Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nenda pale samora ukachungulie tena kwenye bureau de change. Hizi namba zako si sahihi. Hata hivyo thamani halisi ya fedha iko kwenye "stability" sana sana si kwenye exchange rate. Pamoja na kuwa umekosea mno na hesabu zako si sahihi, angalia kwa mwaka thamani ya yen au yuan inapungua kiasi gani? Hicho ndo kipimo cha fedha. Hard currency si fedha yenye exchange rate kubwa, bali ni fedha ambayo thamani yake haiyumbi!! Hizo Namba zako ni uongo ulioshiba!
kweli mkuu....Watanzania tukome kuwapa watu wa pwani Urais, hawa watu asili yao ni uvivu na kukaa vijiweni, hata jana pale Diamond kilikuwa ni kijiwe cha wazee/waswahili wa Dar wasiojitambua. Mambo kama hayo mimi sikuona kulikuwa na haja gani ya kuweka kijiwe, ilikuwa ni kuchukua hatua basi
Mimi sijaona tatizo lolote, kukosa hoja za msingi za kujadili mambo muhimu
tunakaa kushupalia neno 'pesa ya madafu'. Labda hili linaweza kuwa tatizo
kwa watu wa shamba na si mjini. Neno hilo halina athari yoyote iwe kisiasa
kiuchumi nk. Tutafute kukosoa hotuba yake katika mambo mengine
kujadili hili ni upuuzi zaidi.
Kwani hela ya ''madafu'' ina maana gani kwa sababu inawezekana tunalaumu kitu ambacho kinabeba uharisia wa maneno.
Kwani kusema hela ya ''madafu'' ina madhara gani ya moja kwa moja katika uchumi wa nchi?
Naomba unieleweshe kwa sababu sifahamu msingi wa hoja yako.
dos santos ni namna gani umeonyesha gharama ya wazazi wako kukupeleka shule haikupotea !
Ulichokiongea hapa chatosha kua mwisho wa Thrade.
Presidaa aite aitavyo Tz's currency itabaki kua na same value iliyopo .
Hakuna hoja ya kujadili hapa.
Hivi ukimwambia mwanao "Paka wee" ndiyo kawa Paka ?
100% na watu wazima humu JF eti hawaoni tatizo? Yule ni mkuu wa nchi na alikuwa anaongelea hatima ya maisha yetu. Wengi wetu sasa tunashindwa hata kupanga bajeti kwasababu ya mfumuko wa bei. Mada yenyewe aliyokuwa anaongelea sio ya utani kwani wafadhili wamezuia hela na watu wanakufa kwa kukosa dawa
Watanzania tukome kuwapa watu wa pwani Urais, hawa watu asili yao ni uvivu na kukaa vijiweni, hata jana pale Diamond kilikuwa ni kijiwe cha wazee/waswahili wa Dar wasiojitambua. Mambo kama hayo mimi sikuona kulikuwa na haja gani ya kuweka kijiwe, ilikuwa ni kuchukua hatua basi
Hujui chochote wewe,Just shut up!Mimi sijaona tatizo lolote, kukosa hoja za msingi za kujadili mambo muhimu
tunakaa kushupalia neno 'pesa ya madafu'. Labda hili linaweza kuwa tatizo
kwa watu wa shamba na si mjini. Neno hilo halina athari yoyote iwe kisiasa
kiuchumi nk. Tutafute kukosoa hotuba yake katika mambo mengine
kujadili hili ni upuuzi zaidi.
Nimemsikiliza rais Jakaya Kikwete (JK) jana na hotuba yake ya kujibaraguza mbele ya Watanzania. Sikutegemea jipya kwenye story zake za jana na wale Wazee wa vijiwe vya CCM ila hili la yeye kama rais wa nchi kudharau sarafu ya nchi yake mwenyewe hadharani limenisikitisha sana.
Ni ajabu sana kwa rais wa nchi kwenda mbele ya vyombo vya habari kukiwa na halaiki ya watu na kuiita bila haya wala aibu sarafu ya nchi kwa jina la kebehi kuwa eti ni "hela ya madafu" halafu anaachwa tu hakuna kitakachompata. Hii ni fedheha na dharau ya hali ya juu kwa sisi ambao hela hiyo ya 'madafu' ndio mshahara wetu na fedha yetu ya kufanya biashara kila siku.
Tunajua mmeiba sana na tena mkishaiba chap chap mnazibadilisha kuwa dollar hivyo haya "madafu" hata yawe sawa na toilet paper (karatasi za kuchambia) kwenu sio issue. Itakuwa ajabu sana kama nikimsikia tena waziri wa fedha na uchumi akisisitiza wafanyabiashara hasa Wahindi ambao wanajua sana umuhimu wa dhamani ya fedha wasiuze bidhaa zao kwa dollar maana hela wanayoambiwa watumie hata mkuu wa nchi anaiona haina maana yoyote zaidi ya kuwaweza kununulia tunda la bei duni la aina ya madafu.
Rais anatakiwa aelewe kuwa kauli zake za namna hii tena anazozitoa hadharani zina madhara ya moja kwa moja kwa uchumi wetu na achunge sana kauli zake anapozungumza masuala muhimu ya nchi hadharani. Kama ni kutudharau kesha fanya hivo sana lakini atuache basi na hii sarafu yetu ambayo kila kukicha anafanya mbinu za kuishusha dhamani. Kudharau sarafu ya nchi hadharani tena mchana kweupe na mtoa dharau akiwa ndie rais wa nchi inatakiwa liwe kosa la uhujumu uchumi na JK anapaswa kushitakiwa kwa hili.
Tumekuvumilia kwa mengi JK lakini kwa kuifananisha sarafu yetu na madafu umevuka mipaka. Bora ungeiita hivyo ukiwa chumbani kwako au ukisha acha nafasi yako ya urais. Ni kwa sababu unaongoza nchi yenye mifumo mibovu ya sheria inayokulinda laiti ingelikuwa nchi nyingine kauli yako hiyo ingetosha wewe kujiuzulu ukachunge mbuzi wako kule Msoga.
Mwana JF hebu piga picha nini kitampata rais Baraka Obama wa Marekani kama siku atakwenda hadharani kukiwa na vyomba vya habari na kutamka maneno ya dhihaka kwa dollar kama alivyofanya rais Jakaya Kikwete jana pale ukumbi wa Diamond Jubilee. Jibu nadhani unalo mwenyewe mwana Jf.
Wasalaam,
Kinyungu.
Ni kweli matamshi ya kiongozi wa nchi yana nguvu sana, ya kujenga au kubomoa. Kiongozi wa nchi anapashwa kupima kwa makini maneno yote anayoyasema na siyo kuzungumza lugha za mitaani. Tangu tupate uhuru tumesikia matamshi mengi ya viongozi ambayo yamekwamisha nchi. Kwa mfano dhana ya umasikini ambayo imerudiwa mara nyingi na viongozi imetukwamisha sana. Tangu unazaliwa hadi unakuwa mtu mzima unasikia matamshi hayo hayo ya umasikini wa nchi. Hatuwezi kupanda juu zaidi ya fikra zetu.