Rais wangu kipenzi Samia kwaheri umeniumiza sana

Rais wangu kipenzi Samia kwaheri umeniumiza sana

Watu wamepewa green light naona 😄
Yule jamaa aliye trend majuzi kati hapa naona sahv anacheka tu 😄

Ova
 
Rais Samia amini kwa dhati nilikupenda na niliamini kweli umekuja kutufuta machozi baada ya miaka 6 ya hofu na mateso mengi. Ulianza vizuri kufanya upatanisho baada ya mtangulizi wako kuichafua historia nzuri ya taifa letu ukazidi kutufurahisha wapenzi wako baada ya kuja na 4R tukaendelea kukuombea kwa Mungu.

Ila sasa kwa mambo yaliyotokea hasa kuuwawa kwa mzee Ally na baadae kufwatia reaction yako jana kwa kweli umetuumbua wapenzi wako tuliona aibu kumkumbuka magufuli baada ya ile kauli yake mtanikumbuka sasa hakika tunamkumbuka kwani jambo baya akilifanya mwanamke linakuwa baya zaidi mama umefanya jambo baya hukupaswa kuzungumza kwa tone ile wewe ni mfariji mkuu sasa unatufokeaje msibani?

Basi kama tulivyomuachia Mungu wakati wa Magufuli basi tunamuachia Mungu na sasa. Kwaheri ya kuonana!
Kwenda zako uonane na nani wewe kibaraka!
 
Samia alianza vizuri na anaendelea vizuri, muwe waangalifu kuhusu hizo gharama mnazoingia katika kutaka kumchafua Rais ili aonekane kachafuka.
 
Mpaka sasa siamini kama zile kauli alizitoa mama, amepatwa na nini? Ni haya maandamano ndio yamemvuruga kiasi hiki?
Ni uthibitisho wa kuwepo kwa dalili za mwisho kabisa kabla ya 'Kuanguka kwa Mnara wa Babeli.'

Anguko lipo njiani linakuja.
 
3% ya speech ya Samia alitumia kulaani mauaji
97% ya speech alitumia kufokea walio react na utekaji na mauaji

Rais anapaswa kuwa MFARIJI wa taifa hata kama ni KINAFIKI lakini sio kwa vichambo na mipasho na vitisho vile asiee

Mbaya zaidi anawapongeza polisi kwa kazi nzuri ya kutukuka ndani ya ombwe la utekaji na mauaji ambapo hakuna kesi hata moja ilipatiwa majibu
 
Tayari keshatolewa kwenye reli. Halafu cheo chenyewe alikiokota kama embe dodo. Halafu approval rate yake imeshushwa sana na matukio ya utekaji.
 
Uraisi ni taasisi, hiyo taasisi ina mifumo yake ,,,,,

Kuna kipindi we Africans tulimlaumu sana Obama kumuuwa kanal Muammari Gadaffi !
 
Back
Top Bottom