Muharango
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 1,663
- 1,037
Sio yake tu , Maslai ya CCM na wezi wenzie ambao wanajifanya kuvaa mewani ya mbao!Safi sana,malinzi alikuwepo Tff kwa maslahi yke binafsi...tumbo kubwa kubwa kama pipa tu kwanza
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio yake tu , Maslai ya CCM na wezi wenzie ambao wanajifanya kuvaa mewani ya mbao!Safi sana,malinzi alikuwepo Tff kwa maslahi yke binafsi...tumbo kubwa kubwa kama pipa tu kwanza
Ova
Utashanga kuona jamaa wanatusuaSio yake tu , Maslai ya CCM na wezi wenzie ambao wanajifanya kuvaa mewani ya mbao!
Taarifa ni za kweli, anashikiliwa na pccb tokea jana. Ila moja kati ya tuhuma zake, ni ubadhirifu wa fedha za tff na matumizi mabaya ya madaraka.Hii taarifa ni ya uongo ulio dhahiri, Malinzi sio mjinga aanze kuhonga mapema namna hii na wakati hata mchujo wa wagombea haujakamilika wala kampeni kuanza. Kumbukeni wajumbe wanaopiga kura ni wengi wao ni wenyeviti wa mikoa, ni lini wamekuja Dar mpaka waanze kuhongwa na Malinzi? Uchaguzi unafanyika August Malinzi aanze kuhonga leo ana pesa kiasi gani? Kwa taarifa yenu chaguzi hizi rushwa huwa inatembea siku wajumbe wanafika kutoka mikoani na siku ya kupiga kura na sio sasa!
TAKUKURU wamechukua simu zao zote!!Jamal E. Malinzi hakuhitaji kwenda kwa ama Mtabiri au Mganga wa Kienyeji kujua kwamba hatakiwi ' totally ' na System. Sasa naiona njia nyeupe kwa Ally Mayai Tembele kuwa Rais wa TFF na Mzee Mtemi Ramadhan kuwa Makamu wa Rais wa TFF. Katika hili Jamal E. Malinzi Rais wa TFF ndiyo ' ameshajimaliza ' mwenyewe na kuna uwezekano mkubwa Watu wake wa karibu na ambao anawaamini ndiyo walikuwa ' planted ' Kwake kummaliza bila Yeye kujua au kushtukia mchezo.
Nadhani watakuwa Ofisi za TAKUKURU ila kama itagundulika kweli wana hizo ' tuhuma ' basi ' fasta ' watapelekwa Police kwa taratibu zingine kisha ' Mahakama ' ya Ufisadi ambapo kwa Kifungo cha chini sana kwa ' makosa ' ambayo nimesikia kuwa yapo kati ya matano hadi saba anaweza akala ' mvua ' 65 hivyo kumfanya awe Rais wa maisha wa TFF ya ' Wafungwa ' huko Gerezani.
Taarifa ni za kweli, anashikiliwa na pccb tokea jana. Ila moja kati ya tuhuma zake, ni ubadhirifu wa fedha za tff na matumizi mabaya ya madaraka.
Kinara wa hayo yote, ni makamu wa raisi wa sasa anayemaliza muda wake. Naye ameomba nafasi ya uraisi ktk uchaguzi mkuu ujao. Kama zilivyo chaguzi nyingine, fitna huwa haziepukiki, zengwe limetengenezwa kipindi hiki, ili wamshikilie ashindwe kwenda kwenye usahili kesho. Na mgombea akishindwa kufika kwenye usahili, anakuwa amejitoa.
Kwa kadiri nnavyomfahamu jamal, atatoa ushirikiano wa kutosha Kwa pccb ili wakamilishe uchunguzi wao, na wampeleke mahakamani mapema. Kutuhumiwa hakuzii mtu kugombea, nnaimani mahakama itatenda haki, na kumpatia dhamana. Baada ya dhamana, anarudi kuendelea na mapambano ya kutetea nafasi yake.
Ili iweje? ktk ubinadamu hakuna aliyekamilika kama ulivyo wewe au mimi. Jamal ana mapungufu yake pia kama mwanadamu mwingine.Kutetea ulaji wake.
Ili iweje? ktk ubinadamu hakuna aliyekamilika kama ulivyo wewe au mimi. Jamal ana mapungufu yake pia kama mwanadamu mwingine.
Ni mtazamo wako pia... me huwa naheshinu sana mtazamo wa mtu. Ila kwa mtazamo wangu mimi, bado anafaa. Kama kuna vitu kakosea, ni suala la kumrekebisha tu.Hafai.
kwahiyo anaenda kukutana na RUGE?Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Jamal Malinzi amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini(TAKUKURU) akiwa katika harakati za kutembeza Mlungula.
Hatimae "Danganya Toto" ya Malinzi sasa imefikia kikomo.
Taarifa zaidi, zitakujia kupitia Uzi huu...
=====
UPDATE:
Jamal Malinzi![]()
Celestine Mwesigwa![]()
Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Kwa matumizi mabaya ya Ofisi.
======
UPDATES:
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kwamba Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi na katibu mkuu wake Celestine Mwesigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 28, June, 2016 walikatamatwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini – TAKUKURU na huenda leo wakafikishwa mahakama ya mkazi Kisutu kujibu mashtaka juu ya matumizi mabaya ya ofisi.
Kwa muda mrefu kumekuwepo na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na inasemekana TAKUKURU wamekuwa kwenye uchunguzi dhidi kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatiwa nguvuni.
Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.
JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA KUTISHA TFF, Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.
Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.
Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.
Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).
Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.
Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.
Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.
Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza
====
Ndugu mwanaJF, rejea thread hizi nilizowahi kuleta kuhusiana na Ufisadi wa Jamal Malinzi na Timu yake.
1: UFISADI TFF: Bil 1.1 zachotwa ndani ya wiki 1, PCCB washikwa na kigugumizi kumpeleka Malinzi Kortini
2: UFISADI TFF: Malinzi mwogope Mungu, Fedha za TBL dola 425,000 umezichota kutoka akaunti hizi
Ni mtazamo wako pia... me huwa naheshinu sana mtazamo wa mtu. Ila kwa mtazamo wangu mimi, bado anafaa. Kama kuna vitu kakosea, ni suala la kumrekebisha tu.
Njia iliyo tumika mbona ni sahihi tena fifa wataipongeza Tz kwa kuwadaka wahujumu mpira.... Blatteq nae alijisahau kumbe FBI wamesha penyeza watu, akaja kuingia kingi kiulaini...Does FIFA operate that way? Let us wait and see
Ni mtazamo wako pia... me huwa naheshinu sana mtazamo wa mtu. Ila kwa mtazamo wangu mimi, bado anafaa. Kama kuna vitu kakosea, ni suala la kumrekebisha tu.
Amejitahidi sana kuendesha soka letu, na ameweza maeneo mengi. Mifano michache tu ni kama program za soka la vijana. Kuwekeza kwa vijana wa u14 na u17 ni faida kubwa sana kwa nchi maana ndio stars ya siku za usoni. Ligi kuu ya wanawake imewezekana chini uongozi wake, tzu17 imeshiriki afcon kwa kiwango kizuri kabisa etc...Hafai uyo fisadi,soka letu linakufa. Yeye kaendekeza kula pesa za TFF tu.