..lugha yako ni mbaya, ya matusi, na dharau.
..hata hivyo HOJA zako ni NZITO na zinahitaji TAFAKURI.
..mfumo wetu umempa madaraka makubwa sana Raisi.
..pia tuna Raisi anayependa mno madaraka makubwa zaidi ya haya aliyopewa na katiba.
..kitu cha ajabu ni kuwa mtu huyu hataki kuwa mstari wa mbele wananchi wanapopatwa na maafa au misiba.
..pia sina uhakika kama wanaotaka mabadiliko ya katiba au mfumo wanatamani kumuondolea Raisi jukumu lake la kuwa Amiri Jeshi Mkuu, na mfariji mkuu[ comforter in chief ]wa nchi pake panapokuwa na majanga.