Rais wa Zanzibar tafuta washauri wazuri suala la ardhi ya Bagamoyo

Katika suala hili (specifically) ipi ni mamlaka sahihi ya kutoa angalizo kuhusu umiliki wa ardhi husika?: Ni Waziri wa Ardhi wa JMT au Ikulu ya SMZ?

Hiyo ni ardhi ya JMT. SMZ ina hadhi ipi ndani ya serikali ya JMT? Mbia?

Nionavyo ni bora zaidi SMZ washughulikie hilo suala la “ardhi yao” kimya kimya kwenye michakato ya kisheria ndani ya serikali ya JMT badala ya kutoa vitisho kwa raia na wakazi wa Tanganyika ambo wako nje ya mamlaka yao. Hasa ikizingatiwa jinsi wanavyopenda kujitambulisha kama serikali ya nchi rasmi.

Hii nayo ni kero au “chokochoko” nyengine ya muungano ambayo ni pending bado. Kazi kwenu CCM.
 
Kasome katiba ya jmt
Mdhamini wa ardhi ni Rais wa jamuhuri, sasa hiyo ardhi ilo Zanzibar?
 
Unamzungumzia JPM yupi!? Ni yule bingwa wa kukiuka katiba na kupindisha sheria ama mwingine?
 
Mwinyi ndio amekurupuka. Haikuwekwa bendera ya Zanzibar hapo Bagamoyo. Nyerere hakuondoa hata kilometa moja ya eneo la Tanganyika na kuisalimisha kwa visiwa vya Zanzibar.
Najiuliza maswali magumu,

Endapo tukikaidi na kuendelea kulitumia eneo kama tunavyotaka Watanganyika Atatuma JESHI KUJA KULIKOMBOA?

Kama nchi tupo kwenye mtanziko mzito kipindi hiki
 
Kwa sheria zetu ukiwa na ardhi unapaswa kuiendeleza, usipoiendeleza serikali inapaswa kuichukua na kuipangia matumizi mengine.
 
Kwa sheria zetu ukiwa na ardhi unapaswa kuiendeleza, usipoiendeleza serikali inapaswa kuichukua na kuipangia matumizi mengine.
Na kinachokutambulisha kisheria kwamba unamiliki eneo ni hati ya ardhi, siyo maneno ya mdomoni.....maeneo ya serikali tu yana hati, iweje hao SMZ hawana hati ya umiliki wa hizo ekari elfu 6, na pia rais wa jamhuri anayo mamlaka ya kubatilisha hati ya umiliki wa ardhi, sasa hii jeuri sijui inatoka wapi.​
 
Rais Mwinyi anazingua.
 
Wazanzibari hawajui kuongea vizuri, wao ni mikwala tu (tabia za watu sio riziki) full urojooooo
 
Kama ilivyo balozi mbalimbali ndani ya nchi...
 
Mbona nyuma ya Daressalaam wameweka bendera teyari baada ya kudeka mwaka huu wakakubaliwa kuwa Visiwa vidogo mashariki mwa Dar ni sehemu ya zenji kisa tu kuna kumbukumbu ya Sultan kufika miaka 100 iliopita. Hivyo Dar haina bahari
Mwinyi ndio amekurupuka. Haikuwekwa bendera ya Zanzibar hapo Bagamoyo. Nyerere hakuondoa hata kilometa moja ya eneo la Tanganyika na kuisalimisha kwa visiwa vya Zanzibar
 
Hilo ni lako, mimi siyo muumini wa irrational, misguided and misplaced assertions kama hizi

..SMZ wamenyang'anywa hiyo ardhi kama alivyonyang'anywa Mzee Sumaye kule Morogoro.

..Rais ana mamlaka ya kufuta hati ya umiliki wa ardhi kwa mtu au taasisi yoyote.

..Tunachotakiwa kuangalia ni kama Raisi alifuata taratibu zote ktk kufuta umiliki wa ardhi kwa SMZ.

..Labda tungekwenda mbali zaidi na kuuliza SMZ walipewa ardhi hiyo kwa malengo au matumizi gani.

..Pia tujiulize kama SMZ waliitumia ardhi hiyo kwa kuzingatia masharti na malengo ya kupewa ardhi hiyo.

NB:

..huko nyuma kuliwahi kutokea kashfa ktk serikali ya Zanzibar iliyohusisha ardhi hiyo na ilijulikana kama " kashfa ya Makurunge ."
 
hakuna ardhi ya Tanzania iliwahi kugawiwa mazima, waliazimwa tu wawe wanafugia mifugo. unagawaje nchi? ni mjinga tu anaweza kuamini nchi inaweza kugawiwa. Magufuli kama aliwapa watu wengine ardhi hiyo, safi sana. iliyobaki wananchi vamieni mkalime mananasi na nyanyachungu.
 
Mbona nyuma ya Daressalaam wameweka bendera teyari baada ya kudeka mwaka huu wakakubaliwa kuwa Visiwa vidogo mashariki mwa Dar ni sehemu ya zenji kisa tu kuna kumbukumbu ya Sultan kufika miaka 100 iliopita. Hivyo Dar haina bahari

..wakahakiki kama Sultani hakuviuza visiwa hivyo kwa Wajerumani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…