Rais wetu Dkt Magufuli ni mkombozi wa wanyonge, shujaa mpya katika bara la Afrika

Rais wetu Dkt Magufuli ni mkombozi wa wanyonge, shujaa mpya katika bara la Afrika

Mkuu Mimi nakubaliana na wewe 70,% ila approach anayoitumia Magufuli impact yake kwa masikini ni kidogo sana and is not sustainable. Sumbua akili yako kidogo utaliona hili.kwa hii style ya kupiga vigelegele nakwambia ndo mnampoteza kabisa
RAIS WETU DKT MAGUFULI NI MKOMBOZI WA WANYONGE,WANAOMBEZA KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA WALAANIWE MILELE KATIKA JINA LA YESU KRISTO.

Niwajibu wetu Watanzania wazalendo wote kumuunga mkono Rais wetu Dkt Magufuli kwa kazi nzuri na ngumu anayoifanya ya kupambana na wahujumu uchumi . Amejitoa sadaka kwa ajiri yetu wananchi masikini ambao ni muda mrefu tulikuwa tunaonewa, tunanyanyaswa na kudhulumiwa haki zetu na watu wachache ambao waliifanya nchi yetu kuwa shamba la bibi. Rais wetu Mpendwa Dkt Magufuli amerudisha heshima yetu na utu wetu Watanzania.

Kila mmoja wetu katika Imani yake anatakiwa kuwa anamuombea Rais wetu kila Muda ili Mwenyezi Mungu amlinde sikuzote za maisha yake. Kwani ni ukweli usiopingika kwamba Mafisadi, majambazi, vibaka wote, watendaji wabovu wa serikali na wapiga dili wote wanamchukia sana Rais wetu.Sio muda wa kubeza na kumvunja moyo Rais wetu bali ni muda wa kumuunga mkono kwa kila jambo analolifanya kwa maslahi ya wananchi wanyonge wa Tanzania.

Tuwafichueni watu wote wanaoihujumu serikali ya Magufuli bila kuogopa vitisho vyao maana tupo katika Vita kali kati ya kundi kubwa la wajenga nchi yetu na kundi dogo la watu wanaoibomoa nchi yetu kwa kutuibia Raslimali zetu.Silaha ya kuishinda vita hii ni Kushikamana sisi wanyonge na kutengeneza umoja wenye nguvu,kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Mungu amlinde na kumbariki sana Rais wetu kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajiri ya sisi watanzania wanyonge.Na alaaniwe mtu yeyote anayemuombea mabaya Rais wetu Dkt Magufuli.
 
Magufuli ni tumain letu daima kila goti kwake litapigwa.


Tumaini letu ni katika Kristo Yesu. Na kila goti litapigwa mbele zake Kristo na si kwa wanadamu.

Hata Rais wetu anamcha na kumuogopa Mungu pia. Ndio maana anaomba watanzania siku zote tumuombee. Anajua hawezi pasipo Kristo kumtia nguvu na ndio tumaini lake.

Hata yeye atashangaa kuchukua vifungu vya biblia vinavyomwakilisha Kristo na kumuweka yeye. Mungu hashirikiani utukufu wake na wanadamu. Mwogope Mungu, na linda sana uyasemayo yasije kupalia laana kwa uzao wako.

Tuendelee kumuombea Mungu Rais wetu atiwe nguvu afanye yote kwa busara na kumtukuza yeye. Tukimtanguliza Mungu mbele hata yeye uongozi utakuwa rahisi maana mafisadi na wezi watapungua.
 
Be careful na maneno unayodandia bila kuyajua vizuri, yatakugharimu. Ni Yesu pekee tu neno linatuambia kwake kila goti litapigwa na si mwanadamu au kiumbe kingine chochote
Sasa hawa itafikia wakati wataanza kumsujudia
 
Ni wajibu wake kuwatumikia watanzania, ila angekuwa hachapi kazi ndio tungeshangaa.
 
RUKSA KUOMBA UWAZI NA UKWELI UTULETEE UTANDAWAZI ILI TUWE NA MAISHA BORA YATAKAYOLETWA NA HAPA KAZI amina
 
Kujenga nchi ni pamoja na kulipa kodi, hebu tuambie ww unachangiaje kwenye kodi, ukiacha Indirect taxes. Sababu kujenga nchi sio maneno meeengi marefu yasiyo na tija, tuambie category yako ktka kodi sio lazima tujue unalipa sh ngapi, ila tupe tu category, ukiacha indirect taxes.
 
Sijui una maana gani? Labda nikukumbushe kwamba, Dini za kikristo ukisha changuliwa kuwa Rais wa nchi jina lako kamili linatajwa kila jumapili wakati wa sala.
 
Mkubali pia anapokosolewa jamani. Huyo jamaa siyo Mungu.




JPM ni mungu kabisa wa tumbo la huyu jama na CCM kwa ujumla.

Tamko lake moja tu linaweza kuipa neema tumbo la mleta mada.

Udini pia unamsumbua mleta mada. Anaonekana ametaja sifa za JPM kibiblia zaidi.

Amesahau kuwa JK aliwahi kuitwa chaguo la Mungu.

Watanzaia ni watu wenye machungu mengi ya umaskini Moyoni. Ndio maana hata wanafurahia kuona matajiri na wafanyakazi wanasulubiwa. Wanafikiri kuwa huenda hii ikawa ni solution kwa matatizo yao.
Watu bei zimepanda sana na hela zimewapotea mifukoni lakini wameridhika kisa wanaona kuna baadhi ya matajiri wakubwa na wafanyakazi wanatangazwa kwamba ni majipu. Hawajiulizi mbona wanaochaguliwa kujaza nafasi zinazoachwa wazi ni wale wale tu wanaotokana na ukanda,udini na urafiki? Mambo ambayo ndiyo yanayoturudisha nyuma tangu uhuru? Mtu anamfukuzwa kazi kwa sababu anatuhuma ya kulewa lakini anaachwa mwenye tuhuma za wizi wa mabilioni!!
Yani watu wanatamani kupata maisha bora bila mipango ya kitaifa badala ya mipango inaotokana na hisia za mtu mmoja zinazoathiriwa na ubinafsi. Ndio maana mtu anasema huyu nilisoma naye namfahamu . Asiyefahamika hana chake. Hata kushughulikia tuhuma za mtu aliyesoma na rais ni tofauti na yule asiyesoma naye.
 
Kuna upande yuko vizuri na upande mwingine anahitaji kushauri na anaelekea kushindwa. Kwenye mambo ya uchumi anaelekea kushindwa kwa vile ana chuki inborn na wafanyabiasha, hawapendi na hawaamini, anahisi kuwa wafanyabiashara wote ni wezi na amejiweka mbali nao. Hakuna nchi inaweza kuendelea kwa kujitenga na wafanyabiashara kwa vile wao ndio wana ajira na ndio walipakodi. Ila kwa vile ndio walikuwa wanachangia CCM wakaachwa wafanye watakavyo, sasa anavyotaka kuwarudisha mstarini asijiweke mbali nao bali asimamie sheria tu.

Ila kwa ujumla kama raisi atakuwa anashaurika tumempata mtu sahihi kwa wakati sahihi JPM



Ni kweli kabisa JPM ana chuki sana na matajiri wanaofanya biashara zao binafsi.

Anaamini kuwa kila mfanyabiashara ni mhujumu uchumi. Jambo ambalo limejengeka kutokana na siasa ya ujamaa tuliyokuwa nayo.
Hali hii itaporomosha uchumi wa watu sio muda mrefu.
Kodi inayokusanywa kwa miezi aliyotawala ni pesa zile zilizokuwa zimetokana na Mazingira mazuri ya kibiashara aliyoacha Kikwete. Sio muda mrefu watu wengi wataachishwa kazi na kubaki mitaani kutegemea hela za TASAF. Kutokana na kutowaamini matajiri serikali itajiingiza kwenye biashara na itapoteza fedha nyingi sana kutokana na ukweli kuwa hata watu wanaomzunguka kama marafiki wa kumshauri hawana ujuzi wa kivitendo wa biashara zaidi ya kuwa na vyeti vya uchumi. Atajikuta badala ya kutafuta watu kama akina Dr. Kimei kusimamia biashara za umma anatafuta wachunga ng'ombe kutokana na upoti. Kuna watu wana asili ya biashara tangu enzi na enzi, mh. akiwatenga kwa chuki zake binafsi na wapambe wake atashindwa kukuza uchumi.
Serikali iachane kabisa na biashara. Biashara inahitaji uzoefu mkubwa sana ya kivitendo na sio nadharia .
 
nyumbu watapinga sana na watakwita mlevi,hawa wanyama ni ugonjwa
 
Ni kweli anahitaji kuombewa kwani anayafanya yaliyowashinda wengi

Lakini wanasema barabara ndefu haikosi kona na binadamu hatujakamilika ajitahidi asiwe na double standards kwenye kuwajibisha

Apate muda wa kuhakiki tuhuma kabla ya kuhukumu itaongeza kuaminika na kutenda haki


Nani alishindwa?
Kama ni kufukuza Hata Kikwete alifukuza sana Mawaziri na hata kuvunja baraza zima. Na alithubutu hata kuwapeleka mawaziri wengine mahakamani na kuwafunga. Alithubutu hata kumnyang'anya Nkapa mali aliyokuwa amejimilikisha ya Mgodi wa Kiwira.
Matajiri kibao JK aliwafikisha Mahakamani ,mfano wakina Patel na wengine wengi kwenye ushu ya EPA.

Sasa hilo la zaidi kwa JPM ni lipi?
Anatekeleza majukumu yake kama anavyoona inafaa kutokana na ukweli kwamba nchi haina sera maalum ya kitaifa inategemea matakwa ya mtu mmoja. Na huwezi kutoka bila kumwabudu na kumtukuza kama mungu.

Suala hapa ni woga wa watanzania kutokana na umaskini na viongozi wa serikali kufanywa ndio kama mungu wa kuamua nani apate na nani akose?

Kikwete alisifiwa sana wakati wake kwa sababu waliomsifu walijua hatma ya matumbo yao itaboreshwa kwa kumsifu. Ni watu jasiri tu na waliokua wamejitoa mhanga ndio waliokua wanamkosoa kwa wazi na uzuri JK alikua ameacha uhuru wa kujieleza na kumkosoa kwa namna yoyote.
Hata leo sitegemei kamwe mwanaCCM amkosoe Magufuli hata kama atakosea kwa kiwango kikubwa.
Kumkosoa ni kuhatarisha maslahi ya tumbo lako.

Kuna watu wengi sana mfano Paulo Makonda walipata nafasi kutokana na kusifia kila alichofanya JK enzi zake na wakatoka mpaka leo ni vinara.
Mtu pekee aliyewahi kukosoa serikali ndani ya CCM kwa wazi alikua ni Mwalimu Nyerere. Wengine wote kazi yao ni kusifia tu.

Ni hali ya kawaida kwa tawala zenye hulka za kifalme ambapo mamlaka yote anapewa mtu mmoja. Hakuna namana ya kuacha kumpa utukufu kama unahitaji kushiba.
 
Nimekua nikimtafakari Rais Magufuli na mambo anavyoyafanya na anavyoamua yafanyike nimegundua huyu mkuu sio mtu wa kawaida. Yaani sipati neno zuri la kumuita ila kiufupi ni miongoni mwa watu wachache sana wanaotokeaga baada ya vizazi na vizazi. Watu wa aina hii ni watu ambao hufanya vitu tofauti kabisa na ilivyokawaida na hata mafanikio yao huwa si ya kawaida kabisa kiasi cha kubaki kwenye vitabu vya historia vizazi na vizazi. Nimeamua kununua picha yake na kuitundika sitting room kwangu kama nikosa najua watanisamehe.. Hii picha najua itanisaidia sana hasa pale napokua nnamambo ya kutafakari badala ya kuangalia taa au paa ntakua naangalia picha yake. Naawashauri na nyie mnunue muipambe majumbani. Ntapiga picha nikishainunua niweke muamini maneno yangu. Magufuli sio mtu wa kawaida
 
Back
Top Bottom