Rais wa UEFA Ceferin atoa Onyo kinachoendea Saudi Arabia

Rais wa UEFA Ceferin atoa Onyo kinachoendea Saudi Arabia

Rais wa UEFA Ceferin: "Usajili wanaoufanya SAUDIA ni makosa kwa soka la kwao. Wawekeze hizo pesa kwenye academy, walete makocha na waendeleze wachezaji wao wenyewe, kununua wachezaji wanaomalizia soka lao sio mfumo wa kuendeleza soka, kosa kama hilo walilifanya China.”

View attachment 2661869
Mbona wakienda kuwekeza ulaya hawakatazwi Tena wamechangia pakubwa sana kuufanya mpira upendeze.
Waache wajifrahishe bhna alaaaah
 
Kuna long term solution na short term solution.
Saudia wanataka WC, sasa hizi academy zitawasaidia nini kupata WC host?

#YNWA
Sjakuelewa..hizo long term na short unamaanisha solution za nini?
Maana WC host Qatar washaharibu mambo sodhan kama litarudi tena uarabuni ndani ya hii miaka 100 tuliyo hai
 
Kuna long term solution na short term solution.
Saudia wanataka WC, sasa hizi academy zitawasaidia nini kupata WC host?

#YNWA
Hata WC ni short solution,

Saudi wana Project yao inaitwa vision 2030 kuna vitu wanazindua kama Neom smart city, Red sea project na Roshn.

Wanachukua Wachezaji kutengeneza Attention sababu hizo project zao zinaendana na Utalii.

Hata world cup wanataka sababu ya vision 2030.

Tetesi hata Super League Africa wanaitaka nayo, Bilioni kama 400.
 
Huu ndio ushabiki maandazi sasa, mtu wa mpira huwezi kumuita Ronaldo garasa.
Wewe ndo unaleta ushabiki wako na utim ronaldo hapa.
Sasa mtu anakaa bench timu mbovu kama manU kuna mchezaji pale?

We ukiambiwa unatafuta matokeo mechi ngumu kwenye tim yako umchukue ronaldo au mayele utamchukua nan? Be honest kabisa.
(Na mimi sio yanga)
 
Sjakuelewa..hizo long term na short unamaanisha solution za nini?
Maana WC host Qatar washaharibu mambo sodhan kama litarudi tena uarabuni ndani ya hii miaka 100 tuliyo hai
Qatar sio Saudi, Qatar ni ki nchi kidogo, Saudi ni very powerfull wapo kila sehemu.

Pia Qatar ni moja kati ya world cup Bora kupata kutokea kwa wapenzi wa Soka, unless uingize siasa na mambo ya Ushoga.

World cup inayokuja kuna ushirikiano wa mataifa mbalimbali, wengi walioomba wameomba pamoja.

-Saudi, Egpty na Ugiriki ama Saudi na Egpty
-Ugiriki, Bulgaria na Romania
-Spain, Portugal na Morocco ama Spain, Portugal na Ukraine
-Chile, Uruguay, paraguay, Argentina

Hao ndo wanatajwa sana

Sababu Timu zinaongezeka hadi 48 ndio maana unaona Nchi zinaungana, itakua Ngumu sana kwa Nchi moja ku host, na Hapo ndio Saudi wanapojioenyeza, wao wana Hela wanaweza kutafuta Nchi za Africa ama Ulaya Mashariki, wakapenyeza hela na kuwaahidi kuwajengea Viwanja ili wahost.
 
Rais wa UEFA Ceferin: "Usajili wanaoufanya SAUDIA ni makosa kwa soka la kwao. Wawekeze hizo pesa kwenye academy, walete makocha na waendeleze wachezaji wao wenyewe, kununua wachezaji wanaomalizia soka lao sio mfumo wa kuendeleza soka, kosa kama hilo walilifanya China.”

View attachment 2661869
Hela inawawasha waache waitie kiberiti
 
Rais wa UEFA anataia huruma kaona msimu ujao kuanzia ESPN, na ndugu zake wengine wanagombania kuonesha ligi ya Saud arabia anaofia watapunguza wadhamnini kwenye ligi zao
Tuwe serious basi. Yaani Wadhamini waache kupigana vikumbo kwenye ligi yenye Mbappe, Haaland, De Brune, Jude Bellingham na mastaa wengine kibao, Wapungue waende kuonesha ligi za Waastafu?!

Tuwe tunajitahidi kupreview tunachoandika kabla hatujapost.
 
Huyo rais wa UEFA ni kilaza kama vilaza wengine tu.Lengo la Mwarabu ni kuipromote ligi yao iwe kubwa duniani na ukubwa wa ligi hauletwi na wachezaji wazawa tu.

Miaka ya 90 EPL haikuwa kubwa kama ilivyo leo hii, ligi zilizokuwa maarufu ni La liga na Serie A. Epl ilikuwa na wachezaji wengi wa kiingereza wakati hayo mataifa mengine yalivutia wachezaji wengi kwenda huko, Ligi zikakua na biashara nyingi zilifanyika na kupelekea mapato mengi.

The same kama wachezaji wakubwa wakienda Saudia , basi vyombo vya habari vitamulika kule, wachezaji wengi watashawishika kwenda, maslahi ni makubwa, haki za matangazo kwa klabu zitakuwa kubwa, mapato yatakuwa makubwa na automatically soka lao litakuwa kubwa.
 
Rais wa UEFA Ceferin: "Usajili wanaoufanya SAUDIA ni makosa kwa soka la kwao. Wawekeze hizo pesa kwenye academy, walete makocha na waendeleze wachezaji wao wenyewe, kununua wachezaji wanaomalizia soka lao sio mfumo wa kuendeleza soka, kosa kama hilo walilifanya China.”

View attachment 2661869
Naona vikwazo vinaanza taratibu
 
Nina uhakika hili lilikuwa ni swali kutoka kwa muandishi akijibu
Ameongea kitu Cha kweli sana tena na uwazi kama ni wasikivu watamuelewa China walijaribu kufanya hivi wakashindwa
Ukitaka kuendeleza mpira wekeza kwa vijana Kisha miundo mbinu Bora ya viwanja na makocha halafu media baada ya hapo ligi Yako itafanikiwa huu ni ukweli wa maendeleo
Saudi Arabia wana viwanja bora kabisa, academies nzuri na vilevile pesa. Hakuna mchezaji chizi atakubali aendelee kuutumikia mkataba wa £250k per week wakati mwarabu anakupa mara £600k-1M per week.

Hakuna mtu asiyependa pesa hapa duniani.
 
Waache ujinga wakati waarabu wanapeleka pesa ulaya kwa kununua man City na PSG hawakupiga kelele Leo ndio wameshituka wachezaji nyota wanaenda uarabuni, ni wivu unawasumbua.
Nyota Gani sasa? Kina Ronaldo,benzema hao ni wastaafu wanaenda chukua pensheni tu, au mediocre player kama kina neves, hata china walienda wastaafu tu, huwezi msikia mchezaji kama mbappe au haaland akihusishwa ni huu ujinga
 
Sjakuelewa..hizo long term na short unamaanisha solution za nini?
Maana WC host Qatar washaharibu mambo sodhan kama litarudi tena uarabuni ndani ya hii miaka 100 tuliyo hai
Waliharibu vip , kuwakataza watu wasinyanduane ? Kukataza pisi zisiende beach na vyupi ? Kupiga mkwara madanga ya Ulaya na America akina Beyonce ? Kuwalaza watu kwenye makontena 😁😁😁😁😁😁 waarabu walizinguaaaaaaaaaa.....Kobazi hawataona kombe tena
 
Nina uhakika hili lilikuwa ni swali kutoka kwa muandishi akijibu
Ameongea kitu Cha kweli sana tena na uwazi kama ni wasikivu watamuelewa China walijaribu kufanya hivi wakashindwa
Ukitaka kuendeleza mpira wekeza kwa vijana Kisha miundo mbinu Bora ya viwanja na makocha halafu media baada ya hapo ligi Yako itafanikiwa huu ni ukweli wa maendeleo
China serikali iliingilia kati wakaweka vikwazo club zisitoe pesa nyingi kusajili wachezaji, nadhani waliweka rungu la Kodi kubwa huu upumbavu ukaisha
 
Back
Top Bottom