Rais wa TLS anazungumza na Waandishi wa Habari, akosoa Polisi, amtaja Muliro

Hivi ndivyo inavyotakiwa wasomi kusema kweli daima juu ya mifumo ovu ya kukandamiza inayokamata ovyo, kuumiza, kupiga, kutupa watu porini n.k nje ya mfumo rasmi wa haki jinai.
 
Kwa utamaduni wa mfumo wa haki jinai, hukumu za nchi za Commonwealth hutumika kama rejeo :

Mahakamani kunaweza kuleta taharuki hivyo kwa kisingizio cha sheria ya 'Preventive Detention' Polisi wanaweza kukuzuia au kukutoa eneo moja na kukutupa pengine

24 Aprili 2025
TOKA KISUTU HADI UNUNIO

View: https://m.youtube.com/watch?v=3sKHvyb5Z28

April 30th, 2025

MAHAKAMA KUU YATOA HUKUMU YA KIHISTORIA, POLISI HAWARUHUSIWI KUFICHA NYUSO ZAO AU KUVAA KININJA WANAPOKWENDA KUTAWANYA MAANDAMANO

Mahakama hiyo pia imeamuru watu walioumizwa na Polisi kulipwa fidia

WAANDAMANAJI 11 wamefidiwa Sh 200, 000 kila mmoja na Mahakama Kuu ya Kenya baada ya polisi kukiuka haki zao wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.

Aidha, mahakama imeamua kuwa maafisa wa polisi wanaopelekwa kudumisha usalama wakati wa mikutano ya hadhara, maandamano au migomo lazima wavalie sare na wasifiche nyuso zao.

“Afisa yeyote anayeteuliwa kuhakikisha sheria na utulivu wakati wa mkutano wa hadhara, maandamano au migomo lazima awe kwenye sare rasmi, na asifiche uso wake kwa njia yoyote ile ili aweze kutambulika,” alisema Jaji Bahati Mwamuye.

Mahakama iliagiza Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuhakikisha kuwa maafisa wote waliotumwa kudhibiti maandamano au kutoa ulinzi kwa waandamanaji hawavai mavazi ya kiraia au kuvaa barakoa.

Maamuzi haya yalitokana na kesi ya Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) dhidi ya maafisa wawili wa polisi, Martin Mbae Kithinji na Isaiah Ndumba Murangiri, waliokuwa miongoni mwa waliotumwa kudhibiti maandamano ya Juni 2024.

LSK ilidai kuwa Bw Murangiri ndiye aliyehusika na kifo cha Rex Masai, mmoja wa waandamanaji aliyeripotiwa kupigwa risasi na polisi Juni 18, 2024 katika jiji la Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha.

Kulingana na LSK, visa vyote vya mauaji, ukatili wa polisi na unyanyasaji wa waandamanaji vinahusishwa na maafisa wasiovalia sare rasmi.

Mahakama ilisema kuwa kuvaa mavazi ya kiraia kuliwasaidia maafisa wa polisi kujichanganya na waandamanaji waliokuwa na amani.

Serikali iliagizwa kuwalipa waandamanaji — Joy Awich, Muthoni Matu, Kipng’etich Eman, Carolyne Mwikali, Stephen Obunde, Raymond Burgei, Felix Gatobu, Chatherine Njoki Njanja, Tim Kut, Wesley Tome na Imran Kasumba — jumla ya Sh2.2 milioni
 
Mahakama imetenda haki hizo Ksh 200,000 ni sawa na Tsh 4,200,000. Polisi watajua kuwa hawapo juu ya sheria.
 
Wakenya kwa kiasi kikubwa Sana wanajitambua ukilinganisha na waTanzania
 
Yaan nchi yetu...daaah..wanyonge wanapata tabu sana.....yaan kumbe kwa utashi wake tu hakimu annamua kuminya haki ya mtu kufurahisha affiliation zake
 
Back
Top Bottom