Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU


Acha ' Upuuzi ' Wewe ' System ' ikiamua haishindwi kitu. Sasa kwa taarifa yako ili kummaliza zaidi anaweza akahojiwa hapo na haraka haraka akapelekwa Mahakama ya Ufisadi huku akiwekwa bado ' ndani ' halafu ili ujue kuwa ' System ' imebobea / imetukuka ' Kimafia ' Kesi yake inaweza ikawa inarushwa rushwa hadi mwezi August huku akinyimwa ' dhamana ' kwa Kigezo cha Kesi yake kuwa ' nzito ' halafu huku nyuma akina Mayai na Mtemi wanasafishiwa ' njia ' na Kesi yake inaweza ikasikilizwa siku mbili au tatu baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF kufanyika na kumaliza na ' ikala ' Kwake.

Hii ni ' Hesabu ' kali na ya ' Kimafia ' ambayo atake asitake imeshammaliza Rais wa TFF Jamal E. Malinzi. Ili ujue na uamini ninachokuambia Mkuu hakuna ' Mdau ' yoyote wa Soka la Bongo na hasa Siasa za pale TFF aliyekuwa hajui kuwa kwa Kipindi kirefu sana ' Uhusiano ' kati ya Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa ulikuwa ni ' mbaya ' na ilifikia muda wawili hawa walikuwa hata hawaongei bali walikuwa wakiongea kwa kutumia tu Emails na kama hii haitoshi kuna muda ulifika Katibu Mkuu wa TFF alikuwa ' akisusa ' kufanya Kazi.

Sasa ili ujue kuwa ule msemo wa ' Wahenga ' usema ' Kikulacho Ki nguoni mwako ' haukuanzishwa kwa bahati mbaya bali una maana yake jiulize kama hawa Wawili Malinzi na Mwesigwa walikuwa ni ' Maadui ' iweje ghafla tu wawe ' Marafiki ' kiasi cha hadi wao wawili kukubaliana ' Kushirikiana ' kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa TFF?

Hapana chezea ' System ' Wewe!
 
Kwa hiyo siyo tetesi tena? Neno tetesi liondolewe
 
Hadi muda huu yuko Polisi?

Nadhani watakuwa Ofisi za TAKUKURU ila kama itagundulika kweli wana hizo ' tuhuma ' basi ' fasta ' watapelekwa Police kwa taratibu zingine kisha ' Mahakama ' ya Ufisadi ambapo kwa Kifungo cha chini sana kwa ' makosa ' ambayo nimesikia kuwa yapo kati ya matano hadi saba anaweza akala ' mvua ' 65 hivyo kumfanya awe Rais wa maisha wa TFF ya ' Wafungwa ' huko Gerezani.
 
A
Kuna mgombea yuko TRA, sio Ali Tembele..
Anaitwa Ally Mayai Tembele
Hivi yupo TRA au Wizara ya Viwanda na Biashara kama Afisa Masoko(?)
Ngoja watakuja kutusahihisha mkuu,tusubiri wenye uhakika
 
Kumbe kutoa rushwa inaweza kumpeleka kwenye ufisadi, uwiiiiiiiiiiiiiiiii!! kuanzia natamka hadharani rushwa nooooo!!!!
 
Kumbe kutoa rushwa inaweza kumpeleka kwenye ufisadi, uwiiiiiiiiiiiiiiiii!! kuanzia natamka hadharani rushwa nooooo!!!!

Hana tu Kosa la kutoa rushwa Mkuu bali ana tuhuma zingine za ubadhirifu ( Ufisadi ) wa Pesa za TFF kinyume na matumizi yake ambayo yalikusudiwa.
 
daaah aende tu huyu jamaa. alishindwa vibaya mno pale TFF. hata ratiba ya ligi tu ilimshinda kupanga.
Ratiba upangwa na bodi ya ligi,ambayo inaongozwa na nyange kaburu ,huyu nyange kaburu kwa 65% ndio atakuwa makamu wa rais ajaye wa tff,labda tu takukuru nae imuangalie kwa jicho la 3
 
Hana tu Kosa la kutoa rushwa Mkuu bali ana tuhuma zingine za ubadhirifu ( Ufisadi ) wa Pesa za TFF kinyume na matumizi yake ambayo yalikusudiwa.
ooooooooooooooooops! iwe bojo kazirooo! sasa hawa ndugu zangu infwact, wengi wana hizo tuhuma!! nimewaza na yule escrow
 
Hii ni salam tosha kwa CCM maana kuna wabunge wengi wamepita kwa rushwa
 
Tujiulize mpaka mtu anahonga kuna nini huko TFF? Atarudishaje hizo hela anazohonga? Tangu ameingia madarakani Nchi yetu imeendelea kuporoomoka kwenye viwango vya FIFA na bado anataka kugombea tena? anagombea ili nini? Nchi ya Kijuha sana hii.. Kama PCCB wana ushahidi wa kumtia hatiani wamfunge kabisa ili iwe fudisho!
 

Hakuna Kipindi ambacho TAKUKURU / PCCB wanapiga Kazi kama sasa Mkuu. Tegemea mengi zaidi siku za usoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…