Rais wa Zanzibar aagiza Meli zote za Serikali ziuzwe kwa vile hazileti faida

Rais wa Zanzibar aagiza Meli zote za Serikali ziuzwe kwa vile hazileti faida

Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Meli za zanzibar bro zimezeeka mno na hawana fedha za kuzikarabati

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Ma-CCM ni failure kwenye kila kitu.

Watauza halafu wakinunua watarudi tena kulele maana hakuna mipango wala kujipanga bali wanasiasa ndio wanaamua kila kitu huku wataalamu wakibaki kuwa watekelezaji.

Na kwenye huu ununuzi, kunaweza pia kukawa na agenda ya upigaji.

Sina imani naa hawa watu.
Watauziana wenyewe meli moja laki tatu.
 
Hasara kwasababu inawezekana viongozi husafiri bure,

Bado ndugu zao,Wanaandikiwa vimemo.

Wakikagua kuanzia hapo.

Pili,Watendaji walioajiriwa hapo ni kweli walipatikana kwa njia halali au kwa njia ya vimemo?
 
Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Kwani Meli ni Ndege ?
 
Haina wataalamu wa mambo ya biashara na ujuaji ambao hauhusiani na biashara mwingi sana.
BAK huo uamuzi unaweza kuwa na manufaa iwapo tu waliosababisha hizo meli za zamani kufikia hatua hiyo hawatahusika tena kwenye kuendesha hizo mpya. Na zaidi njia za uendeshaji wa biashara wa meli za zamani usirudiwe tena, yaani waanze na watendaji wapya wenye kutumia njia tofauti na upimaji wa matokeo uwe wazi na ufanywe kila mwaka. Vinginevyo hata hizo mpya zitaishia kuwa kama hizo za zamani. Kwa kifupi tatizo liko kwa watendaji na njia za utendaji na siyo meli. Kingine: mara nyingi kumekuwa na visingizio kuwa eti serikali haiwezi kufanya biashara na ikifanya lazima ifeli. Hii ni dhana ya uongo kwa sababu kuna nchi ambazo serikali inafanya biashara na biashara hizo zinakuwa na maendeleo mazuri tu. Waende nchi za Scandinavia wakajifunze.
 
Wakati rais wa Zanzibar anauza Meli, Rais wa Tanzania yuko busy kusaini mikataba mipya ya kununua ndege
 
CCM watauza kila kitu ,mkumbuke tu hawa si watu wema,wamejivalisha ngosi ya kwondoo,kila siku wanaanza upya,hawa hawana mapenzi ya Mungu kuwepo madarakani kiongozi wao ni shetani kwani ,Mungu hawaongozi madhalimu hata mkiwaombea dua,anakwambia ukivambia uovu basi anakusukumiza na kukunogesha huko huko na ndio tuwaonavyo viongozi wa CCM hakuna jema hata moja kila wanalolifanya ili liwapendeze wananchi hudumu kwa muda tu na baadae hugeuka kuwa majuto. Dhulma hio.
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?
Hata kwa kanuni simpo ya Pythagoras haiingii kichwani. Ninanusa watu wanafanya biashara nyuma ya pazia na wanataka biashara zao zisitawi. Serikali inakosa meli hata moja? Na mnajiita serikali? Bora hako kazanzibar kawe moja ya mikoa ya TZ bara
🏃🏃🏃🏃🏃💨💨💨
 
Naunga mkono!
Unaposema uanze upya maana yake uunde authority upya bodi na menejimenti kwa ujumla kisha uingie mfukoni tena kununua meli halafu usubiri tena miaka kadhaa ya kuanza kutemgeneza faida hizo akili za pwagu au za mwenzake pwaguzi?
 
Hivi kwanini serikali huwa inafeli kwenye biashara nini tatizo haswa?
Biashara ya serikali sio yako binafsi ,Serikalini kumejaa incompetent people ambao hupewa Kazi kwa kujuana na sio uwezo unlike private sector.

Ili biashara za serikali zifaulu lazima ajira zizingatie uwezo na ziwe za mkataba yaani performance based ndio tija itapatikana .
 
Meli za Azam Fast Ferries, Flying Horse, Zanzibar One zinatusua pesa ila za SMZ hasara tupu??

Does it stick in mind?
Wazee wakupinga kila kitu!! Kwaiyo mnataka haziache zijiendeshe kwa hasara
 
Back
Top Bottom