Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

EFM wamethibitisha,Clouds Fm wamethibitisha. Halafu sio kuonga ni kutumia vibaya madaraka yao,walikua wanakula pesa za TFF.
Kwa hiyo inatakiwa utoe ufafanuzi ya kwamba wamekamatwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kipindi cha uongozi wao na sio kama taarifa inavyosema kuwa wamekutwa wakitoa rushwa kwa wajumbe. Pia inabidi uelewe ya kwamba hizi bado ni tuhuma tu zitakuwa valid baada ya kuthibitishwa na mahakama, kipindi cha uchaguzi kina mambo mengi sana, jiulize kwanini wakamatwe sasa? Kuna kikundi cha watu kinatengeneza mazingira baada ya kuona Malinzi njia nyeupe urais kwa Mara ya pili, hawatamuweza kwani huu ni mchezo wa kitoto sana
 
Hii taarifa ni ya uongo ulio dhahiri, Malinzi sio mjinga aanze kuhonga mapema namna hii na wakati hata mchujo wa wagombea haujakamilika wala kampeni kuanza. Kumbukeni wajumbe wanaopiga kura ni wengi wao ni wenyeviti wa mikoa, ni lini wamekuja Dar mpaka waanze kuhongwa na Malinzi? Uchaguzi unafanyika August Malinzi aanze kuhonga leo ana pesa kiasi gani? Kwa taarifa yenu chaguzi hizi rushwa huwa inatembea siku wajumbe wanafika kutoka mikoani na siku ya kupiga kura na sio sasa!
Umeongea uhalisia!
 
Sheria za mpira zinasemaje kwa yule aliye na kashfa kama hizo bado anazo sifa za kuwa mgombea hadi mahakama ithibitishe?
Kwann hizi kashfa zinaibuka wakati huu wa uchaguzi? Je uko nyuma zilikuwa azijatambulika?
 
Ni aibu kubwa kwa mgombea wa Urais kukutwa na tuhuma,tuhuma tu inaonyesha hafai tena kuwa Rais.
 
Hata hao wanaohongwa alafu na wanamchagua kweli nao wanatakiwa wasome alama za nyakati...hivi ukila hela ya rushwa ambayo sio halali alafu ukienda kumpigia mwingine sijui utakosa nini maana jamaa akiingia kama sio kikwazo kwake hela aliyokuhonga ndio hiyo hiyo labda kwa wale wenye ushawishi nd pamoja na kwamba alikupa rushwa bado ataendelea kukuziba mdomo katika kipindi chake chote cha uongozi
Hivi kumbe huko TFF kuna hela mpaka kufikia kutoa rushwa maanake mimi naonaga hamna hata kitu huko!!!
 
Sheria za mpira zinasemaje kwa yule aliye na kashfa kama hizo bado anazo sifa za kuwa mgombea hadi mahakama ithibitishe?
Kwann hizi kashfa zinaibuka wakati huu wa uchaguzi? Je uko nyuma zilikuwa azijatambulika?
Skendo za malinzi refer kashfa yake ya upangaji matokeo na rushwa na uthibitisho ulitolewa mwaka Jana
 
Hii taarifa ni ya uongo ulio dhahiri, Malinzi sio mjinga aanze kuhonga mapema namna hii na wakati hata mchujo wa wagombea haujakamilika wala kampeni kuanza. Kumbukeni wajumbe wanaopiga kura ni wengi wao ni wenyeviti wa mikoa, ni lini wamekuja Dar mpaka waanze kuhongwa na Malinzi? Uchaguzi unafanyika August Malinzi aanze kuhonga leo ana pesa kiasi gani? Kwa taarifa yenu chaguzi hizi rushwa huwa inatembea siku wajumbe wanafika kutoka mikoani na siku ya kupiga kura na sio sasa!
Unaushahidi wowote wa kukanusha hili au unaleta utetezi usikuwa na tija? Mpaka sasa ni tetesi na habari hizo ziko kila kona basi ajitokeze akanushe sio kukutuma wewe bila data
 
  • Thanks
Reactions: Dkt
Apewe huyo afisa wa TRA.. bila shaka hana Ushabiki wa klabu hizi mbili. Malinzi aliegemea mno upande mmoja.
Yupo Wizara ya Viwanda na Biashara na si TRA
Alimaliza CBE,Mayayi anajielewa,aliamua kuacha mpira huku akiwa na nguvu ili arudi shule kujiendeleza
Suala la kuegemea upande mmoja huwezi kulisema kabla mtu hajaaingia madarakani,Ally Mayayi ni mchezaji wa zamani ya Yanga,mpenzi na mwanachama mwenye kadi ya Yanga.

Kwenye uongozi wa soka Tz,huwezi kukwepa Usimba na Uyanga
 
Shule sio kigezo.
1. Sep Blatter hakuwa na shule
2. Uongozi ni jinsi unavyo endesha Taasisi unayoiongoza huku ukiwa na dhamira ya kweli moyoni wala sinkwa mtazamo wa kujinufaisha binafsi.
3. Mbona kule sifa ni kusoma na kuandika na bado watu wanaongoza!!
4. Ally Mayai anafaa sana kwa sababu, secretariet ndio mtendaji, yeye anakuwa ni figure tu.
Btw, Ally Mayai hana shule?
 
Yupo Wizara ya Viwanda na Biashara na si TRA
Alimaliza CBE,Mayayi anajielewa,aliamua kuacha mpira huku akiwa na nguvu ili arudi shule kujiendeleza
Suala la kuegemea upande mmoja huwezi kulisema kabla mtu hajaaingia madarakani,Ally Mayayi ni mchezaji wa zamani ya Yanga,mpenzi na mwanachama mwenye kadi ya Yanga.

Kwenye uongozi wa soka Tz,huwezi kukwepa Usimba na Uyanga
Kuna mgombea yuko TRA, sio Ali Tembele..
 
Back
Top Bottom