Rais wa Zanzibar tafuta washauri wazuri suala la ardhi ya Bagamoyo

Rais wa Zanzibar tafuta washauri wazuri suala la ardhi ya Bagamoyo

Hili sakata la ardhi ya Bagamoyo ya hekari elfu sita kuwa ni mali ya Zanzibar lina ukakasi na halifai kupita bila ya kupata mawazo mbalimbali yenye lengo la kuboresha uelewa mpana wa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ni kweli Mwalimu Nyerere aliwapa Zanzibar ardhi ya Bagamoyo ili waweze kulima miaka hiyo ya sabini, hilo halina ubishi. Na pia ni kweli hayati Rais Magufuli akaja kuwapa wawekezaji wa Azam ardhi hiyo hiyo ili wafanye shughuli zao halali.

Kumuona Charles Hillary akipiga mkwara kwamba ardhi hiyo ni mali halali ya Zanzibar ndio kinapokuja kichekesho chenyewe.

Cession ni mchakato ambao sehemu ya ardhi ya nchi moja inatolewa rasmi na kuwa ni mali ya nchi nyingine, zipo sababu nyingi zenye kuyafikia maamuzi hayo.

Kwa kiswahili tunaita KUKOMA, yaani ardhi hiyo inakoma kuendelea kutumiwa na wakazi wa nchi husika inakuwa ni sehemu halali ya nchi nyingine na kiutaratibu inawekwa bandera ya nchi iliyoichukua kuanzia siku hiyo inapokoma kuwa ni mali ya nchi inapopatikana ardhi hiyo.

Je tangu miaka hiyo ya sabini kuna bendera yoyote inayopepea hapo Makurunge Bagamoyo kuonyesha kukoma kutumika kwa kipande hicho cha ardhi?, haijawahi kuwekwa bendera ya Zanzibar kuonyesha kuwa sehemu hiyo imekoma kuwa ni mali ya Tanzania, kiutaratibu bado ukubwa wa nchi ni ule ule unaotambulika kisheria tangu Tanzania ianze kuwa nchi kamili mwaka sitini na nne.

Hayati Rais Magufuli alikuwa na haki kabisa kumpatia muwekezaji Bakhresa sehemu ya ardhi iliyo chini yake kwa mujibu wa katiba. Kitendo cha Rais Mwinyi kuja na agizo la kufukuza waliopo katika ardhi hiyo wakati mchakato wa Cession haukuwahi kufanyika ni kosa la kiufundi la serikali anayoiongoza.

Naona kama wenye mamlaka ya kumshauri Rais Samia wameamua kutulia kwanza kutazama upepo wa huko juu utapita vipi. Wameliona hili kosa la kiufundi na nahisi ni suala litakalomalizwa kimya kimya tofauti na ule mkwara wa Charles Hillary alioutoa mbele ya media kule visiwani Unguja.

Mchakato wa Cession haukufanyika na hakuna bendera mahali pale yenye kuonyesha kuwa eneo limeshamilikishwa moja kwa moja kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Hayati Magufuli alikuwa na haki zote kuligawa eneo hilo na pengine sababu za Mwalimu Nyerere kuwapa serikali ya Mapinduzi miaka hiyo ya sabini hazikuwa na mashiko ya muda mrefu, zilikuwa ni temporary measures.

Rais wa awamu ya nane Zanzibar na washauri wake wamechemka katika suala hili, warudi nyuma na wajipange upya kabla ya kutoka hewani na matamko yenye kuzua maswali mengi yenye utata ndani yake.

THE LAND WAS NOT CEDED TO ZANZIBAR BUT GIVEN FOR USE BUT STILL UNDER TANGANYIKA.
Zanzibar walimilikishwa hiyo ardhi kama ambavo wewe umemilikishwa hilo shamba lako .yaani ardhi ni mali ya taasisi iitwayo SMZ Kama ilivo ardhi wanayomiliki kanisa katoliki hapa tanzania .ile ardhi ni sehemu ya nchi ya Tanzania bara kama zilivo ardhi za wananchi tu mmoja mmoja .ukiwa kwenye ile ardhi bagamoyo hauko zanzibar.ni.kama zanzibar leo ikanunue ardhi marekani inaruhusiwa kabisa na hadhi ya kumiliki ni kama hiyo ya bagamoyo ambayo duniani bagamoyo.yote ni sehemu ya nchi moja tu duniani inaitwa tanzania bara.
 
Ushahidi wa hiyo cession upo wapi?. Sidhani kama hayatI JPM angekuwa na mamlaka ya kumkabidhi sehemu ya eneo hilo Bakhresa iwapo angejua kuwa kuna mchakato halali wa kulikabidhi eneo hilo kwa serikali ya Mapinduzi.

Unapolimilikisha eneo kwa kuweka bendera ya nchi husika hata eneo zima la nchi linalojulikana kijiografia huwa linapungua, kitu ambacho hakijawahi kutokea. Hizo ekari elfu sita zingetosha kupunguza ukubwa wa eneo la kilomita za mraba za Tanzania.
Phillipo, nakuelewa sana kuhusu cession na nakuhakikishia ni topic isiyoeleweka kirahisi. Una hoja sana

Swali la Kujiuliza ni hili, ardhi waliyopewa ni ya Zanzibar? au wamekodishwa?
Jibu ni rahisi, Nyerere aliwapa ardhi watumie kwa Ranchi kama sehemu ya Tanzania. Ni kwa msingi huo Zanzibar wana hati miliki kama alivyo nayo mtu mwingine.

Mfano Tanzania imetoa ardhi kule Arusha kwa HQ ya EAC, EAC Law society na Court of Africa.
Hii haina maana ardhi imechukuliwa, la hasha, wamemilikishwa tu kama Zanzibar

C.Hillary hakueleza vizuri, alichosema eti ni ardhi ya Zanzibar ni ignorance tu.

Hata hivyo kitendo cha SMZ kutoa kauli juu ya ardhi ya Tanzania na Rais wa JMT ambaye ni 'trustee' kukaa kimya kinaeleza jambo. Swali la kujiuliza katika mazingira kama haya nani anaitetea Tanganyika?

JokaKuu Pascal Mayalla
 
.THE LAND WAS NOT CEDED TO ZANZIBAR BUT GIVEN FOR USE BUT STILL UNDER TANGNYIKA.
Naunga mkono hoja, ila Nyerere hakuligawa eneo hilo kuwa sehemu ya Zanzibar, Zanzibar walipewa offer tuu ya kulimiliki, kama wamiliki wengine wote, na eneo hilo bado ni sehemu ya Tanzania.

Zanzibar ilipaswa kulisurvey na kuomba hati miliki, hawakufanya!. Baada ya kashfa ya Makurunge, Zanzibar ililitekekeza eneo hilo kwa miaka 45 mpaka juzi!. Serikali ya Kikwete ililimega kuwapa wawekezaji, serikali ya JPM ikalimega kumpa Bakheresa, na Halmashauri ya Bagamoyo ikalimega kuwapa wananchi!.
Karibu mitaa hii Wabara ondoeni shaka, ardhi ya SMZ Bagamoyo si sehemu ya Zanzibar. SMZ haina hati; limetelekezwa miaka 45 ila SMZ inamiliki kihalali
P
 
Ardhi yote ya Jamhuri ya Muungano inamilikiwa na Rais. Hivyo JPM alikuwa na haki kumpa Bakhresa eneo la kuwekeza akiwa ndio mmiliki mkuu wa ardhi yote.

Iwapo angekuta ni eneo lenye bendera ya Zanzibar na Mwalimu Nyerere akiwa amelisalimisha kwa majirani zetu asingeweza kulitoa kumpa Bakhresa ili awekeze,

Rais Mwinyi analeta ujeuri usiokuwa na msingi, anapenda mno kuonyesha anazo nguvu za kushindana na mamlaka ya Jamhuri ya Muungano, huwa anakwaruzana na baadhi ya wakurugenzi wa mamlaka za kiserikali kwa kigezo hicho hicho cha urais wake.
Hujui unalolisema. Smz imemilikishwa na Ina uwezo wa kulirudisha mikononi mwake na kuwekeza.
 
Back
Top Bottom