TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Anauliza
1. Uhakiki wa vyeti feki utaendelea au utasimamishwa?

2. Ajira zitaanza kutoka kwa kada ya ualimu na madaktari kama mwanzo kwenye awamu ya Nyerere-Kikwete?

3. Nyongeza ya mshahara itakuwepo?
Mzee Lowasa anasemaje.
 
Siwezi kuwa mnafiki kamwe....
Na si ukubali unafki,
Asa mtu ambaye jana kafungua uzi akichagiza kamanda aende afu saiv apa anajitia anatia maneno ya Faraja na yote.
Unajifanya una uchungu kuliko mama Janet na familia.Acha unafiki.Mungu anakuona.
 
Wazungu au hao mabeberu wanakujaje hapo sasa! Kuwa mkweli wacha fitna mzee. We ukifa pia umebeberushwa si ndio!?
Nyerere alifariki wakati keshastaafu, Mkapa naye alishazoea maisha mtaani, ni kwa Mara ya kwanza Tanzania tunapoteza Rais aliye madarakani, kweli Mabeberu wametuweza
 
RIP kiongozi wetu.
 
Alitaka kumaliza urais wake akiwa ameweka miundombinu muhimu yote ili ajae ajishuhulishe na mengine. Aliipa TZ heshima kwa nchi jirani.

Anyways, anaejua sheria inasemaje tujuzane, mama Samia ataongoza nchi mpaka 2025 au utaitishwa uchaguzi mpya?
Soma hapo
 
Kuna mambo hatukukubaliana naye, lakini msiba huu umeniuma, umeniuma sana.

Nilijua anaumwa, lakini kulikuwa na hali ya matumaini kuwa huenda angepona.

Sijui nimpe pole nani - Pole sana Janet, pole watoto wa marehemu.

Funzo kwetu tuliobaki - maisha yetu ni mafupi sana Duniani, tujitahidi zaidi kutengeneza marafiki kuliko maadui.

Baba wa mbinguni, hekima yako si yetu, lakini maombi yetu ni kuwa uipumzishie Roho ya Marehemu John Magufuli mahala pema peponi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…