Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Exactly, FIFA does not operate that way. Waliwahi kumfanyia figisu ikaenda FIFA wakatupilia mbali upuuzi akashinda!
Hizi ni figisu za wazi na siyo mara ya kwanza kumuita huko, several times. Hili limekuwa la nguvu kwa ajili ya uchaguzi.
Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa haimuachi mtu..Hata kama FIFA watamuachia lakini sheria za nchi zitamshughulikia.
 
daaah aende tu huyu jamaa. alishindwa vibaya mno pale TFF. hata ratiba ya ligi tu ilimshinda kupanga.
Hujui unaloliongea, anayepanga ligi ni kamati husika na si mwenyekiti pekee yake,. ondoa mtima nyongo usio na sababu ya msingi.
 
Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa haimuachi mtu..Hata kama FIFA watamuachia lakini sheria za nchi zitamshughulikia.
Si mpaka uthibitishe? Mnashangilia nini? Na hakuna uthbitisho ni figisu tu
 
Safi sana ila naomba kuuliza swali: Kukamatwa kwa Jamal E. Malinzi kunamuondolea sifa ya kugombea Urais wa TFF?
 
Wana taratibu zao! Tafuta utaona.
nimezitafuta sijaona walipo na uwezo wa kumtetea/kuingilia mhalifu/mtuhumiwa anayeshikiliwa na mamlaka za nchi yake, ila hawako tayar kuona serikali inaingilia masuala ya mpira. Rejea sakata la Blatter, huwa fifa haiwezi kusimama kumtetea mtu asihukumiwe au asikamatwe kama kuna sheria kavunja.......kuna masakata ya kina Messi, Ronaldo, Neymar kuitwa kortini kwa kesi za kodi, na wapo wacheaji pia wamefungwa gerezeni kwa makosa yao ila hakuna siku hata moja FIFA wametetea au kuingilia maswala hayo.
Malinzi na mwenzake sio kesi ya soka kabisa ila tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi/fedha za shirikisho.
 
Shule sio kigezo.
1. Sep Blatter hakuwa na shule
2. Uongozi ni jinsi unavyo endesha Taasisi unayoiongoza huku ukiwa na dhamira ya kweli moyoni wala sinkwa mtazamo wa kujinufaisha binafsi.
3. Mbona kule sifa ni kusoma na kuandika na bado watu wanaongoza!!
4. Ally Mayai anafaa sana kwa sababu, secretariet ndio mtendaji, yeye anakuwa ni figure tu.
Humfahamu Ally Mayay wewe, Yule alikuwa Mwalimu kwa Taaluma yake, baadae akaenda kujiendeleza pale CBE ni afisa fulani kwenye Taasisi X na mpira ni kipaji toka utoto wake akiwa na Polisi Shirati.
 
Hii taarifa ni ya uongo ulio dhahiri, Malinzi sio mjinga aanze kuhonga mapema namna hii na wakati hata mchujo wa wagombea haujakamilika wala kampeni kuanza. Kumbukeni wajumbe wanaopiga kura ni wengi wao ni wenyeviti wa mikoa, ni lini wamekuja Dar mpaka waanze kuhongwa na Malinzi? Uchaguzi unafanyika August Malinzi aanze kuhonga leo ana pesa kiasi gani? Kwa taarifa yenu chaguzi hizi rushwa huwa inatembea siku wajumbe wanafika kutoka mikoani na siku ya kupiga kura na sio sasa!
Ww ni tomaso
 
Hujui unaloliongea, anayepanga ligi ni kamati husika na si mwenyekiti pekee yake,. ondoa mtima nyongo usio na sababu ya msingi.
kwa akili yako ile kamati inajichagua yenyewe. na kamati zilizo chini ya Rais kama zinakosea kila siku who's to blame ?.
 
Wangemkamata na yule mpiga debe wake hapa JF Wanjiru
 
Back
Top Bottom