Rais wetu Dkt Magufuli ni mkombozi wa wanyonge, shujaa mpya katika bara la Afrika

Fanya kazi uchumi wa nchi ukue sio kuangalia picha
Nikitoka kazini huwa nnavitu vya kutafakari na mara nying nikiwa na tafakari naangalia taa au paa...sasa ntakua naingalia hiyo picha yake maana hata ofisini huwa naiangalia sana
 
Kwangu nitainunua mwaka 2019, bado yupo kwenye mizani.
 
Tumia muda wako mwingi kumuombea. Ndio rai yake, pia Fanya Kazi kwa bidii Na chukia ufisadi.
 
Magufuli is far, far the best compared to what we endured under the ever laughing previous president of the last CCM regime.

Ubovu alionao Magufuli ni bora sana kuliko wema unaosemekana kufanywa na Kikwete pamoja na mkapa wake, ingawa sasa hivi Mkapa anajifanya ni rafiki sana wa Magufuli.
 
Kwa mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu hii, ataunga mkono hoja yako. Mimi naunga mkono hoja yako. Siku zote NABII HAKOSI HESHIMA ISIPOKUWA KATIKA NCHI YAKE. Mungu amlinde na kumbariki Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli.
 
Mungu mwenye nguvu amzidishie ulinzi, hekima, akili, afya na maarifa rais wetu John Pombe Joseph Magufuli. Amen.
 
Kuna baadhi ya makanisa kila siku walikuwa wanamuombea ila siku hizi hakuna kitu kama hicho
Huo ni uzushi usio na mshiko. Sisi kanisa letu tunamuombea kila siku pamoja na serikali yake. Hata JK tulikuwa tunamuombea lakini ndio hivyo tena trip za nje zilikuwa nyingi kwa hiyo sala zilibaki nyumbani mzee yupo nje
 
Huo ni uzushi usio na mshiko. Sisi kanisa letu tunamuombea kila siku pamoja na serikali yake. Hata JK tulikuwa tunamuombea lakini ndio hivyo tena trip za nje zilikuwa nyingi kwa hiyo sala zilibaki nyumbani mzee yupo nje
Mimi nimesema ninaposalia, au wewe kila sehemu unasali
 
Una matatizo,maisha yanazidi kuwa magumu,watu wanapunguzwa kazi sekta binafsi,sukari inapanda,mapato bandarini yanashuka...wewe unatuletea ngonjera..Rais hapimwi kwa kufukuza watu,anapimwa kwa kuboresha maisha ya watu na kuzalisha ajira.Hopeless..
 
Siku hizi makanisa hayamuombei tena,mwanzo walimuombea sana,sukar ilipoanza kuadimika,sadaka na fumgu la kumi kupungua aaah,makanisa yameyumba,hali ya uchumi kwa waumin imeyumba!,waumini walikuwa wakiombewa wapate safar zenye posho sasa wapi,waumin walikuwa wakiombewa wapate warsha zenye hela sasa wapi,mifuko ya waumin imefungwa.
 
Anapokosea tumkosoe bila haya!Hili la ndiyo mzee kwa kila jambo hapana!
 
Ama kweli ubabe umepungua mtaani, hakuna muziki munene kwa magari kama ilivyozoeleka kwa vijana wa town, uchumi wa MTU mmoja mmoja umeleta utata
Magufuli shikamoo..

Bank nako hakuna foleni, tulizoea kuona foleni ndefu kuanzia kuweka hadi kuchukua pesa kwa ATM lakini hazipo tena, sasa ukienda bank unanyoosha kaunta,
Nasema tena shikamooo.

Ubabe wa matajiri na wenye Nazo nao umepungua, sasa tunaheshimiana.
Ninakuamkia..shikamooo.

Ofisi za umma Nazo zilikuwa na miungu watu, sasa no watumishi wa umma na sio miungu watu tena, baba Jesca shikamooo.

Umetumbua majipu bila ganzi na usaha umetudondokea mifukoni,
Mkuu shikamooo.
Wewe ni kiboko
Nasema shikamooo umeleta heshima MUJINI...japo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…