Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amshukuru Rais Samia Suluhu na IMF

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amshukuru Rais Samia Suluhu na IMF

===
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Hussein Ally Hassan Mwiny amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Samia Suluhu Hassan kwa Upambanaji wake kwa Taifa lake la Tanzania na kumtaka aendelee hivyohivyo kuumizwa na umasikini wa watu wake anaowaongoza toka pande zote za Muungano,
===
"Tumepata bahati ya kupata mkopo wa IMF dola za Marekani milioni 100 sawa na bilioni 230, nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha serikali ya Zanzibar inapata mgao wake katika mkopo ule wa trilioni 1.3 uliokopwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" -Rais Hussein Mwinyi


VIVA SAMIA VIVA ||VIVA MWINYI VIVA
Haya mambo ya mkopo na muungano ni shida,pesa imekopwa na serikali ya muungano,kiasi kimeperekwa Zenj ambayo ni sehemu ya muungano,wakati wa kulipa,inabidi serikali ikusanye mapato ndani ya muungano ilipe,lakini Hari haipo hivyo,TRA bara sio sehemu ya muungano Wala haikusanyi mapato zenj,kule Kuna ZRB,sasa wao watalipa kiasi gani na je kwenye mfuko wa muungano wao wanachangia asilimia ngapi?kwa vigezo gani?,uchache wa watu sio hoja,UK ina watu hawafiki milioni 40,lakini ni tajiri kuliko nchi ya Nigeria yenye watu milioni 200!!
 
Sawa kabisa. Jiwe alikopa matrilioni ya hela ila hakupeleka zanzibar hata mia.
apeleke za nn,wakati mkioewaga mgao hamlipi !!,hata suluhu amekosea kuwapa huo mgao,lipeni deni tunawadai pesa nyngi tu na hamjalipa hata Mia!!
 
Back
Top Bottom