TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Tunaomba Mungu Ampe Pumziko la Amani Rais Wetu Mpendwa.

Lakini wakati haya yakiendelea tunaomba Daktari wake; Katibu Mkuu kiongozi na genge lote la wasaidizi wa karibu wakiohusika hasa kwenye utoaji wa Taarifa wawekwe mahali watueleze ni nini kilikua kinaendelea

Kama Alilazwa Rasmi Tarehe 6/3 pamoja na kuwa kuna taarifa aliugua toka tarehe 3/3 na kabla ya tarehe 10/3 Alikua clinically Dead ; ni jambo Gani liliwafanya hadi kuficha habari za huu ugonjwa hadi kufikia viongozi wakuu kila mmoja anaongea lake ina maana ni kama “walimteka”rais na kudhibiti kila kitu pengine kwa manufaaa yao ; basi ni vema wawekwe mahali waseme vizuri!
 
Rest in peace.

A point of curiosity though...

CHADEMA wameitisha press conference kesho and usiku huu Mama Samia comes with this news.

Coincidence? Or has Chadema become a force to be reckoned with.

Waliokua wanashikilia mwili wa Rais toka tarehe 10/3 hawakutaka hata kutoa Tangazo; pressure imekuwa kubwa na hata hizo habari za wizi na mengine imelazimika Makamu akachukuliwe haraka aje atangaze kabla ya asubuhi
 
Lema alifunuliwa akasema Mungu amemuonyesha ya kwamba Rais magufuli akiendelea kujiona yeye ni mungu hatafika 2020 lakini hakubadilika Mungu akamuongezea muda kidogo wa kujisahihisha lakini hakubadilika.
Spika katajwa pia huko
 
Japokuwa kifo ni chetu sote na njia yetu hapa duniani ila kifo cha hayati Rais Magufuli John P. kimenishitua sana nafsi.

Nimepitia kipindi kigumu sana huu mwezi kwa kuondokewa na shangazi yangu kipenzi. Sijakaa vyema bibi mzaa mama. Ni misiba mizito sana kwangu ila ghafla tena na huyu mzee Magufuli nae ametutoka. Imeniuma sana japo watu walikuwa wanamchukia ila sinaga nyongo nae. Nilikuwa naheshimu misimamo yake tu.
 
Tunaomba Mungu Ampe Pumziko La Amani Rais Wetu Mpendwa

Lakini wakati haya yakiendelea tunaomba Daktari wake ; Katibu Mkuu kiongozi na genge lote la wasaidizi wa karibu wakiohusika hasa kwenye utoaji wa Taarifa wawekwe mahali watueleze ni nini kilikua kinaendelea

Kama Alilazwa Rasmi Tarehe 6/3 pamoja na kuwa kuna taarifa aliugua toka tarehe 3/3 na kabla ya tarehe 10/3 Alikua clinically Dead ; ni jambo Gani liliwafanya hadi kuficha habari za huu ugonjwa hadi kufikia viongozi wakuu kila mmoja anaongea lake ina maana ni kama “walimteka”rais na kudhibiti kila kitu pengine kwa manufaaa yao ; basi ni vema wawekwe mahali waseme vizuri !!!
 
Tuombe mema...hopeful Mungu anajua namna ya kurekebisha na atasimama na mama Samia, thou it's hard Ila najua atashinda cha muhimu apate strong&true support kutoka kwenye inner circle.
Kweli, huyu JPM nitamkumbuka misimamo yake thabiti, napenda mtu kwenye misimamo

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Wewe jamaa Sasa hivi nakufuatilia Sana post zako.
Nimegundua unajua mambo mengi Sana mazito ya nchi hii.
Ulikua mtu wa kwanza kusema
Soooooooooooooo sad.
Kwa kifupi nimekukubali.asante sana.ukaendelea kutoa yaliyokua yanajiri nyuma ya pazia.
Salute sir.
 
Kwa haya.

1. Kuminywa kwa Vyombo vya Habari,
2. Wawekezaji Wakubwa Kusumbuliwa,
3. Matajiri Kutishwa, Kunyang'anywa Mali zao,
4. Kulipiza Visasi, Ukomoaji na Kutekwa hovyo Watu,
5. Ukabila ndani ya Mfumo Nyeti wa nchi,
6. Watanzania Kugawanya Kimatabaka,
7. Ajira kutoweka kwa Wasomi, Hali mbaya ya Kiuchumi kwa Watanzania na Kuanzisha Miradi kwa Kukurupuka hadi Kuigharimu nchi Kimapato,

Hakika nakubaliana nawe Ndugu tena 100% kabisa kuwa ametuacha pazuri tena hata kuliko Watangulizi wake akina Hayati Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na Mzee Kikwete.

R.I.P Kwake na Poleni kwa mlioguswa.
 
Kama kichwa cha habari kinanyosema; nisiwachoshe wafiwa,mh Rais ndo kama tulivyosikia; na kwa mujibu ya katiba yetu mama Samia ndo atakua Rais wetu kwa muda uliobaki hadi 2025. Sasa swali linakuja, atakua rais wa awamu ya sita....au ya tano inaendelea!?
 
Maisha ya mwanadamu hapa ulimwenguni ni hadithi, basi kuwa hadithi nzuri kwa wale watakao simuliwa hadithi yako.

Sote ni wa mwenyezimungu, na kwake yeye tutarejea.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…