GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kwa hiyo inatakiwa utoe ufafanuzi ya kwamba wamekamatwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kipindi cha uongozi wao na sio kama taarifa inavyosema kuwa wamekutwa wakitoa rushwa kwa wajumbe. Pia inabidi uelewe ya kwamba hizi bado ni tuhuma tu zitakuwa valid baada ya kuthibitishwa na mahakama, kipindi cha uchaguzi kina mambo mengi sana, jiulize kwanini wakamatwe sasa? Kuna kikundi cha watu kinatengeneza mazingira baada ya kuona Malinzi njia nyeupe urais kwa Mara ya pili, hawatamuweza kwani huu ni mchezo wa kitoto sana
Acha ' Upuuzi ' Wewe ' System ' ikiamua haishindwi kitu. Sasa kwa taarifa yako ili kummaliza zaidi anaweza akahojiwa hapo na haraka haraka akapelekwa Mahakama ya Ufisadi huku akiwekwa bado ' ndani ' halafu ili ujue kuwa ' System ' imebobea / imetukuka ' Kimafia ' Kesi yake inaweza ikawa inarushwa rushwa hadi mwezi August huku akinyimwa ' dhamana ' kwa Kigezo cha Kesi yake kuwa ' nzito ' halafu huku nyuma akina Mayai na Mtemi wanasafishiwa ' njia ' na Kesi yake inaweza ikasikilizwa siku mbili au tatu baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF kufanyika na kumaliza na ' ikala ' Kwake.
Hii ni ' Hesabu ' kali na ya ' Kimafia ' ambayo atake asitake imeshammaliza Rais wa TFF Jamal E. Malinzi. Ili ujue na uamini ninachokuambia Mkuu hakuna ' Mdau ' yoyote wa Soka la Bongo na hasa Siasa za pale TFF aliyekuwa hajui kuwa kwa Kipindi kirefu sana ' Uhusiano ' kati ya Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa ulikuwa ni ' mbaya ' na ilifikia muda wawili hawa walikuwa hata hawaongei bali walikuwa wakiongea kwa kutumia tu Emails na kama hii haitoshi kuna muda ulifika Katibu Mkuu wa TFF alikuwa ' akisusa ' kufanya Kazi.
Sasa ili ujue kuwa ule msemo wa ' Wahenga ' usema ' Kikulacho Ki nguoni mwako ' haukuanzishwa kwa bahati mbaya bali una maana yake jiulize kama hawa Wawili Malinzi na Mwesigwa walikuwa ni ' Maadui ' iweje ghafla tu wawe ' Marafiki ' kiasi cha hadi wao wawili kukubaliana ' Kushirikiana ' kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa TFF?
Hapana chezea ' System ' Wewe!