Rais wa Somalia apinga uvamizi wa Israel kwenye ardhi yake.

Rais wa Somalia apinga uvamizi wa Israel kwenye ardhi yake.

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,661
Reaction score
40,890
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ameiambia Al Jazeera kuwa nchi yake haitakubali uwepo wa Israel nchini humo "chini ya hali yoyote ile" na itapinga jaribio lolote la kuvutwa katika migogoro ya Mashariki ya Kati.

2988469f2e3db996a3ecb50447db51b1.jpg

Rais wa Somaliland na waziri mkuu wa Israel.

Katika mahojiano maalum, Mohamud alisema kuwa Israel ilikuwa ikipanga kuanzisha kituo cha jeshi la wanamaji huko Berbera na kutumia uwanja wa ndege wa mji huo, huku akiongeza kuwa lengo lake halisi lilikuwa kujisogeza karibu zaidi na mataifa ya Ghuba pamoja na Iran.

Berbera ni mji wa bandari kwenye pwani ya Ghuba ya Aden huko Somaliland – jamhuri iliyotangaza uhuru wake yenyewe kaskazini-magharibi mwa Somalia, ambayo ilitambuliwa na Israel mwaka jana lakini inadaiwa na Mogadishu.

Berbera inatazamana na Yemen ng'ambo ya bahari, karibu na mlango-bahari wa kimkakati wa Bab al-Mandeb. Kundi la Houthi, ambalo lina uhusiano na Iran, hapo awali limeweka vizuizi dhidi ya meli zenye uhusiano na Israel katika eneo hilo.

"Tutashinda changamoto zinazoikabili nchi yetu kutokana na hatua za Israel," alisema Mohamud katika mahojiano yake mapana.

Aliongeza kuwa mipango ya Israel ni sehemu ya mradi wa "Israel Kubwa" (Greater Israel) – neno linalorejelea mapendekezo mbalimbali, ambayo mara nyingi hutokana na tafsiri za kibiblia, kuhusu Israel kumiliki maeneo yaliyo nje ya mipaka yake ya sasa. Baadhi ya matoleo ya mpango huo yanajumuisha eneo linaloanzia Mto Nile hadi Mto Eufrate.

The-alarming-details-of-Israels-future-ambitions.jpg

Ramani ya "Greater Israel".

Rais wa Somalia aliielezea Israel kama "nguvu inayovuruga utulivu" na isiyoheshimu sheria za kimataifa.
Hakuna nchi nyingine isipokuwa Israel inayotambua Somaliland, huku wakazi wa eneo hilo wenyewe wakipinga vikali uwepo wa Israel, alisema Mohamud.

Source: Al Jazeera
 
Je ni kwanini Israel inaunga mkono "magaidi" wa Somali National Movement ilihali dunia nzima hakuna nchi hata moja inawatambua waasi hao kama taifa huru?

Je kivipi nchi inayojinasibu kupambana na ugaidi na machafuko middle east inafadhili machafuko huko Somalia?

Na kwanini AU ipo kimya huku ikiona wazi Israel inaweza sababisha Iran na houthi wahamishie mashambulizi Afrka mashariki.

Cc Tresor Mandala Proved
 
Let Israel settle and control Horn of Africa, watu wanao waza mabikira peponi sio wa kuwa acha hivi hivi
Kwani hao somaliland si nao ni "wawaza mabikra" au ghafla wamekua watakatifu kisa wapo upande wa Israel?

Huoni risk ya Houthis na Iran kuanza kushambulia nchi zetu maskini hizi kama Kenya, Tanzania ili kupata ground ya kupambana na Israel ya somaliland?

Hizi risk hamzioni? Nchi maskini kama yetu ikipigwa na Khoramshar 4 ya Iran si tutabaki majivu??
 
Kwa hiyo serikali tufuge magaidi coz tunawaogopa , na kwanza hatuwaogipi hao magaidi
 
Haya mawazo ya majitaka ndiyo yamekufanya uwe na siasa za majitaka mpaka kwenye siasa umepoteza mvuto.

Israel ni ka nchi kadogo sana lakini Iran ameshindwa kuisambaratisha na kwa akili zako zilivyo ndogo unafikiri Iran anaweza kupiga nchi zote yaani tayari Iran ni super power😄😄😄😄

Iran ameweza kupiga kwa wajinga wenzake wavaa kobazi basi unaona Iran ni super power.😄😄😄

Endelea kuota maana hata viongozi marehemu wa Iran waliona Iran ni super power kwahiyo wanaweza kujilinda na kuipiga Israel ila mwisho wa siku hata mtoto wa marehemu naye yupo mapangoni akijitokeza analambwa kichwa
 
Kimataifa Israel inaitambua Somaliland hivyo inaweza kushirikiana nayo. Na kisheria ukishaitambua nchi huwezi tena kurudi nyuma na kusema huitambui.
 
Ajabu ni kwamba huyu Rais wa Somalia hawezi kabisa kwenda Hargeisa huko Somaliland. Anawezaje kudai eneo hilo ni la Somalia?

Hakuna Rais wa Somalia amewahi tembelea Somaliland kwa ziara rasmi tangu ilivyozuka vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Wasomali mwaka 1991.
 
Sasa mkuu anaendaje na mgogoro upo? Usalama wake unakuaje?

Somalia imekua na mapigano mengi baada ya 1991 ikiwemo kuamka kwa mahakama za sharia na Al Shabaab muda wote huo serikali ya somalia haina meno nakumbuka uchaguzi wa miaka ya 2000 Rais alichaguliwa kwenye uwanja wa mpira tena Kenya!! Sasa serikali kama hiyo inawezaje kuwaza ziara za somaliland wakati nchini palikua hapakaliki?

Wanahitaji umoja zaidi kuliko hii migogoro inayoenda kuzalishwa na Israel.
 
Kimataifa Israel inaitambua Somaliland hivyo inaweza kushirikiana nayo. Na kisheria ukishaitambua nchi huwezi tena kurudi nyuma na kusema huitambui.
Ni nchi kivipi? Kwahiyo leo M23 wakitangaza Congo Mashariki ni nchi kamili basi ni haki watu kuitambua bila kujali uhalali wa kisheria? Ni lazima kuwepo na treaty (Somalia na somaliland) inayotambulika sio umeamka asubuhi tu unatangaza basi inakua halali, huo ni uhuni.

Pia kisheria sio kweli huwezi rudi nyuma, mfano Israel ilikua inatambua uhuru wa Sahara Democratic Republic (SADR) ila baadae ikabadili mawazo na kutambua SADR kama sehemu ya morocco na sio nchi huru.
 
Somaliland imetulia na Kuna amani asilimia 100. Wanafanya chaguzi zao kwa amani na demokrasia ipo juu sio kama Tanzania. Hiyo Somalia inayopigwa kelele hamna lolote ni mapigano Kila siku tu.
 
Kwa hiyo serikali tufuge magaidi coz tunawaogopa , na kwanza hatuwaogipi hao magaidi
Kwani somaliland sio magaidi? SNM imeua sana watu somalia, lakini ina supportiwa na Israel sasa huoni ni unafiki?

Siku Israel ikianza support waasi wa msumbiji kupora gesi ya lindi na mtwara ndio akili itatukaa.
 
Je ni kwanini Israel inaunga mkono "magaidi" wa Somali National Movement ilihali dunia nzima hakuna nchi hata moja inawatambua waasi hao kama taifa huru?

Je kivipi nchi inayojinasibu kupambana na ugaidi na machafuko middle east inafadhili machafuko huko Somalia?

Na kwanini AU ipo kimya huku ikiona wazi Israel inaweza sababisha Iran na houthi wahamishie mashambulizi Afrka mashariki.

Cc Tresor Mandala Proved

MBABE NETANYAU ANAWATEMBEZEA MOTO MAGAIDI KILA SEHEMU. LILE JAMAA NI BABE SANA. HALICHEKI NA KIMA. LINAPELEKA MOTO KILA SEHEMU KWA HAO MBWA
 
Sasa mkuu anaendaje na mgogoro upo? Usalama wake unakuaje?

Somalia imekua na mapigano mengi baada ya 1991 ikiwemo kuamka kwa mahakama za sharia na Al Shabaab muda wote huo serikali ya somalia haina meno nakumbuka uchaguzi wa miaka ya 2000 Rais alichaguliwa kwenye uwanja wa mpira tena Kenya!! Sasa serikali kama hiyo inawezaje kuwaza ziara za somaliland wakati nchini palikua hapakaliki?

Wanahitaji umoja zaidi kuliko hii migogoro inayoenda kuzalishwa na Israel.
Somali land kwanini walijitenga na somalia?

Na vipi kuhusu maisha yao ya sasa ukilinganisha na Somalia je wamepiga hatua au wako kama somalia tu?
 
Israel ni ka nchi kadogo sana lakini Iran ameshindwa kuisambaratisha na kwa akili zako zilivyo ndogo unafikiri Iran anaweza kupiga nchi zote yaani tayari Iran ni super power😄😄😄😄
Ndio ni super power, huoni ana control siasa za mashariki ya kati. Nani alijua Yemen ingechukuliwa kutoka mikono ya Saudi Arabia na UAE kwa spidi ya wiki moja? na leo hii meli haipiti Baab al Mandeeb wala Hormuz bila ruhusa ya Iran. Na wao ndio wanaamua waziri mkuu wa Iraq na Lebanon na sasa Turkey na Oman ziko upande wa Iran.
Iran ameweza kupiga kwa wajinga wenzake wavaa kobazi basi unaona Iran ni super power.😄😄😄
Hizo kambi za USA ni kobaz? Mbona zimefungwa sasa kama Iran si chochote?
Israel ni ka nchi kadogo sana lakini Iran ameshindwa kuisambaratisha
Sababu inalindwa na USA, hata Trump amesema hilo mara nyingi kuwa bila ya USA hao Israel wanapigwa ndani ya wiki moja tu. Nakumbuka hata Turkey ilipotaka kuingia upande wa Iran ni hao USA ndio walienda kumtuliza maana yake Israel inafanya fujo ikijua italindwa ila yenyewe kma yenyewe si lolote.
 
Sasa mkuu anaendaje na mgogoro upo? Usalama wake unakuaje?

Somalia imekua na mapigano mengi baada ya 1991 ikiwemo kuamka kwa mahakama za sharia na Al Shabaab muda wote huo serikali ya somalia haina meno nakumbuka uchaguzi wa miaka ya 2000 Rais alichaguliwa kwenye uwanja wa mpira tena Kenya!! Sasa serikali kama hiyo inawezaje kuwaza ziara za somaliland wakati nchini palikua hapakaliki?

Wanahitaji umoja zaidi kuliko hii migogoro inayoenda kuzalishwa na Israel.
Kwa ilipofikia Somaliland lazima itakuwa tu nchi kamili yenye kutambulika. Ni suala la muda tu USA na nchi za west zote zitaitambua kutokana na strategic location yake ambayo mataifa hayo yanataka ili kulinda usalama wa Bab el Mandeb.

Kingine ni kuwa Turkiye wameshajimilikisha Somalia. Kwa hiyo West nao lazina wajimililikishe Somaliland ili kum-keep in check mturuki.

Kitu kibaya zaidi kitakachotokea kwa Somalia ni kujitenga kwa Puntland. Japokuwa Puntland bado hawajafanikiwa sana kama najirani zao wa Somaliland ila na wao ndiko wanakoelekea.
 
MBABE NETANYAU ANAWATEMBEZEA MOTO MAGAIDI KILA SEHEMU. LILE JAMAA NI BABE SANA. HALICHEKI NA KIMA. LINAPELEKA MOTO KILA SEHEMU KWA HAO MBWA
Hata Somaliland chini ya SNM ilifanya matukio ya kigaidi na uhalifu wa kivita kipindi cha vita ya kujitenga 1991.

Sasa kivipi Netanyahu anasupport kobaz? Au vita ya ugaidi ni unafiki?
 
Back
Top Bottom