mh. Kikwete akiita pesa ya Tanzania kuwa ni pesa ya madafu, kwa kweli nilikuwa naumia sana, nilikuwa naumia kwa kuwa nilikuwa najua madhara ya rais kudharau thamani ya pesa ya nchi yake na nafikiri tunaiona mwishoni mwa kipindi chake. Watu wanalipana kwa dora au Euro na si shilingi tena.
Magufuli usije ukafanya haka ka mchezo, pesa yetu ina thamani sana kama ikithaminiwa na kuheshimiwa
 
Asee yule jamaa sijui alikuwaje, kumbe tuliokuwa tunashangazwa tulikuwa wengi!!?
 
Hilo likuwa ni kuongozwa na wacheza segere na taarabu. Mwisho wake nchi imekuwa shamba la bibi kila mtu aliyeona ya kukwapua anakwapua tu
 
Mwacheni mswahili wa watu aendelee kupokea tuzo na kutambulisha makamo wa raise.
 
Apige marufuku mauzo yote ndani ya nchi kufanywa kwa hela za kigeni. Hilo litasaidia sana kuipa thamani pesa yetu. Kwasasa wafanyabiashara wanauza kwa pesa za kigeni hata kwa vitu vya kawaida. Pia kodi za nyumba baadhi ya wenye nyumba wanalipwa kwa dola na mahotelini
 
Khaa!! Jamani nyie wakimbizi nini? Hicho ni kiswahili safi kikiwa na maana pesa ya ndani ( local currency). Sasa Kama mnashindwa hata kuelewa maana ya pesa ya madafu basi idara ya uhamiaji inahusika :mvutaji:
 
Back
Top Bottom