Ni kweli anahitaji kuombewa kwani anayafanya yaliyowashinda wengi
Lakini wanasema barabara ndefu haikosi kona na binadamu hatujakamilika ajitahidi asiwe na double standards kwenye kuwajibisha
Apate muda wa kuhakiki tuhuma kabla ya kuhukumu itaongeza kuaminika na kutenda haki
Nani alishindwa?
Kama ni kufukuza Hata Kikwete alifukuza sana Mawaziri na hata kuvunja baraza zima. Na alithubutu hata kuwapeleka mawaziri wengine mahakamani na kuwafunga. Alithubutu hata kumnyang'anya Nkapa mali aliyokuwa amejimilikisha ya Mgodi wa Kiwira.
Matajiri kibao JK aliwafikisha Mahakamani ,mfano wakina Patel na wengine wengi kwenye ushu ya EPA.
Sasa hilo la zaidi kwa JPM ni lipi?
Anatekeleza majukumu yake kama anavyoona inafaa kutokana na ukweli kwamba nchi haina sera maalum ya kitaifa inategemea matakwa ya mtu mmoja. Na huwezi kutoka bila kumwabudu na kumtukuza kama mungu.
Suala hapa ni woga wa watanzania kutokana na umaskini na viongozi wa serikali kufanywa ndio kama mungu wa kuamua nani apate na nani akose?
Kikwete alisifiwa sana wakati wake kwa sababu waliomsifu walijua hatma ya matumbo yao itaboreshwa kwa kumsifu. Ni watu jasiri tu na waliokua wamejitoa mhanga ndio waliokua wanamkosoa kwa wazi na uzuri JK alikua ameacha uhuru wa kujieleza na kumkosoa kwa namna yoyote.
Hata leo sitegemei kamwe mwanaCCM amkosoe Magufuli hata kama atakosea kwa kiwango kikubwa.
Kumkosoa ni kuhatarisha maslahi ya tumbo lako.
Kuna watu wengi sana mfano Paulo Makonda walipata nafasi kutokana na kusifia kila alichofanya JK enzi zake na wakatoka mpaka leo ni vinara.
Mtu pekee aliyewahi kukosoa serikali ndani ya CCM kwa wazi alikua ni Mwalimu Nyerere. Wengine wote kazi yao ni kusifia tu.
Ni hali ya kawaida kwa tawala zenye hulka za kifalme ambapo mamlaka yote anapewa mtu mmoja. Hakuna namana ya kuacha kumpa utukufu kama unahitaji kushiba.