Rais wa UEFA Ceferin atoa Onyo kinachoendea Saudi Arabia

Eeh mkuu nilikuwa sijui kumbe hadi Beyonce ni dangaπŸ˜…πŸ€£ aisee
 
M
China serikali iliingilia kati wakaweka vikwazo club zisitoe pesa nyingi kusajili wachezaji, nadhani waliweka rungu la Kodi kubwa huu upumbavu ukaisha
Mwarabu sio bahili kama mchina linapokuja suala la kumwaga pesa. Hizo teams za Saudi Arabia zinamilikiwa na makampuni makubwa sana yenye thamani ya ma trillion ya dollar. Haziwezi kuyumba kama zilivyoyumba teams za china
 
M

Mwarabu sio bahili kama mchina linapokuja suala la kumwaga pesa. Hizo teams za Saudi Arabia zinamilikiwa na makampuni makubwa sana yenye thamani ya ma trillion ya dollar. Haziwezi kuyumba kama zilivyoyumba teams za china
Kuna kitu Unashindwa kuelewa, sio kwamba club za china ziliishiwa pumzi, serikali iliona ni uwekezaji usio na tija, wakaja na mpango wa miaka 100 kuboresha mpira wao wakaachana na huu ujinga wa kununua ma star

Serikali kupitia chama Cha mpira wakaweka limit ya Kila club inayopaswa kutumia kwa mwaka, walifanya hivyo makusudi ili club zisiweze ku afford kuwaleta Hawa ma star wa ulaya na kuwalipa pesa kichaa

Kuna club iliyokua bingwa nimesahau jina walikiuka hii sheria wakashushwa daraja kwa miaka mitano ili iwe fundisho, Yani bingwa akashushwa daraja miaka mitano

Hapo ndo huu upumbavu ulipokoma
 
China mpira ulienda kama bahati mbaya wachina hawana passion na mpira tofauti na waarabu
 
wanachokifanya Saudi kilishafanyika zamani tu pale England, mpaka timu zinazogombea kushuka daraja zinalipa mishahara ya laki na nusu Paund kwa wiki wakati huo ni mshahara wa mchezaji wa timu kubwa kwenye nchi nyengine palepale ulaya.
Kwahiyo kwanini wakifanya wazungu ni sawa wakifanya waarabu iwe si sawa? Wivu unawasumbua sana mabeberu, always wao wanataka wao ndio wawe juu kwa kila kitu na kila mda. hawapendi kabisa kuwa na mshindani asiekuwa katika wao.
 

Saudi wanataka kuinua Ligi yao, hapo hakuna mahusiano na masuala ya timu ya taifa. na kama wanataka kuinua vipaji vya nchini kwao pia hawashindwi kuanzisha hizo academy, Hata England mara ya mweisho kubeba taji ni 1996 tena la mchongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…