zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,661
- 40,890
- Thread starter
-
- #21
Lakini hii ni precedent mbaya sana, ina maana hata magaidi wa Al shabaab wakiweza iteka NLD ama Coastal region (Lamu, Mombasa, Kwale etc) na kujitenga kuwa nchi huru na wakaalika wachina au Israel kujenga naval base basi automatically serikali za kigaidi zinapata recognition?Kwa ilipofikia Somaliland lazima itakuwa tu nchi kamili yenye kutambulika. Ni suala la muda tu USA na nchi za west zote zitaitambua kutokana na strategic location yake ambayo mataifa hayo yanataka ili kulinda usalama wa Bab el Mandeb.
Kingine ni kuwa Turkiye wameshajimilikisha Somalia. Kwa hiyo West nao lazina wajimililikishe Somaliland ili kum-keep in check mturuki.
Kitu kibaya zaidi kitakachotokea kwa Somalia ni kujitenga kwa Puntland. Japokuwa Puntland bado hawajafanikiwa sana kama najirani zao wa Somaliland ila na wao ndiko wanakoelekea.
Inaanza kwa kutambulika na nchi zingine.Somaliland haitambuliki na AU,IGAD ,UN kama nchi huru ila inatambulika bado ni sehemu ya Somalia.
Nchi inakuwa nchi kwa kutambuliwa na nchi zingine. Eneo la M23 likianza kutambuliwa na nchi zingine ndipo linaanza kuwa nchi. Ndiyo maana Somaliland wanauhuru wote ila wanazunguka dunia nzima kuomna nchi ziitambue.Ni nchi kivipi? Kwahiyo leo M23 wakitangaza Congo Mashariki ni nchi kamili basi ni haki watu kuitambua bila kujali uhalali wa kisheria? Ni lazima kuwepo na treaty (Somalia na somaliland) inayotambulika sio umeamka asubuhi tu unatangaza basi inakua halali, huo ni uhuni.
Pia kisheria sio kweli huwezi rudi nyuma, mfano Israel ilikua inatambua uhuru wa Sahara Democratic Republic (SADR) ila baadae ikabadili mawazo na kutambua SADR kama sehemu ya morocco na sio nchi huru.
Hata Somaliland chini ya SNM ilifanya matukio ya kigaidi na uhalifu wa kivita kipindi cha vita ya kujitenga 1991.
Sasa kivipi Netanyahu anasupport kobaz? Au vita ya ugaidi ni unafiki?
YEYE ANAPIGA PIPE MTU YEYOTE AMBAYE ATAKUWA GAIDI. YBWYBHata Somaliland chini ya SNM ilifanya matukio ya kigaidi na uhalifu wa kivita kipindi cha vita ya kujitenga 1991.
Sasa kivipi Netanyahu anasupport kobaz? Au vita ya ugaidi ni unafiki?
Sasa mbona huko Ukraine yale majimbo yaliyojitenga 2014 kwenda urusi na yakatambuliwa haraka haraka na Putin hao EU na US wamekataa kuyatambua? Ni wapi mstari unachorwa kuwa waasi wakijitenga nchi itambuliwe au isitambuliwe? Otherwise itakua kila siku mtu anaanzisha uasi anajitangazia taifa jipya!!Nchi inakuwa nchi kwa kutambuliwa na nchi zingine. Eneo la M23 likianza kutambuliwa na nchi zingine ndipo linaanza kuwa nchi. Ndiyo maana Somaliland wanauhuru wote ila wanazunguka dunia nzima kuomna nchi ziitambue.
Suala la kubadili utambuzi wa nchi bado linabishaniwa kisheria.
Hiki ni kisingizio tu, mbona marekani imeweka kambi karibu nchi zote zinazoizunguka Iran ila hao hao Iran wakiwa na washirika hapo mashariki ya kati inakua haramu?Iran kufadili magaidi wa Houthi nchini Yemen ndio imeleta shida yote hii bila ya hivyo Israel haikuwa na mpango wa kuja Samaliland.
Munataka muachwe pekeenu muzidi kuinukisha dunia mavi😡🤔🙆🏿Let Israel settle and control Horn of Africa, watu wanao waza mabikira peponi sio wa kuwa acha hivi hivi
Na Ukraine kufadhili magaidi wapi ndio imeleta shida yote kule Ukraine????Hizi miungano feki lazima zitakuja tu kutokomea kwa sababu misingi yake haikuwa wananchi bali watawala.
Tuliona kwa iliyokuwa Yugoslavia, Ujerumani, USSR na hata Tanzania pia muungano umeshikiliwa na kauzi tu.
Huyo Samaliland baada ya kutambuliwa na Israel sasa itakuja kutambuliwa na Marekani na kisha mataifa yote ya magharibi yatafuata na hao wengine hata wasipoitambua kutakuwa hamna madhara yoyote.
Iran kufadili magaidi wa Houthi nchini Yemen ndio imeleta shida yote hii bila ya hivyo Israel haikuwa na mpango wa kuja Samaliland.
Kuna maeneo yalikwepo kabla ya Neno Somalia na kuna watu walizaliwa Somaliland hivyo wanatohaki ya kujitenga na kuishi maisha yao.Lakini hii ni precedent mbaya sana, ina maana hata magaidi wa Al shabaab wakiweza iteka NLD ama Coastal region (Lamu, Mombasa, Kwale etc) na kujitenga kuwa nchi huru na wakaalika wachina au Israel kujenga naval base basi automatically serikali za kigaidi zinapata recognition?
Tunapoelekea Africa itakua battle ground ya mabeberu, tumerudi enzi za scramble and partition of Africa ambapo kila nchi ya magharibi inajimegea kipande chake bila kujali fate ya nchi husika.
Kwa sasa Iran nayo inafadhili makombora na drones serikali ya Sudan huku Israel ikifadhili RSF. Tunapoelekea hizo proxy wars zitahamia somalia/Kenya kupambania horn of Africa.
Nilitarajia AU ingepinga hii precedence ila ni toothless kabisa
Umeongea pointless kabisa. Kwahiyo kila jamii ikiamua kuasi na kujitenga iangaliwe tu!? Unajua madhara yake!? Si itakua ni machafuko kila kona kwa mtindo huo!? Dunia ina utaratibu ambao ulishabadilika kiustaarabu wa kale na kuja kwa ustaarabu mpya wa sasa.Kuna maeneo yalikwepo kabla ya Neno Somalia na kuna watu walizaliwa Somaliland hivyo wanatohaki ya kujitenga na kuishi maisha yao.
Viongozi wapuzi wasiyojali maisha ya wengine ndiyo chanzo cha yote hayo.
Kipindi cha Mobutu hakutambua kuwa anatengeneza sumu itakayoigawanyisha nchi yake hata baada ya miaka 50.
Kinachofanyika Somalia (Putland, Somalilland), DRC (M23), Sudan (Sudan Kusini na sasa vita), Sudan Kusini (Sasa vita) kinaonesha kabisa chini ya utawala wa CCM hapa Tanzania tunaelekea hukohuko.
Dalili za mvua ni mawingu, kuna watu walizaliwa kabla ya Upuuzi unaoitwa Tanzania hivyo wakiamua kwa ridhaa yao kurudi kwenye nchi yao ya asili walikozaliwa wakaikuta nani wa kuwazuia? na kwasababu gani?
Wapuuzi wa CCM wanairudisha jamii zetu upande uleule ambapo Omar Al Bashir aliwarudisha watu wa Sudan.
Hapana lo vita sio poa