Rais wapunguzie kina Mbowe asali, wamepagawa

Msiturudishe kwenye viroba, sio tu walambe bali wanywe kabisa asali kama inanyweka ila isiwakabe

Upinzani sio uadui
Mimi vote yangu iko conservatives ila kwa huko bora iwe hivyo walambishwe tu
Siasa ya kubakana hatutaki tena
Waache ndugu wajitanue ila mpambane na ajira na viwanda tu

Ajali nazo mkaziangalie maana kila leo mnakufa kwa ajali za kizembe
 
Mheshimiwa Rais, Shikamoo.

Pole na hongera kwa majukumu mazito ya kujenga Taifa.

Nakuandikia andiko hili kukuomba kwa hishima na taadhima kubwa kwamba , Mheshimiwa. Tafadhali, Tafadhali sana. Sana sana. Wapunguzie akina Mbowe na genge lake asali. Inawalevya, Wanapagawa na wanafanya mambo mpaka hata sisi wafuasi wa siasa za upinzani tunawashangaa.

Mheshimiwa Rais,
Bila shaka umejionea wazi kuwa kumbe kosa la hayati Magufuli kwa hawa vinyonga ni kugoma kuwalambisha asali, laiti angeshauriwa mapema kabisa mwa utawala wake kuwa hawa ni waganga njaa tu, na kwamba ukiwapa buyu la asali na mirija isiyochomolewa, hawa hakuna cha ukamanda, wala utetea haki, wala upigania katiba mpya. Hawa ni njaa tu.

Nataka nikuthibitishie kuwa hawa ni njaa kwa nini.

Kama siyo njaa hebu niambie mheshimiwa rais, wako wapi makamanda wao wavaa kombati waliounga mkono juhudi?- Si walikaribishwa mezani kula na wakaja mzobemzobe wakakimbia wakaja CCM kula?.
Sasa kweli unadhani, hawa akina Mbowe na wenzie ni tofauti na wale?. Wote ni walewale tu isipokuwa JPM alistuka baadae sana kuwa hawa wote ni njaa tu. Ila angeanza nao kwa mwendo wa asali kama hii unayowalambisha taratiib wala usingesikia kelele za wao kumuita dikteta.

JPM angeanza nao hawa kwa kuwalambisha asali wasingehoji ishu zake kama ambavyo leo ishu zako za tozo, mfumuko wa bei, kufukuza wamasai loliondo, uhaba wa maji na vitu kama hivyo wasivyovishikia bango. Yaani ajenda hizo kisiasa zingekukalia vibaya mno mbele ya wananchi kama wangevishikia bango kisawasawa, ila wameamua kuviongelea kwa "forked tongue", au kuviongolea kijuujuu tu ili usije kukasirika ukawachomolea mirija ya asali.

Mheshimiwa Rais,
Jipige kifua, simama, jipongeze, hawa umeshawashika vizuri. Hakuna wapinzani hapa, kuna genge la masilahi binafsi. Yaani usipogusa biashara zao, wakubwa wao usipowanyang'anya viti vyao vya ubunge kama wakishinda hapa namaanisha wale wajumbe wa kamati kuu na baadhi wale wa baraza kuu lao, basi kelele za udikteta, au kutaka katiba mpya utazisikia kwa mbaali kama kelele za mbuzi aliyekwisha chinjwa na sasa anakata roho. Laiti JPM angeijua siri hii angewaacha baadhi yao wale vinara wakashinda ubunge, wala usingesikia kelele zile walizoanza nazo wakati ulipoapishwa kuwa rais. Ila nakupongeza, sasa umewasoma,umewaelewa. Hawa dawa yao asali tu, lakini isizidi sana, inawalevya!

Mheshimiwa Rais, kwa nini nakuomba uwapunguzie asali?

1. Mosi, ili kuwasitiri, Siku hizi katika mikutano yao wamegeuka chawa wako mpaka tunaogopa. Yaani kila wakiongea ni kukupongeza tu kuliko pitiliza, tinajiuliza huu urafiki wa ghafla wa chama tawala na hawa watu umekuja lini? - Wao wanajificha katika kivuli cha Maridhiano , tunajiuliza mmeridhiana nini?, kwa kweli hakipo maana kila wanachosema eti maridhiano yamepelekea kipatikane ni kwa mujibu wa katiba na wala si kwa hisani yako au upambanaji wao. Kwa mfano
a) Ishu ya mikutano ya hadhara, hiyo ni haki ya vyama ya kikatiba. Huhitaji maridhiano yoyote ili hilo liwepo.
Lakini pia nikukumbushe kuwa Ishu ya mikutano ya hadhara kuachiwa ilipendekezwa na kikosi kazi chako cha akina Profesa Mukandala kabla hata hivi vikao vya kuwalambisha asali hawa wanaosema eti ni maridhiano havijawa vingi.

b) Kufutwa kesi za kubambikiza. Kwanza kesi za kubambikiza hazipaswi kuwepo, maana hilo ni kinyume cha sheria. Huhitaji maridhiano ili hilo liwepo. Lakini pia nikukumbushe mheshimiwa Rais kuwa ni wewe uliagiza toka zamani tu kabla hata ya hivi vikao vya kuwapa asali hawa waganga njaa kuwa kesi za kubambikiza zifutwe, na Tukaona Kesi nyingi tu zikifutwa. Sasa hawa Walamba asali leo wanapokuja kudai kuwa eti kesi zao zimefutwa sababu ya maridhiano wanajaribu kujipa umuhimu ambao hawana.

Mheshimiwa Rais
Yaani nimecheka namna walamba asali walivyokukaribisha katika shughuli ya chama chao cha BAWACHA. Eti leo wanakuona wewe ni bora kuliko aliyekuwa mwenyekiti wa baraza lao Halima Mdee ambaye leo wanamuita eti ni mmoja wa kirusi cha Covid.
Mdee ambaye kwa mamlaka ya Urais unamlipa wewe mshahara, ambaye wewe kama mkuu wa nchi na serikali uliyeapa kulinda katiba kama ukiamua kunyoosha rula hapaswi kuwa bungeni lakini eti wewe wanakuona unafaa kuwa mgeni wa heshima ila yeye huyo unayemkingia kifua anaonekana traitor. Mheshimwa rais, hili siyo kosa lao, asali uliyowapa imewalevya, wamechanganyikiwa na sasa wako Irrational kabisa!

Mheshimiwa Rais nimalize barua yangu kwa kusema.

Kwa kweli move za kisiasa ulizofanya ktk mwaka huu wa fedha ni za kitaalamu sana.
Umeweza kuwasoma hawa walamba asali kuwa ni makamanda feki, Njaa kali. Ukiwaonyesha kipande cha mkate tu wanasahau hata majina yao. Ukiwapa asali ndo kabisaaa inawalevya.

Mheshimiwa tafadhali sana, wapunguzie hawa watu asali

Nawasilisha!

Naona CHADEMA wamewaingiza kwenye mtego. Mmebakia na kaneno kulamba asali Basi. CHADEMA itawapiga suprises mpaka mchanganyikiwe.
 
Chadema wanafanana na wale wanyama wa serengeti wanaohama hama kwenda Kenya na kurudi kwa msimu.

Sijui wanaitwaje wale nimesahau jina lao?

Ndio kilichobaki, ila nimependa CHADEMA wanavyofanya, yani kuwafanya muwajadili wao na kuwapa influence. Big up CHADEMA.
 
Naona CHADEMA wamewaingiza kwenye mtego. Mmebakia na kaneno kulamba asali Basi. CHADEMA itawapiga suprises mpaka mchanganyikiwe.
Samia keshawajulia.
Sasa hivi akina Mbowe hawewezi kumkosoa maana wako busy kuimba sifa zake
 
Tofautisha kati ya siasa za maridhiano na siasa za kishosti kati ya chama tawala na upinzani. Hakuna siasa za hivyo zenye tija

Juzi mlikiita chama Cha fujo, leo mnalia lia eti Rais asiwape asali. Mbona hamueleweki? CHADEMA endelea na suprises mpaka watu wasiojulikana wajulikane.
 
Mikutano ya kupiga kelele majukwaani imekusaidia nini mpaka sasa toka lema aanze kubweka?

Wewe Kama haikusaidii kaa kimya. Waache inao wasaidia waendelee nayo. Mkoloni mwenyewe aliwaruhusu TANU wafanye mikutano nchi nzima, ila wewe ngozi nyeusi unaona shida wenzako kufanya mikutano.
 
Magufuli aliwapiga pini au uoga? Aliogopa kutokana na uchaguzi wanot2015, kwamba Upinzani ungepata influence kubwa.

Mwanaume mzima unazidiwa na mwanamke aliyeamua kuwaruhusu wapinzani wafanye siasa. Magufuli was a coward.
 
Inawezekana Jiwe alipopewa mafaili yao akaona hawa ni waganga njaa tu. Mwanzo akaamua kudeal nao kibandidu ila baadae akaona awape mkate baadhi yao waliounga mkono juhudi. Kama angeanza kula na hawa makamanda wakubwa huenda zile kelele zote walizokuwa wanampigia zosingekuwepo

Hakuna Cha faili Wala Nini. Yule Magufuli kwanza kaingia ikulu kibahati kwa asilimia 58, yani asilimia chache kuliko mgombea yeyote wa CCM aliyewahi kushinda urais. Sasa kwa uoga akaona awazuie Upinzani kufanya siasa, ila mwisho kafa kawaacha Upinzani wanaendelea na mambo yao.
 
Kwa hoja hizi dhaifu tulizo zisikia siku mbili hizi tokea hio mkutano yao ya hadhara kulikua na umuhimu wa kuifungia hio mikutano.

Siasa ni utapeli uliohalalshwa na wanasiasa ni matapeli ambao wanaubinafsi ulio pitiliza

Pole Sana. Utapeli ulikuwa awamu ya tano. Unanua watu halafu wanahamia chama tawala na kupewa ubunge na unaibu waziri.
 
Poleni sana, Samia anawaanika viongozi wenu waganga njaa.

Mnaumia lakini Mtafanyaje sasa Mbowe na genge lake wako busy na asali yao na wala hawana mpango na nyinyi na hamna cha kuwafanya!

Tatizo lako njaa zako unadhani kila mtu yupo Kama wewe. Mbowe awe na njaa kwa lipi?. Kubalini, CHADEMA imewapiga chenga ya mwili mmebaki na masononeko. Hamuamini kwamba leo Hakuna watu wasiojulikana.
 
Poleni sana, Samia anawaanika viongozi wenu waganga njaa.

Mnaumia lakini Mtafanyaje sasa Mbowe na genge lake wako busy na asali yao na wala hawana mpango na nyinyi na hamna cha kuwafanya!
Ni kweli waendelee kulamba asali. So long Akina Ben Saanane na Risasi za akina Lisu hazitatokea tena. Supu ya Damu mmemiss sana nyie Wapumbavu.
 
Mnaongea sana alafu mnajisahau haya twambie sasa hivi mpo kwenye chama chenu chini ya MBOWE au mpo kwenye Chama cha ccm chini ya SAMIA?

Hayo ni mawazo yako. Mwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe na Mama Samiah ni Rais wa nchi. CHADEMA baada ya maridhiano na serikali imeamua kumtambua. Shida ipo wapi?. Siasa za kulimana risasi na viroba ziliishia na mwendazake.
 
Weee dogo wewe, umesema aliyezuiq mikutano alikuwa yuko right.
Nikakuuliza uoni kuwa unaona hapo ni kuvunja katiba and you are supporting that??

Hayo ni mawazo yako. Mwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe na Mama Samiah ni Rais wa nchi. CHADEMA baada ya maridhiano na serikali imeamua kumtambua. Shida ipo wapi?. Siasa za kulimana risasi na viroba ziliishia na mwendazake.
Jengeni chama hacheni uzumbukuku,Mmeishiwa hoja mnaishia kumzungumzia tu Huyo mtu.
 
Mheshimiwa Rais, Shikamoo.

Pole na hongera kwa majukumu mazito ya kujenga Taifa.

Nakuandikia andiko hili kukuomba kwa heshima na taadhima kubwa kwamba , Mheshimiwa. Tafadhali, Tafadhali sana. Sana sana. Wapunguzie akina Mbowe na genge lake asali. Inawalevya, Wanapagawa na wanafanya mambo mpaka hata sisi wafuasi wa siasa za upinzani tunawashangaa.

Mheshimiwa Rais,
Bila shaka umejionea wazi kuwa kumbe kosa la hayati Magufuli kwa hawa vinyonga ni kugoma kuwalambisha asali, laiti angeshauriwa mapema kabisa mwa utawala wake kuwa hawa ni waganga njaa tu, na kwamba ukiwapa buyu la asali na mirija isiyochomolewa, hawa hakuna cha ukamanda, wala utetea haki, wala upigania katiba mpya. Hawa ni njaa tu.

Nataka nikuthibitishie kuwa hawa ni njaa kwa nini.

Kama siyo njaa hebu niambie mheshimiwa rais, wako wapi makamanda wao wavaa kombati waliounga mkono juhudi?- Si walikaribishwa mezani kula na wakaja mzobemzobe wakakimbia wakaja CCM kula?.
Sasa kweli unadhani, hawa akina Mbowe na wenzie ni tofauti na wale?. Wote ni walewale tu isipokuwa JPM alistuka baadae sana kuwa hawa wote ni njaa tu. Ila angeanza nao kwa mwendo wa asali kama hii unayowalambisha taratiib wala usingesikia kelele za wao kumuita dikteta.

JPM angeanza nao hawa kwa kuwalambisha asali wasingehoji ishu zake kama ambavyo leo ishu zako za tozo, mfumuko wa bei, kufukuza wamasai loliondo, uhaba wa maji na vitu kama hivyo wasivyovishikia bango. Yaani ajenda hizo kisiasa zingekukalia vibaya mno mbele ya wananchi kama wangevishikia bango kisawasawa, ila wameamua kuviongelea kwa "forked tongue", au kuviongolea kijuujuu tu ili usije kukasirika ukawachomolea mirija ya asali.

Mheshimiwa Rais,
Jipige kifua, simama, jipongeze, hawa umeshawashika vizuri. Hakuna wapinzani hapa, kuna genge la masilahi binafsi. Yaani usipogusa biashara zao, wakubwa wao usipowanyang'anya viti vyao vya ubunge kama wakishinda hapa namaanisha wale wajumbe wa kamati kuu na baadhi wale wa baraza kuu lao, basi kelele za udikteta, au kutaka katiba mpya utazisikia kwa mbaali kama kelele za mbuzi aliyekwisha chinjwa na sasa anakata roho. Laiti JPM angeijua siri hii angewaacha baadhi yao wale vinara wakashinda ubunge, wala usingesikia kelele zile walizoanza nazo wakati ulipoapishwa kuwa rais. Ila nakupongeza, sasa umewasoma,umewaelewa. Hawa dawa yao asali tu, lakini isizidi sana, inawalevya!

Mheshimiwa Rais, kwa nini nakuomba uwapunguzie asali?

1. Mosi, ili kuwasitiri, Siku hizi katika mikutano yao wamegeuka chawa wako mpaka tunaogopa. Yaani kila wakiongea ni kukupongeza tu kuliko pitiliza, tinajiuliza huu urafiki wa ghafla wa chama tawala na hawa watu umekuja lini? - Wao wanajificha katika kivuli cha Maridhiano , tunajiuliza mmeridhiana nini?, kwa kweli hakipo maana kila wanachosema eti maridhiano yamepelekea kipatikane ni kwa mujibu wa katiba na wala si kwa hisani yako au upambanaji wao. Kwa mfano
a) Ishu ya mikutano ya hadhara, hiyo ni haki ya vyama ya kikatiba. Huhitaji maridhiano yoyote ili hilo liwepo.
Lakini pia nikukumbushe kuwa Ishu ya mikutano ya hadhara kuachiwa ilipendekezwa na kikosi kazi chako cha akina Profesa Mukandala kabla hata hivi vikao vya kuwalambisha asali hawa wanaosema eti ni maridhiano havijawa vingi.

b) Kufutwa kesi za kubambikiza. Kwanza kesi za kubambikiza hazipaswi kuwepo, maana hilo ni kinyume cha sheria. Huhitaji maridhiano ili hilo liwepo. Lakini pia nikukumbushe mheshimiwa Rais kuwa ni wewe uliagiza toka zamani tu kabla hata ya hivi vikao vya kuwapa asali hawa waganga njaa kuwa kesi za kubambikiza zifutwe, na Tukaona Kesi nyingi tu zikifutwa. Sasa hawa Walamba asali leo wanapokuja kudai kuwa eti kesi zao zimefutwa sababu ya maridhiano wanajaribu kujipa umuhimu ambao hawana.

Mheshimiwa Rais
Yaani nimecheka namna walamba asali walivyokukaribisha katika shughuli ya chama chao ya BAWACHA. Eti leo wanakuona wewe ni bora kuliko aliyekuwa mwenyekiti wa baraza lao Halima Mdee ambaye leo wanamuita eti ni mmoja wa kirusi cha Covid.
Mdee ambaye kwa mamlaka ya Urais unamlipa wewe mshahara, ambaye wewe kama mkuu wa nchi na serikali uliyeapa kulinda katiba kama ukiamua kunyoosha rula hapaswi kuwa bungeni lakini eti wewe wanakuona unafaa kuwa mgeni wa heshima ila yeye huyo unayemkingia kifua anaonekana traitor. Mheshimwa rais, hili siyo kosa lao, asali uliyowapa imewalevya, wamechanganyikiwa na sasa wako Irrational kabisa!

Mheshimiwa Rais nimalize barua yangu kwa kusema.

Kwa kweli move za kisiasa ulizofanya ktk mwaka huu wa fedha ni za kitaalamu sana.
Umeweza kuwasoma hawa walamba asali kuwa ni makamanda feki, Njaa kali. Ukiwaonyesha kipande cha mkate tu wanasahau hata majina yao. Ukiwapa asali ndo kabisaaa inawalevya.

Mheshimiwa tafadhali sana, wapunguzie hawa watu asali watawehuka.

Nawasilisha!

IMG_8396.jpg

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom