PreGE2025 POTOSHI Rais wa TEC amesema ana imani kubwa na Jeshi la polisi

PreGE2025 POTOSHI Rais wa TEC amesema ana imani kubwa na Jeshi la polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu nmekutana na hili sijui gazeti sijui kipeperushi kikielezea kuwa Rais wa TEC amesema ana imani na jeshi la polisi na amewasailiana na IGP Wambura kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Katibu wa TEC Padre charles Kitima wanadai ni kutokana na mahojiano aliyoyafanya na Dw, Je ni kweli?
POSHI_TEC.jpg
 
Tunachokijua
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania yaani Tanzania Episcopal Conference (TEC),Askofu Pisa Wolfgang alifanyiwa mahojiano na kituo cha Deustche Welle chenye makao yake makuu nchini Ujerumani kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Katibu mkuu mkuu wa Baraza hilo, Padre Charles Kitima.

Kwa mujibu wa Taarifa ya polisi Padre Kitima alishambuliwa usiku wa April 30, 2025 alipokuwa maeneo ya ofisi za TEC Kurasini, Dar es laam ambapo hadi sasa wanamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na tukio hilo.

Madai

Kumekuwapo na kipeperushi kijulikanacho kwa jina la ‘Kishindo cha kutetemesha’ kinachosambaa mtandaoni kikiwa na tarehe ya Mei 1, 2025 kikiwa na Taarifa inayosomeka “RAIS WA TEC: TUNAYO IMANI KUBWA NA JESHI LA POLISI”. Taarifa hiyo imeambatana na maelezo mbalimbali huku ikidai kuwa Rais wa TEC aliitoa kauli hiyo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha kimataifa cha DW ( Deustche Welle).

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefnya ufuatiliaji na kubaini kuwa Taarifa hiyo inapotosha. Ufuatiliaji umebaini kuwa ni kweli Rais wa TEC alifanya mahojiano na kituo cha DW yaliyorushwa katika matangazo yao ya mchana na kuwekwa Youtube ambapo katika mahojiano yake yote aliyofanyiwa hakusema kuwa ana imani kubwa na jeshi la polisi. Matangazo ya DW Mei 1, 2025 mchana yamehifadhiwa hapa, na mahojiano kwa kirefu yaliyowekwa katika mtandao wa Youtube yamehifadhiwa hapa.

Taarifa iliyopo kwenye kipeperushi hicho inaeleza kwa kumnukuu Rais wa TEC “Nimekuwa na mawasiliano mazuri na Jeshi la polisi tangu kutokea kwa suala hilo yakiwemo na IGP Wambura wamekuwa wakitupa ushirikiano mkubwa”. Ufuatiliaji umebeini ni kweli katika mahojiano hayo Askofu Pisa alisema wamewasiliana na polisi pamoja na serikali lakini hakutaja kuwa amewasiliana na IGP Wambura.

JamiiCheck imefuatilia pia madai yaliyomo kwenye kipeperushi hiko ya kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wametoa tamko kuhusiana na tukio hilo kwa lugha ya kiingereza wakati wafuatiliaji wake ni waswahili na kubaini kuwa ni potoshi. CHADEMA wametoa tamko la kulaani tukio hilo kwa lugha zote mbili yaani Kiswahili na Kiingereza. Tazama hapa tamko la kiswahili na hapa tamko la kiingereza.

Ufuatiliaji pia umebaini kuwa madai yaliyowekwa kwenye kipeperushi hiko yanayodai kuwa mume wa Maria Sarungi amekamatwa na madawa ya kulevya si ya kweli, ambapo JamiiCheck ilifuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Tazama hapa kuona ufuatiliaji wa madai hayo uliofanywa na JamiiCheck April 17, 2025.

Aidha TEC wametoa tamko lao Mei 1, 2025 kuhusu kuvamiwa kwa katibu wao mkuu Padre Charles Kitima. Katika taarifa hiyo TEC imeonesha kusikitishwa kwakwe na kulitaka jeshi la polisi kuchukua hatua za haraka za kuwabaini na kuwakamata wale wote waliohusika katika kupanga na kutekeleza uhalifu huo. Tazama hapa
Mh gazeti linaitwa kishindo, Mbona kama utapeli wa waziwazi huu
 
Wakuu nmekutana na hili sijui gazeti sijui kipeperushi kikielezea kuwa Rais wa TEC amesema ana imani na jeshi la polisi na amewasailiana na IGP Wambura kuhusu tukio la kushambuliwa kwa Katibu wa TEC Padre charles Kitima wanadai ni kutokana na mahojiano aliyoyafanya na Dw, Je ni kweli?
View attachment 3322167
Hii ni kazi ya Wanaccm.

Yaan wanaccm mambo Yao lazima ujue tu hili ni la CCM.


Cheki gazeti lilivyoandikwa, mistari miwili tu unajua ni CCM .
 
Back
Top Bottom