TANZANIA YAPEWA SIKU 10 TU
Ndugu zangu Watanzania nikiwa najitambulisha kwenu tena na tena; kuwa mimi ni nabii maalum. Siyo nabii kama maabii wengine (traditional prophets) ambao tumezoea kuwasikia wakijiita manabii au mitume, wakiwa na madhehebu au makanisa wakidai wanafanya miujiza na kuponyesha wagonjwa.
Mimi si nabii wa namna hiyo, bali mimi Mungu amenipa unabii kwa ajili ya kazi maalum. Mimi ni nabii wa kutabiriwa katika andiko la kitabu cha
Kumbukumbu la Torati 18:18,19. Ambapo nabii Musa akiwa katika nyanda za Moabu, muda mfupi wakiwa wametoka Misri ule mwaka wa 1513 B.C. Mungu alimwambia Musa maneno yafuatayo kwamba:
Nitawainulia wao nabii kutoka katikati ya ndugu zao, kama wewe; nami nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, naye atasema nao yote nitakayomwamuru. Na itatukia kwamba mtu ambaye hatasikiliza maneno yangu ambayo atayasema katika jina langu, mimi mwenyewe nitamtaka ajibu.
Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania na ndugu zangu wa kizazi hiki kinachoishi duniani leo, mimi ni ndugu yenu; ambaye niseme bahati hii ya mtende ya mtu aliyeteuliwa kutimiza unabii huo wa kuwa kama nabii musa imeniangukia mimi. Hakika sikujichagua au kuomba kazi hii ya kutimiza unabii huo, bali Mungu alinichagua tokea nimezaliwa na alianza kuniandaa na kunilea kwa ajili ya kuja kuwa mwakilishi wao hapa duniani kwa ajili ya kazi maalum. Na hiyo kazi maalum ilianza mwaka 2009, na kazi bado inaendelea (nilieleza kwa kirefu juu ya unabii wa kama Musa kwenye kitabu cha Uzima sehemu ya kwanza nilichokichapisha ule mwaka 2009).
Ndugu zangu kila jambo huwa lina mwanzo wake na bila shaka; jambo lenye mwanzo lazima litakuja kuwa na mwisho wake! Kwa hiyo unabii huo wa Kumbukumbu la Torati 18:18,18, ndipo sasa umepata mwanzo wake kwa kutimia kwangu, baada ya miaka karibu 3,500 kupita.
Kwa hiyo ndugu zangu; wakati huu siyo wakati wa kutukana, kusonya, kubeza au kupinga kwa sababu muda siyo muda kila mtu atajua awe anataka au hataki kwamba kweli unabii wa Musa umetimia (ni jambo la wakati tu na wakati huo ahuna madhara kwa yeyote).
Kwa hiyo kitakacho fanya unabii ujulikane Tanzania na duniani kote; ni kama ambavyo nimekuwa nikieleza kwenye barua mbalimbali ambazo nimeiandikia ikulu tokea ule mwaka wa 2012 na nikiwa nimeandika makala nyingi katika magazeti mbalimbali, yanayoeleza nia ya kuomba kukutana na Mh. Kikwete. Kwa sababu ndilo sharti la kwanza ambalo napaswa kufanya ili nimueleze Rais wangu anayetawala kipindi hiki ambacho unabii umeanza; juu ya makusudi ya Mungu anayo kusudia kuyafanya hapa duniani hivi sasa.
Rais atakapokuwa ameelewa ndipo sasa watu wote mtakuja kufahamu kinachomaanishwa na unabii huo wa mimi kuteuliwa kuwa nabii kama Musa. Kwa hiyo sala za kila mtu ni kuomba Mh. JK kunipa nafasi ya kumuona na kunielewa juu ya utume wangu kwa sababu ni mzuri sana na ndilo suluhisho la matatizo mengi yanayolikumba taifa hili na dunia kwa ujumla.
MUNGU AMPA SIKU 10 MH. KIKWETE
Kama nilivyoeleza hapo juu kuwa tokea mwaka 2012 nimekuwa nikiandika barua ikulu za kuomba kukutana ana kwa ana na Rais kwa ajili ya kuwakilisha utume nilio nao na nikieleza utume huu si wangu peke yangu bali na taifa letu linahusika kwa asilimia 100 na unabii huu. Na tokea mwaka 2009, nimeendesha vipindi vya televisheni na kuandika makala nyingi ambazo Rais na watendaji wake wa serikali wangepaswa kusituka na kuniita ili nitoe maelezo kwao, lakini wamekuwa wakifumba macho na masikio.
Mara nyingi wasaidizi wa Rais wamekuwa wakitoa kisingizio cha kwamba Mheshimiwa ana kazi nyingi sana, ambavyo ni kweli, lakini jambo hili hata mtu mwenye upeo mdogo, anapaswa kulipa umuhimu wake, kwa sababu siku zote nimekuwa nikilieleza kwenye ukubwa wake.
Nasikitika kusema kuwa Mungu amekasirika sana sana na mimi nabii wao nimekwazika sana sana. Kwa sababu tokea mwaka 2012 naiandikia ikulu umuhimu wa kukutana na Rais naambiwa ana kazi nyingi sana na tarehe 29/11/2014 niliandika makala ambayo niliichapisha waraka ambao nilimwandikia Rais mwaka 2012 ambao ukapuuzwa na kusababisha ufisadi mkubwa na matatizo mbalimbali yanayoendelea nchini.
Lakini mpaka naandika makala hii bado sijaitwa kumuona Raisi. Isitoshe tarehe 15/12/2014 nimemwandikia barua binafsi Rais ambayo maudhui yake nitayaeleza hapa chini na nikamkabidhi mkononi msaidizi wake wa habari Bw. Salva Rweyemamu; lakini mpaka sasa bado sijaitwa. Cha kushangaza wasanii wetu wawili ambao wameshinda tuzo na ushindi wa BBA juzi tu, Rais akawa hana kazi nyingi sana, kwani aliwapatia wasanii hao nafasi ya kwenda kupongezwa na Rais ikulu (ambalo ni jambo zuri sana).
Nimesema ni jambo la kushangaza kwa sababu thamani ya tuzo na zawadi za wasanii hao ambao kwa Rais wameonekana ni wa muhimu sana kuliko nabii Buberwa, ambapo thamani ya tuzo zao haiwezi kuhudumia hata kijiji kimoja chenye wakazi 100 tu kwa mwaka hata mmoja. Lakini nabii Buberwa siku zote karibu miaka 2 sasa nimemwandikia barua Rais na kutoa makala magazetini kuwa nina fomula ya kutoka kwa Mungu ya kuondoa vita duniani, kufufua uchumi wa nchi na dunia, napuuzwa.
Sasa Mungu anaagiza; hatumii tena lugha laini, bali anamwagiza Mh. Prof. Jakaya Kikwete na washauri wake wawe wamekutana nami ndani ya siku 10, tokea tarehe 25/12/2014, kinyume cha hivyo Mungu anasema utukufu ambao Tanzania ilikuwa ipewe utahamishiwa katika nchi nyingine mojawapo ya Afrika Mashariki kati yenye watawala wenye alama za majina JK. Na Mungu anasema waziwazi kwamba kwa taifa hili kupuuza daraka ambalo alitaka kulipatia taifa hili hakika kutatokea mtikisiko mkubwa sana sana kuliko yote iliyowahi kutokea katika taifa hili tokea lipate uhuru.
BARUA KWA RAIS
Hapa chini ni baadhi ya makusudi ya barua niliyomwandikia Rais ya tarehe 15/12/2014, amabayo Mungu anasema yatekelezwe ndani ya siku 10, tokea tarehe 25/12/2014.
YAH: OMBI LA KUKUONA KWA UHARAKA ILI NIKUJULISHE MIKAKATI AMBAYO MUNGU WA KWELI MUUMBA ANATAKA KUIFANYA JUU YA TAIFA HILI NA DUNIA KWA UJUMLA KUPITIA TAIFA LETU NA UONGOZI WAKO.
Mh. Rais bila ya kutoa maelezo marefu ningependa nijitambulishe kwako kwa ufupi; mimi Mungu aliniandaa tokea nilipozaliwa kuja kutimiza makusudi makuu ya Mungu hapa duniani kwa ajili ya kubadilisha maisha ya wanadamu wote duniani yawe mazuri kwa kupitia taifa letu Tanzania.
Mh. Rais, napenda kukutaarifu kuwa makusudi hayo ambayo Mungu wa Kweli alikusudia kuyatimiza, alipanga yatimizwe chini ya utawala wako Mheshimiwa Dr. JK Mrisho.
Mungu alitengeneza Tanzania katika jiografia ya dunia kuja kuwa taifa la kipekee na lenye utukufu duniani kwenye nyakati za siku za mwisho. Mungu alianza kuandaa watu wa taifa hili kuwa wamoja na kuwa watu wenye utu wa kipekee duniani chini ya Baba wa taifa Mwl. JK Nyerere.
Lengo la Mungu la kutengeneza utu huu tulio nao Watanzania chini ya Mwl. JK Nyerere ni kwa sababu Mungu alitaka tuwe watu wa kwanza kuyapokea na kuyakubali makusudi yake makuu yanayokuja kutangazwa kabla ya watu wengine duniani kukubali kuyatekeleza na kuyatumia.
Kwa ufupi Mh. Rais, mwaka 2009 ndipo Mungu alinifunulia kuwa mimi ni nabii maalum ninayetimiza unabii ambao ulitabiriwa miaka 3,500 iliyopita katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati sura ya 18:18,19. Kwa hiyo mimi si kama manabii ambao wapo duniani siku hizi wanaodai wanatabiri matukio mbalimbali na kudai kuponya wagonjwa kimuujiza kutoka katika imani tofauti tofauti.
Kwa hiyo mimi ni nabii mwenye makusudi mahsusi kwa dunia kama ambavyo Mungu alimtumia Musa wa taifa la Israeli la kale kukomboa watu wa taifa la Mungu Israeli kutoka utumwani Misri; ndivyo Mungu anataka kukomboa watu wote duniani wanaoishi katika kipindi hiki kinachoelekea Kiama.
Mungu anataka kutimiza nia hiyo kupitia taifa letu ambalo nyutu za watu wake zilitengenezwa chini ya utawala wa baba wa taifa Mwl. JK Nyerere na makusudi hayo ya Mungu yanaanza kutekelezwa chini ya utawalo wako Dr. JK Mrisho na maagizo ya makusudi hayo ya Mungu yatakuwa yakielekezwa na Mungu kupitia malaika zake kwa kupitia mwanadamu mimi Dr. JK Buberwa. (Alama JK ndizo Mungu amezitumia kuthibitisha unabii wake kuwa huko hakika)
MAOMBI YANGU RASMI KWAKO NI:
1. Nakuomba Mh. Rais kunipatia nafasi ya kukuona ana kwa ana kwa ajili ya kukueleza maagizo mahsusi toka kwa Mungu ambapo nilifanya jitihada mbalimbali tokea mwaka 2011 bila ya mafaniko.
2. Nchi yetu itakumbwa na mtikisiko wa nne ambao utakuwa mkumbwa kuliko mitikisiko 3 iliyopita. Na taifa letu litazidi kukumbwa na mabalaa mbalimbali madogo kwa makubwa na taifa halitaweza kuendelea kiuchumi. Na si hivyo tu kama Mh. Rais utaendelea kupuuza maombi ya barua hii stability ya nchi itakuwa mashakani.
3. Kwa hiyo Mh. Rais Mungu atafungua baraka hizi pindi nitakapokuona na kukueleza jukumu rasmi la Tanzania katika mpango huo. Makusudi hayo Mungu hatayafungulia mtaani bali ikulu inapaswa kuyaidhinisha kwa sababu ni mambo makubwa sana.
MAKUSUDI YA MUNGU KWA DUNIA NI YAPI KATIKA WAKATI WETU HUU?
Kwa ufupi taifa letu la Tanzania Mungu ameliteua kama taifa kusimamia makusudi yake ya kuleta mabadiliko duniani tokea Novemba 5, 2012 ambapo ni miaka 2 sasa imepita kwa sababu ya uongozi wa kitaifa kupuuzia au kuyaona mambo haya kama ya kiuendawazimu.
MIKAKATI MIKUU YA MUNGU NI:-
1. Kukomesha vita duniani katika miaka 7 tokea Novemba 5, 2012
2. Kukomesha njaa na umasikini duniani katika miaka 14 tokea Novemba, 2012
3. Kukomesha duniani uharifu, ufisadi, wizi, unyanganyi, ugaidi na matendo mengine mabaya katika jamii katika miaka 14 tokea Novemba, 2012
Katika unabii huu Tanzania ni mratibu wa mipango ya Mungu kwa niaba ya dunia na Marekani na Uingereza watakuwa wasimamizi na watekelezaji wa mipango hiyo duniani kwa kushirikiana na serikali mbalimbali duniani kama ilivyoelezwa katika gazeti la Daily News la Juni 10, 2013.
MUHIMU: Kwa hiyo Mh. Rais Mungu anakusubiri kuelewa, kukubali na kuidhinisha makusudi hayo ya Mungu kuanza. Bila ya wewe Mh. Rais uliyeko madarakani kukubali kuidhinisha mipango hiyo hakika Mungu hatafungua baraka hizi kwa taifa hili na dunia, kama ambavyo Musa hakuweza kuwatoa wana wa Israeli Misri bila kauli ya mfalme Farao kuwa sasa
ondokeni.
Wako Mtiifu,
Dr. JK Buberwa
NABII KAMA MUSA (KUMBUKUMBU 18:18,19)
Simu: 0769 800 100 na Email:
dr.josephbuberwa@gmail.com