SI KWELI Rais wa Urusi, Vladimir Putin alifanya kazi Nchini Tanzania

SI KWELI Rais wa Urusi, Vladimir Putin alifanya kazi Nchini Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
1658127191139.png
Picha ambayo baadhi ya watu wanadai kuwa inamuonyesha raisi wa Urusi Vladimir Putin akitoa mafunzo kwa wapigania uhuru kusini mwa Afrika ilisambaa na kutumiwa na baadhi ya watu kuhalalisha kuwa nchi za kiafrika zinapaswa kuunga mkono Urusi katika vita vya Ukraine.

Picha hiyo ilisambazwa sana mtandaoni baada ya kuchapiswa katika blogu za Zibwabwe mwishoni mwa mwaka 2018, machapisho hayo yalidai yanamuonyesha Putin katika mafunzo ya kijeshi ya Tanzania kwaajili ya harakati za kupigania uhuru katika nchi za Afrika mwaka 1973.
 
Tunachokijua
Hakuna ushahidi kutoka katika rekodi za Urusi na za Kiafrika zinazo onesha kuwa Putin aliwahi kufika nchini Tanzania kufundisha mafunzo kwa wapigania uhuru katika nchi za Afrika.

Putina mezaliwa mwaka wa 1952, na kusoma katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Leningrad na kuhitimu mwaka wa 1975, na kufanya kazi kama wakala wa KGB huko Ujerumani Mashariki kati ya mwaka 1985 na 1990.

Poul Fauvet, ambaye ni mwandishi wa habari aliyeishi nchini Msumbiji kwa miongo kadhaa anasema “Mafunzo yaliyotolewa kwa wapigania uhuru wa Msumbiji katika kambi nchini Tanzania yaliendeshwa na wakufunzi wa Kichina na sio Wasoviet.”

Georgi Derluguian, ambaye alifanya kazi kama mkalimani wa Kireno-Kirusi katika miaka ya 1980, ambaye sasa ni profesa katika chou kikuu cha New York Abu Dhabi, anasema kuwa “Madai kuwa mtu aliyeko kwenye picha ni Putin, ni madai ya kimzaha. Buti zilizovaliwa na mtu huyo katika picha ni za mwanajeshi, wakati Bwana Putin alikuwa ni afisa wa ujasusi.”

Isitoshe, Emmerson Mnangagwa anayetajwa pia kuwepo kwenye picha hiyo asingeweza kuwa nchini Tanzania mwaka wa 1973, kwa sababu alikamatwa mwaka 1965 na kufungwa jela kwa miaka kumi na serikali ya Rhodesia Kusini, ambayo wakati huo wengi wao walikuwa wazungu.

Madai haya yanathibitishwa kuwa yasiyo na ukweli wowote ndani yake, ingawa mtu aliyeko pichani anadhaniwa kuwa ni afisa wa Usovieti, bado hadi sasa hakuna mtu ambaye ameweza kuthibitisha utambulisho wake halisi.

Mwandishi wa Msumbiji Renato Matusse alitumia picha hiyo katika kitabu chake cha 2018, ambapo alisema inamuonyesha Bw. Machel akiwa na washauri wa kijeshi wa Usovieti wakitembelea kituo cha kijeshi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo, katikati ya miaka ya 1980.
Back
Top Bottom