Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Acha ' Upuuzi ' Wewe ' System ' ikiamua haishindwi kitu. Sasa kwa taarifa yako ili kummaliza zaidi anaweza akahojiwa hapo na haraka haraka akapelekwa Mahakama ya Ufisadi huku akiwekwa bado ' ndani ' halafu ili ujue kuwa ' System ' imebobea / imetukuka ' Kimafia ' Kesi yake inaweza ikawa inarushwa rushwa hadi mwezi August huku akinyimwa ' dhamana ' kwa Kigezo cha Kesi yake kuwa ' nzito ' halafu huku nyuma akina Mayai na Mtemi wanasafishiwa ' njia ' na Kesi yake inaweza ikasikilizwa siku mbili au tatu baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF kufanyika na kumaliza na ' ikala ' Kwake.

Hii ni ' Hesabu ' kali na ya ' Kimafia ' ambayo atake asitake imeshammaliza Rais wa TFF Jamal E. Malinzi. Ili ujue na uamini ninachokuambia Mkuu hakuna ' Mdau ' yoyote wa Soka la Bongo na hasa Siasa za pale TFF aliyekuwa hajui kuwa kwa Kipindi kirefu sana ' Uhusiano ' kati ya Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa ulikuwa ni ' mbaya ' na ilifikia muda wawili hawa walikuwa hata hawaongei bali walikuwa wakiongea kwa kutumia tu Emails na kama hii haitoshi kuna muda ulifika Katibu Mkuu wa TFF alikuwa ' akisusa ' kufanya Kazi.

Sasa ili ujue kuwa ule msemo wa ' Wahenga ' usema ' Kikulacho Ki nguoni mwako ' haukuanzishwa kwa bahati mbaya bali una maana yake jiulize kama hawa Wawili Malinzi na Mwesigwa walikuwa ni ' Maadui ' iweje ghafla tu wawe ' Marafiki ' kiasi cha hadi wao wawili kukubaliana ' Kushirikiana ' kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa TFF?

Hapana chezea ' System ' Wewe!
Does FIFA operate that way? Let us wait and see
 
The Rise and Fall of Malinzi Jamal. Kuna mdau mmoja alinitukana humu kisa Malinzi nilipomuambia huyo ni fisadi namtafuta kwa udi na uvumba.
Jamaa mmoja hivi anaitwa [HASHTAG]#Frank[/HASHTAG] wanjiru hata Mimi alinitusi!
Jamaa alikuwa anamtetea malinzi kinoma!sijui alikuwa malinzi mwenyewe!
 
Hapo ndio patakuwa pagum,yatatokea kama yaliyotokea ya Ndolanga na usishangae tukafyata mkia
Exactly, FIFA does not operate that way. Waliwahi kumfanyia figisu ikaenda FIFA wakatupilia mbali upuuzi akashinda!
Hizi ni figisu za wazi na siyo mara ya kwanza kumuita huko, several times. Hili limekuwa la nguvu kwa ajili ya uchaguzi.
 
Safi sana,malinzi alikuwepo Tff kwa maslahi yke binafsi...tumbo kubwa kubwa kama pipa tu kwanza

Ova
 
Habari njema kwa wana msimbazi.....

Habari mbaya kwa wana jangwani......


ANGUKO LA YANGA LINAKWENDA SAMBAMBA NA VIBARAKA WAO PALE TIFUA TIFUA.....

KILA MTU ATAVUNA KILE ALICHOKIPANDA....


CELEBRATIONS TIME.....

3cc61aebb95caaaeb270a39314630939.jpg
ALLY%2BMAYAY%2BNA%2BCHAMA.jpg


Chama vs Mayai
 
Ilibidi akutukane, una ushahidi gani kuwa ni fisadi? Mbona kuitwa PCCB ni kawaida kwa watu wenye majukumu, wana maadui wengi kiasi lazima wapeleke umbea pccb. Sioni ajabu.
Hahahaahaha nendeni sasa mkamuekee dhamana cheza na serikal awamu ya 5...shubaaamiit
 
Hivi kumbe huko TFF kuna hela mpaka kufikia kutoa rushwa maanake mimi naonaga hamna hata kitu huko!!!
Mkuu kuna hela ya kufa mtu kwa maisha yetu ya Kitanzania si haba...kama kuna kipindi TFF walitoka Karume na kwenda kupanga ofisi kwa milioni 400 ni kielelezo tosha kuna hela kwa maisha yetu ya kibongo hivyo mtu akiingia kwa misingi ya rushwa kuna uwezekano wa kutafuta vijisenti vya kuendeshea maisha though wengine ni shortcut ya kufikia mataajio yao ya kisiasa kwa siku za usoni ndo maana watu hujifanya watu wa soka alafu jina likivuma unaona anahamia kwenye siasa
 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Jamal Malinzi amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini(TAKUKURU) akiwa katika harakati za kutembeza Mlungula.

Hatimae "Danganya Toto" ya Malinzi sasa imefikia kikomo.

Taarifa zaidi, zitakujia kupitia Uzi huu...

=====
UPDATE:
5d33c4389fb4ac0e184df79b48284a85.jpg

Jamal Malinzi
9d00e86a6e1309c125c313431a0c0257.jpg

Celestine Mwesigwa

Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Kwa matumizi mabaya ya Ofisi.
Good.Hongereni vijana keep it up.Hawa ndio wanaokichafua chama na serikali.Deal with them harshly if proved guilty.Tumechoka kuwa mocked mitaani.
 
Back
Top Bottom