Rais wapunguzie kina Mbowe asali, wamepagawa

ACT walipokuwa wakitamka neno "Maridhiano", Chadema walikuwa wakiwaponda.

Chadema leo nao wameazima neno "Maridhiano" kujustify udalali wao wa kisiasa, halafu wanadhani WaTZ watawapa blank checque
Chadema walikua wanawatukana TLP, CUF, NCCR. Kumbe nao walikua wanataman hiyo nafasi
 
Rubbish, unashindwa kusema tu kilichoujaza moyo wako kwamba mmemisi kunywa damu za watu na kusambaza chuki na ubaguzi.

Hakika Sasa ndio tofauti inaonekana wazi Tanzania ilikuwa inatawaliwa na Lucifer himself.
Nakuona mvaa kobaz uko katika zamu ya kumtetea mvaa kobaz mwenzio
 
Too low.....

Umeandika ushabiki tu.

Huu ndio msimamo wenu Act ?
Hao ni wanafiki, waliotaka maridhiano yaguse pengine pote, isipokuwa kwenye ruzuku tu!.

Chadema kupokea ruzuku kumewauma sana.
 
Poleni sana, Samia anawaanika viongozi wenu waganga njaa.

Mnaumia lakini Mtafanyaje sasa Mbowe na genge lake wako busy na asali yao na wala hawana mpango na nyinyi na hamna cha kuwafanya!
Haka kazee kamejaa mihemko sana🥱🥱
 
Mbona ACT-Wazalendo walipoingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar mulikiwa mnawaponda sana.Sasa tulieni na nyie mle nondo za vichwa.

CCM ameoa ACT ila Bi.Mdogo CHADEMA alikuwa ana malingo sasa hivi amekubali show!
Chadema hawakutia neno kuhusu ACT kuingia SUK kwani wao siyo wa kwanza kuingia kwenye SUK ulianza CUF.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mheshimiwa Rais, Shikamoo.

Pole na hongera kwa majukumu mazito ya kujenga Taifa.

Nakuandikia andiko hili kukuomba kwa heshima na taadhima kubwa kwamba , Mheshimiwa. Tafadhali, Tafadhali sana. Sana sana. Wapunguzie akina Mbowe na genge lake asali. Inawalevya, Wanapagawa na wanafanya mambo mpaka hata sisi wafuasi wa siasa za upinzani tunawashangaa.

Mheshimiwa Rais,
Bila shaka umejionea wazi kuwa kumbe kosa la hayati Magufuli kwa hawa vinyonga ni kugoma kuwalambisha asali, laiti angeshauriwa mapema kabisa mwa utawala wake kuwa hawa ni waganga njaa tu, na kwamba ukiwapa buyu la asali na mirija isiyochomolewa, hawa hakuna cha ukamanda, wala utetea haki, wala upigania katiba mpya. Hawa ni njaa tu.

Nataka nikuthibitishie kuwa hawa ni njaa kwa nini.

Kama siyo njaa hebu niambie mheshimiwa rais, wako wapi makamanda wao wavaa kombati waliounga mkono juhudi?- Si walikaribishwa mezani kula na wakaja mzobemzobe wakakimbia wakaja CCM kula?.
Sasa kweli unadhani, hawa akina Mbowe na wenzie ni tofauti na wale?. Wote ni walewale tu isipokuwa JPM alistuka baadae sana kuwa hawa wote ni njaa tu. Ila angeanza nao kwa mwendo wa asali kama hii unayowalambisha taratiib wala usingesikia kelele za wao kumuita dikteta.

JPM angeanza nao hawa kwa kuwalambisha asali wasingehoji ishu zake kama ambavyo leo ishu zako za tozo, mfumuko wa bei, kufukuza wamasai loliondo, uhaba wa maji na vitu kama hivyo wasivyovishikia bango. Yaani ajenda hizo kisiasa zingekukalia vibaya mno mbele ya wananchi kama wangevishikia bango kisawasawa, ila wameamua kuviongelea kwa "forked tongue", au kuviongolea kijuujuu tu ili usije kukasirika ukawachomolea mirija ya asali.

Mheshimiwa Rais,
Jipige kifua, simama, jipongeze, hawa umeshawashika vizuri. Hakuna wapinzani hapa, kuna genge la masilahi binafsi. Yaani usipogusa biashara zao, wakubwa wao usipowanyang'anya viti vyao vya ubunge kama wakishinda hapa namaanisha wale wajumbe wa kamati kuu na baadhi wale wa baraza kuu lao, basi kelele za udikteta, au kutaka katiba mpya utazisikia kwa mbaali kama kelele za mbuzi aliyekwisha chinjwa na sasa anakata roho. Laiti JPM angeijua siri hii angewaacha baadhi yao wale vinara wakashinda ubunge, wala usingesikia kelele zile walizoanza nazo wakati ulipoapishwa kuwa rais. Ila nakupongeza, sasa umewasoma,umewaelewa. Hawa dawa yao asali tu, lakini isizidi sana, inawalevya!

Mheshimiwa Rais, kwa nini nakuomba uwapunguzie asali?

1. Mosi, ili kuwasitiri, Siku hizi katika mikutano yao wamegeuka chawa wako mpaka tunaogopa. Yaani kila wakiongea ni kukupongeza tu kuliko pitiliza, tinajiuliza huu urafiki wa ghafla wa chama tawala na hawa watu umekuja lini? - Wao wanajificha katika kivuli cha Maridhiano , tunajiuliza mmeridhiana nini?, kwa kweli hakipo maana kila wanachosema eti maridhiano yamepelekea kipatikane ni kwa mujibu wa katiba na wala si kwa hisani yako au upambanaji wao. Kwa mfano
a) Ishu ya mikutano ya hadhara, hiyo ni haki ya vyama ya kikatiba. Huhitaji maridhiano yoyote ili hilo liwepo.
Lakini pia nikukumbushe kuwa Ishu ya mikutano ya hadhara kuachiwa ilipendekezwa na kikosi kazi chako cha akina Profesa Mukandala kabla hata hivi vikao vya kuwalambisha asali hawa wanaosema eti ni maridhiano havijawa vingi.

b) Kufutwa kesi za kubambikiza. Kwanza kesi za kubambikiza hazipaswi kuwepo, maana hilo ni kinyume cha sheria. Huhitaji maridhiano ili hilo liwepo. Lakini pia nikukumbushe mheshimiwa Rais kuwa ni wewe uliagiza toka zamani tu kabla hata ya hivi vikao vya kuwapa asali hawa waganga njaa kuwa kesi za kubambikiza zifutwe, na Tukaona Kesi nyingi tu zikifutwa. Sasa hawa Walamba asali leo wanapokuja kudai kuwa eti kesi zao zimefutwa sababu ya maridhiano wanajaribu kujipa umuhimu ambao hawana.

Mheshimiwa Rais
Yaani nimecheka namna walamba asali walivyokukaribisha katika shughuli ya chama chao ya BAWACHA. Eti leo wanakuona wewe ni bora kuliko aliyekuwa mwenyekiti wa baraza lao Halima Mdee ambaye leo wanamuita eti ni mmoja wa kirusi cha Covid.
Mdee ambaye kwa mamlaka ya Urais unamlipa wewe mshahara, ambaye wewe kama mkuu wa nchi na serikali uliyeapa kulinda katiba kama ukiamua kunyoosha rula hapaswi kuwa bungeni lakini eti wewe wanakuona unafaa kuwa mgeni wa heshima ila yeye huyo unayemkingia kifua anaonekana traitor. Mheshimwa rais, hili siyo kosa lao, asali uliyowapa imewalevya, wamechanganyikiwa na sasa wako Irrational kabisa!

Mheshimiwa Rais nimalize barua yangu kwa kusema.

Kwa kweli move za kisiasa ulizofanya ktk mwaka huu wa fedha ni za kitaalamu sana.
Umeweza kuwasoma hawa walamba asali kuwa ni makamanda feki, Njaa kali. Ukiwaonyesha kipande cha mkate tu wanasahau hata majina yao. Ukiwapa asali ndo kabisaaa inawalevya.

Mheshimiwa tafadhali sana, wapunguzie hawa watu asali watawehuka.

Nawasilisha!
mamayenu amelambishwa asali na kesho kule moshi anakabidhiwa kadi ua chadema huku mapoyoyo ya ccm yakibwekabweka hayajui yashike wapi.
 
Ila mkilamba nyie na kile chama chenu cha kigoma ni sawa sio?
 
Poleni sana, Samia anawaanika viongozi wenu waganga njaa.

Mnaumia lakini Mtafanyaje sasa Mbowe na genge lake wako busy na asali yao na wala hawana mpango na nyinyi na hamna cha kuwafanya!
samia ameyatelekeza mapoyoyo ua ccm naada ya kuyagundua kuwa kumbe alikua anaongoza mapoyoyo kaamua kuyaacha solemba.
 
Nataka nikuthibitishie kuwa hawa ni njaa kwa nini.

Kama siyo njaa hebu niambie mheshimiwa rais, wako wapi makamanda
 
Hujui hata kuandika bro. Juu umesema kwamba nataka kuwathibitishia kuwa ni njaa halafu ukakacha kithibitisha ukarukia prngine
 
Tofautisha kati ya siasa za maridhiano na siasa za kishosti kati ya chama tawala na upinzani. Hakuna siasa za hivyo zenye tija
We umezoea siasa za kutukana au vipi? Shida yenu mlizoeahwa na jpm kwamba ili uitwe mpinzani lazima.upigwe lisasi na lazima upambane na utawala bila sababu ya msingi
 
Kila kipeperushi mnachokiona huko barabarani mnakiokota, kukisoma, na kukiamini, hamna tofauti na wendawazimu[emoji1787][emoji1787]
Tutakuwa tunakuletea hivi vipeperushi vya kiwendawazimu ili uvihakiki kwanza kabla havijasambaa mitandaoni humu. Na kwa vile sasa kuna ruzuku (inayotokana na Covid 19 na uchafuzi wa 2020) bila shaka utakuwa unalipwa [emoji16][emoji16][emoji16]
 
We umezoea siasa za kutukana au vipi? Shida yenu mlizoeahwa na jpm kwamba ili uitwe mpinzani lazima.upigwe lisasi na lazima upambane na utawala bila sababu ya msingi

Sasa yafaa nini kutokuwa chawa wa Magufuli ila kuwa chawa wa Samia?. Kimsingi haifai kuwa chawa wa mtu yeyote!.
Uchawa kwa Samia usidhani ndo utaifanya CCM isiibe chaguzi zijazo!
 
Back
Top Bottom