Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Haya mambo yenu ya kijinga ndio yanadogosha muungano mkuu
Ujinga mzigo.
Fikiria idadi ya watu Tanzania bara 59 million.Zanzibar watu 1.5 ukimaliza tazama ukubwa wa eneo halafu angalia huo mgao wa Zanzibar kama ni haki.
Hizo hela za mkopo zitalipwa na Serekali ya Muungano ambayo kihalisia ni Tanzania bara.
Kati mambo ya hovyo ambayo Mwl Nyerere alituachia ni huu muungano ambao sijawahi kuona faida zake zaidi ya Zanzibar kubebwa bebwa.
Lipo suala la ajira kwa taasisi zote za muungano,Zanzibar wamepewa 21% huku Tanzania bara ikipewa 79%.Chukua idadi ya watu Zanzibar 1.5 million na bara 59 million.Utaona baada ya miaka 5 ukosefu wa ajira Zanzibar utamalizika ikiwa huu ujinga utaachwa uendelee.Baada ya miaka mitano taasisi kama TRA,BOT,JWTZ,JKT,POLISI,Uhamiaji,Wizaramambo ya ndani,ulinzi,Uchukuzi...... kila ukikuta wafanyakazi 100 wafanyakazi au watumishi 21 watakuwa waZanzibar.
Kama mpaka hapo huoni tatizo,hakikisha wakati unavuka barabara unasindikizwa na mtu mzima na timamu.