Rais wa zamani wa ICC: Nina uhakika Putin atafika/kufikishwa mahakamani

Messenger RNA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
1,411
Reaction score
3,712
Rais wa zamani wa mahakama ya kimataifa ya ICC amesema anao uhakika kabisa kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Dr Chile Eboe-Osuji ameongeza kuwa katika miaka ambayo hati hizo za kukamatwa zimekuwa zikitolewa wote wamejikuta mwisho wa siku wanaletwa mahakamani kujibu mashtaka huku akitolea mfano maraisi wa zamani wa Rwanda,Serbia na Liberia.

"Hii haiwezi kuwa hadithi tofauti kwa Putin,kama sio sasa,baadae lazima afike kwa hukumu"ameongeza.

===================

Former international court chief 'confident' Putin will stand trial​

A former president of the International Criminal Court said he is confident Vladimir Putin will be brought to trial.
Dr Chile Eboe-Osuji said in every modern instance when an arrest warrant has been issued, somebody ended up in court.

He pointed to former leaders of Rwanda, Serbia and Liberia who had been served warrants.

"There is no basis for me to think that this will be a different story.

"Yes this will be the most important man to date that an arrest warrant has been served against, but lets see what happens."

He added: "I am confident that sooner or later this [a trial] will happen."

Source: Sky News
 
Rais wa zamani wa mahakama ya kimataifa ya ICC amesema anao uhakika kabisa kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Dr Chile Eboe-Osuji ameongeza kuwa katika miaka ambayo hati hizo za kukamatwa zimekuwa zikitolewa wote wamejikuta mwisho wa siku wanaletwa mahakamani kujibu mashtaka huku akitolea mfano maraisi wa zamani wa Rwanda,Serbia na Liberia.
"Hii haiwezi kuwa hadithi tofauti kwa Putin,kama sio sasa,baadae lazima afike kwa hukumu"ameongeza.
============================
Noma sana
USSR
 
Anajitekenya na kucheka...
Wanajeshi tu wa marekani waliwashindwa kuwafikisha baada ya kutishiwa kuwekewa vikwazo na wakapiga kimya na mafaili nadhani walishayachoma ije kuwa Putin...
Hii mahakama haina meno inaweza tu kudeal na viongozi wa Afrika huko kwingine inapiga kelele tu kwa sasa
 
Putin atue NY ku-address UNGA and other global and regional summits zinazomhusu aache kutuma foreign minister kama mbabe kweli!

Atadakwa kama kuku mwenye kideri vinginevyo aendelee kujichimbia chumbani kama mwali huku wababe wa dunia wakipasua anga end to end!
 
Sababu ile ile iliyofanya kuundwa kwa NATO ndiyo hiyo hiyo itakuwa kizuizi au njia ya kumkamata putin. Sababu yenyewe ni RUSSIA.

Huwezi sema unamshtaki mtu ambaye nchi inayomlinda kuingia nayo vita vya moja kwa moja haijawezekana. Nani atamkamata sasa? Unless nchi yake imtelekeze, kumkamata kutabaki kuwa kwenye makaratasi.
 
Muda utaongea.
 
Ni muda mrefu sana marais wa nchi kama Russia na China wameacha kabisa kuja NY kuhutubia UNGA.

Sisi Africans ndio tunaenda kwa sababu za Per Diem na kwenda kuomba omba misaada.
 
Putin atue NY ku-address UNGA and other global and regional summits zinazomhusu aache kutuma foreign minister kama mbabe kweli!

Atadakwa kama kuku mwenye kideri vinginevyo aendelee kujichimbia chumbani kama mwali huku wababe wa dunia wakipasua anga end to end!
Wameshamfungia ndani ya pipa hana uwezo wa kutembea kwa uhuru duniani tena, ataenda Iran, China, N. Korea, nk. Ameshafungwa miguu tayari.
 
Sababu ile ile iliyofanya kuundwa kwa NATO ndiyo hiyo hiyo itakuwa kizuizi au njia ya kumkamata putin. Sababu yenyewe ni RUSSIA.

Huwezi sema unamshtaki mtu ambaye nchi inayomlinda kuingia nayo vita vya moja kwa moja haijawezekana. Nani atamkamata sasa? Unless nchi yake imtelekeze, kumkamata kutabaki kuwa kwenye makaratasi.
USSR tayari wamechoshwa na putin wanaweza kumpeleka warudi wajenge nchi yao waondokane na udikteta
 
Back
Top Bottom