Does FIFA operate that way? Let us wait and seeAcha ' Upuuzi ' Wewe ' System ' ikiamua haishindwi kitu. Sasa kwa taarifa yako ili kummaliza zaidi anaweza akahojiwa hapo na haraka haraka akapelekwa Mahakama ya Ufisadi huku akiwekwa bado ' ndani ' halafu ili ujue kuwa ' System ' imebobea / imetukuka ' Kimafia ' Kesi yake inaweza ikawa inarushwa rushwa hadi mwezi August huku akinyimwa ' dhamana ' kwa Kigezo cha Kesi yake kuwa ' nzito ' halafu huku nyuma akina Mayai na Mtemi wanasafishiwa ' njia ' na Kesi yake inaweza ikasikilizwa siku mbili au tatu baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF kufanyika na kumaliza na ' ikala ' Kwake.
Hii ni ' Hesabu ' kali na ya ' Kimafia ' ambayo atake asitake imeshammaliza Rais wa TFF Jamal E. Malinzi. Ili ujue na uamini ninachokuambia Mkuu hakuna ' Mdau ' yoyote wa Soka la Bongo na hasa Siasa za pale TFF aliyekuwa hajui kuwa kwa Kipindi kirefu sana ' Uhusiano ' kati ya Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa ulikuwa ni ' mbaya ' na ilifikia muda wawili hawa walikuwa hata hawaongei bali walikuwa wakiongea kwa kutumia tu Emails na kama hii haitoshi kuna muda ulifika Katibu Mkuu wa TFF alikuwa ' akisusa ' kufanya Kazi.
Sasa ili ujue kuwa ule msemo wa ' Wahenga ' usema ' Kikulacho Ki nguoni mwako ' haukuanzishwa kwa bahati mbaya bali una maana yake jiulize kama hawa Wawili Malinzi na Mwesigwa walikuwa ni ' Maadui ' iweje ghafla tu wawe ' Marafiki ' kiasi cha hadi wao wawili kukubaliana ' Kushirikiana ' kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa TFF?
Hapana chezea ' System ' Wewe!