Rais wapunguzie kina Mbowe asali, wamepagawa

Rais wapunguzie kina Mbowe asali, wamepagawa

Jengeni chama hacheni uzumbukuku,Mmeishiwa hoja mnaishia kumzungumzia tu Huyo mtu.

Tumeishiwa hoja gani? Chama kilishajengwa ndio maana leo kinaongelewa nchi nzima na kufatiliwa na watanzania wengi.

Ila Shetani lazima akemewe hata Kama haonekani. CHADEMA kwa raha zetu tunapasua anga wafuasi wa ibilisi wamenuna, walifurahia Lissu kulimwa risasi na mauaji ya saa nane. Ila CHADEMA kuwa huru kufanya siasa imekuwa nongwa.
 
Si kwamba Magufuli alikuwa mbaya, ubaya wake uliletwa na propaganda kutoka kwa wachumia tumbo wa kisiasa ambao mianya yao ya upigaji ilibanwa ghafla tofauti na walivyozoea huko nyuma, maisha yao yakawa magumu bila zile favour walizozoea, na hawakuwa na namna zaidi ya kuwa wapiga kelele.

Kwasasa huwezi kuwasikia wakipiga kelele kwakua wanakula na utawala, hata ufisadi utoker vipi, hela ziliwe hovyo hautasikia wakipayuka kwasababu hiyo haijawahi kuwa kazi yao mpaka pale wanaponyimwa masilahi.

Tunamshukuru Mungu kwa Sasa watu wasiojulikana hawapo na kulima watu risasi kumeisha. Kiongozi yeyote ambaye aheshimu uhai wa raia hata mmoja hafai kuishi kwenye uso wa Dunia. Huwezi kumwaga damu ya Rais wako ukategemea kuishi, ndio maana wengine wamekufa kwa aibu huku wamefichwa.
 
Tumeishiwa hoja gani? Chama kilishajengwa ndio maana leo kinaongelewa nchi nzima na kufatiliwa na watanzania wengi.

Ila Shetani lazima akemewe hata Kama haonekani. CHADEMA kwa raha zetu tunapasua anga wafuasi wa ibilisi wamenuna, walifurahia Lissu kulimwa risasi na mauaji ya saa nane. Ila CHADEMA kuwa huru kufanya siasa imekuwa nongwa.
ni CDM au ilikuwa ni kwa vyama vyote?tuweke sawa hapa tusipotoshane.
 
Hayo ni mawazo yako. Mwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe na Mama Samiah ni Rais wa nchi. CHADEMA baada ya maridhiano na serikali imeamua kumtambua. Shida ipo wapi?. Siasa za kulimana risasi na viroba ziliishia na mwendazake.
maridhiano gani wewe unayoyazungumzia?

Wanaoridhiana ni pande mbili zilizokoseana, Sasa Chadema walimkosea nini Samia hadi waridhiane naye?
 
Tumeishiwa hoja gani? Chama kilishajengwa ndio maana leo kinaongelewa nchi nzima na kufatiliwa na watanzania wengi.

Ila Shetani lazima akemewe hata Kama haonekani. CHADEMA kwa raha zetu tunapasua anga wafuasi wa ibilisi wamenuna, walifurahia Lissu kulimwa risasi na mauaji ya saa nane. Ila CHADEMA kuwa huru kufanya siasa imekuwa nongwa.
Mnavyosemaga saa nane aliuwawa mlishaonaga mwili wake,lissu kumiminiwa lisasi hajawai semwa ni akinani na yeye kaishi huko kwa basha wake yuko free kusema hajawai wataja mpka sasa mana alisema anawafahamu.
Chama kinazungumziwa sio kwa mazuri bari kwa ujinga wenu.
 
ni CDM au ilikuwa ni kwa vyama vyote?tuweke sawa hapa tusipotoshane.

Ni CDM tu, Kuna chama kilipitia changamoto Kama CHADEMA?. Tuache unafiki Hadi wananchi waliogopa kuhusishwa na CHADEMA.
 
Mheshimiwa Rais, Shikamoo.

Pole na hongera kwa majukumu mazito ya kujenga Taifa.

Nakuandikia andiko hili kukuomba kwa heshima na taadhima kubwa kwamba , Mheshimiwa. Tafadhali, Tafadhali sana. Sana sana. Wapunguzie akina Mbowe na genge lake asali. Inawalevya, Wanapagawa na wanafanya mambo mpaka hata sisi wafuasi wa siasa za upinzani tunawashangaa.

Mheshimiwa Rais,
Bila shaka umejionea wazi kuwa kumbe kosa la hayati Magufuli kwa hawa vinyonga ni kugoma kuwalambisha asali, laiti angeshauriwa mapema kabisa mwa utawala wake kuwa hawa ni waganga njaa tu, na kwamba ukiwapa buyu la asali na mirija isiyochomolewa, hawa hakuna cha ukamanda, wala utetea haki, wala upigania katiba mpya. Hawa ni njaa tu.

Nataka nikuthibitishie kuwa hawa ni njaa kwa nini.

Kama siyo njaa hebu niambie mheshimiwa rais, wako wapi makamanda wao wavaa kombati waliounga mkono juhudi?- Si walikaribishwa mezani kula na wakaja mzobemzobe wakakimbia wakaja CCM kula?.
Sasa kweli unadhani, hawa akina Mbowe na wenzie ni tofauti na wale?. Wote ni walewale tu isipokuwa JPM alistuka baadae sana kuwa hawa wote ni njaa tu. Ila angeanza nao kwa mwendo wa asali kama hii unayowalambisha taratiib wala usingesikia kelele za wao kumuita dikteta.

JPM angeanza nao hawa kwa kuwalambisha asali wasingehoji ishu zake kama ambavyo leo ishu zako za tozo, mfumuko wa bei, kufukuza wamasai loliondo, uhaba wa maji na vitu kama hivyo wasivyovishikia bango. Yaani ajenda hizo kisiasa zingekukalia vibaya mno mbele ya wananchi kama wangevishikia bango kisawasawa, ila wameamua kuviongelea kwa "forked tongue", au kuviongolea kijuujuu tu ili usije kukasirika ukawachomolea mirija ya asali.

Mheshimiwa Rais,
Jipige kifua, simama, jipongeze, hawa umeshawashika vizuri. Hakuna wapinzani hapa, kuna genge la masilahi binafsi. Yaani usipogusa biashara zao, wakubwa wao usipowanyang'anya viti vyao vya ubunge kama wakishinda hapa namaanisha wale wajumbe wa kamati kuu na baadhi wale wa baraza kuu lao, basi kelele za udikteta, au kutaka katiba mpya utazisikia kwa mbaali kama kelele za mbuzi aliyekwisha chinjwa na sasa anakata roho. Laiti JPM angeijua siri hii angewaacha baadhi yao wale vinara wakashinda ubunge, wala usingesikia kelele zile walizoanza nazo wakati ulipoapishwa kuwa rais. Ila nakupongeza, sasa umewasoma,umewaelewa. Hawa dawa yao asali tu, lakini isizidi sana, inawalevya!

Mheshimiwa Rais, kwa nini nakuomba uwapunguzie asali?

1. Mosi, ili kuwasitiri, Siku hizi katika mikutano yao wamegeuka chawa wako mpaka tunaogopa. Yaani kila wakiongea ni kukupongeza tu kuliko pitiliza, tinajiuliza huu urafiki wa ghafla wa chama tawala na hawa watu umekuja lini? - Wao wanajificha katika kivuli cha Maridhiano , tunajiuliza mmeridhiana nini?, kwa kweli hakipo maana kila wanachosema eti maridhiano yamepelekea kipatikane ni kwa mujibu wa katiba na wala si kwa hisani yako au upambanaji wao. Kwa mfano
a) Ishu ya mikutano ya hadhara, hiyo ni haki ya vyama ya kikatiba. Huhitaji maridhiano yoyote ili hilo liwepo.
Lakini pia nikukumbushe kuwa Ishu ya mikutano ya hadhara kuachiwa ilipendekezwa na kikosi kazi chako cha akina Profesa Mukandala kabla hata hivi vikao vya kuwalambisha asali hawa wanaosema eti ni maridhiano havijawa vingi.

b) Kufutwa kesi za kubambikiza. Kwanza kesi za kubambikiza hazipaswi kuwepo, maana hilo ni kinyume cha sheria. Huhitaji maridhiano ili hilo liwepo. Lakini pia nikukumbushe mheshimiwa Rais kuwa ni wewe uliagiza toka zamani tu kabla hata ya hivi vikao vya kuwapa asali hawa waganga njaa kuwa kesi za kubambikiza zifutwe, na Tukaona Kesi nyingi tu zikifutwa. Sasa hawa Walamba asali leo wanapokuja kudai kuwa eti kesi zao zimefutwa sababu ya maridhiano wanajaribu kujipa umuhimu ambao hawana.

Mheshimiwa Rais
Yaani nimecheka namna walamba asali walivyokukaribisha katika shughuli ya chama chao ya BAWACHA. Eti leo wanakuona wewe ni bora kuliko aliyekuwa mwenyekiti wa baraza lao Halima Mdee ambaye leo wanamuita eti ni mmoja wa kirusi cha Covid.
Mdee ambaye kwa mamlaka ya Urais unamlipa wewe mshahara, ambaye wewe kama mkuu wa nchi na serikali uliyeapa kulinda katiba kama ukiamua kunyoosha rula hapaswi kuwa bungeni lakini eti wewe wanakuona unafaa kuwa mgeni wa heshima ila yeye huyo unayemkingia kifua anaonekana traitor. Mheshimwa rais, hili siyo kosa lao, asali uliyowapa imewalevya, wamechanganyikiwa na sasa wako Irrational kabisa!

Mheshimiwa Rais nimalize barua yangu kwa kusema.

Kwa kweli move za kisiasa ulizofanya ktk mwaka huu wa fedha ni za kitaalamu sana.
Umeweza kuwasoma hawa walamba asali kuwa ni makamanda feki, Njaa kali. Ukiwaonyesha kipande cha mkate tu wanasahau hata majina yao. Ukiwapa asali ndo kabisaaa inawalevya.

Mheshimiwa tafadhali sana, wapunguzie hawa watu asali watawehuka.

Nawasilisha!
Kwaiyo inamaana Mwenyekiti ana tabia za Mnyama aitwae "HONEY BADGER" au wazalamo wanamwita "NYEGERE"!

CHADEMA=HONEY BADGERS
 
Huna hoja umejawa na roho mbaya na umasikini wa akili. Sukuma Gang mbali hili
Mbona ACT-Wazalendo walipoingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar mulikiwa mnawaponda sana.Sasa tulieni na nyie mle nondo za vichwa.

CCM ameoa ACT ila Bi.Mdogo CHADEMA alikuwa ana malingo sasa hivi amekubali show!
 
Pole mkuu, shida ni kuwa wewe na uzao wako mmezoea na mlifuraia kuwaona watu...
Wakibambikiwa kesi.
Wakimwagwa damu zao
Wakipotea milele
Wakitekwa na kuteswa etc

I wish angetekwa mamako au dada zako wakalatiwa na wale wahuni wa dictator JPM the devil ungeelewa why people are happy now.

Overrr
Kwani Samia hakuwepo kwenye serikali ya watekaji?tulieni mmeshikwa pabaya this time!

Mliwaponda sana ACT-Wazalendo walipoingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar,sasa zamu yenu sitaki nataka yenu ndiyo imewaponza.Mara ooh,hatuchukui ruzuku na hatuitambui serikali iliyotokana na uchaguzi wa 2020,sasa kimebadilika nini?,Samia si alikuwa Mgombea mwenza na alidiriki kusema kuwa,"ata tusipopiga kura, CCM itashinda tu" [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ACT walipokuwa wakitamka neno "Maridhiano", Chadema walikuwa wakiwaponda.

Chadema leo nao wameazima neno "Maridhiano" kujustify udalali wao wa kisiasa, halafu wanadhani WaTZ watawapa blank checque
 
Back
Top Bottom