Rais William Ruto atuma Jeshi Congo, KDF direct to DRC

Rais William Ruto atuma Jeshi Congo, KDF direct to DRC

Wewe ndio huelewi, model ya M23 na Alshabaab ni sawa kabisa, wote wanalo jeshi lenye uniform na vikosi kamili, wote huteka na kutawala maeneo, tofauti ni kwamba Alshabaab wakati Fulani hutumia wapiganaji wa kujitoa muanga, lakini hiyo sio tatizo Kama jeshi ni imara katika(military intelligence)

Unatishika na nguo ambazo huvaa wakati wanapiga picha baadae huvua na kuvaa kanzu na kujichanganya na raia ili wasipatikane halafu baadae kuvizia mashambulizi ya kujitoa muhanga?
 
al shabaab wanaopigana jangwani panapoonekana tu wamewashinda, wataweza kupigan ana watu wa msituni wanaojificha kwenye miti? wakenya wanachekeshaga sana. wanachotuzidi ni uchumi tu na kiingereza, ila vingine hawana uwezo. inasemekana al shabab hadi wanawala kiboga hao askari huko somalia.
Alshabab aka wavaa kobazi hawako uwanja wa vita.... ustadh wako kakupiga kamba huko madrassatul
 
Mkuu na wewe ukawe Frontline maana unaonekana mzalendo ...Marekani imeweka kitita Cha kumsaka Joseph Koni....kwhy huko sio lelemama
Ikitakiwa kuwa ivyo nitaenda Kwa ajili ya nchi yangu,hii nchi sio ya kuchezewa.
 
Ww bado mdogo sana, unajua Kagame alikuwa nusura Tz imtoe wakati alimtusi JK.. Aliomba msamaha haraka, baada ya JPM kuingia madarakani akajipendekeza haraka sana kisa JK alimtengeneza na kumtia adabu. Unajua TZ ilimaliza kabisa M23 na kupotea kabisa, Kagame hawezi chukua round kwa Tz.. Tatizo lako utoto hujui kitu.
Itakua alikua shule miaka Ile M7 ndio alisuluhisha Lile suala na Pk alikaliwa kooni kweli kweli.
 
Haya sio maamuzi ya Ruto, ni mpango ameukuta ulioandaliwa na mataifa yote ya EAC, imefikia hatua DRC isaidiwe...

Ndio na mwenyekiti wa East Africa alikua Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kikosi hicho maalumu kilipewa jina la EACRF- East African Community Region Force na ikashauriwa kwa mfano hao makamanda 1000 waliopelekwa ni wale special force ambao wanaweza kupiga kazi kubwa kwa muda mfupi, nchi za Burundi, Sudan Kusin na Uganda nazo zinatakiwa kupeleka askari wao haraka sana wakashirikiane na Jeshi la DRC ambalo linaonekana kua dhaifu mbele ya waasi.
 
Alshabab aka wavaa kobazi hawako uwanja wa vita.... ustadh wako kakupiga kamba huko madrassatul

Wangekua front wangeshamalizwa muda mrefu lakini wanapigana huku wakitumia jamii kama ngao yao ya kujificha, na mbaya zaidi wanaenda msikitini kuswali huku wakipata muda wa kupanga mambo yao kupigana nao ni ngumu si unaona waasi wa msumbiji walivyopotezwa haraka sana. Kwa sababu walikua wako uwanja wa vita kabisa
 
[emoji1][emoji1] kwamba Nyie Sasa ndio mmegeuka kua Savior wa East Africa [emoji1][emoji1][emoji1],acheni kujipa umuhimu msiokua nao.
Umesahau kilichomkuta Makenga na M23 yake Ile kazi ilifanywa na Jeshi la Kongo TZ ilikua inatoa ushauri tu wa kimedani ila Sultan alikumbia sasa hivi wakongo wakae pembeni kwanza tunataka kuonyesha izi kazi zinavyofanyika.
 
Majeshi ya nchi zifuatazo yako Congo huko miaka na miaka na hayajaweza kuleta amani(Pakistan, India, Bangladesh, Brazil, Ukraine, Paraguay,SouthAfrica, Senegal, Egypty, Malawi, Niger, Morocco,Tanzania.

Sasa ngoja tuone Jeshi la Kenya litaweza kuleta utofauti wa Aina gani.
 
Dawa ni kuwapelekea moto tu Rwanda alienda Msumbiji kutusukumia wale magaidi yaingie nchini kupitia Mtwara Wala hatukulialia tulipambana tu na hali zetu. Ni muda sasa wa kwenda Mashariki mwa Congo kusukuma waasi wanaoisumbua Congo watafute Kwa kwenda na hatutaki kusikia kelele humu.
Hao M23 siku zote wakizidiwa huwa wanakimbilia Rwanda na kupewa hifadhi, Rwanda akiulizwa mbona unawatetea anakwambia nimewaweka kwenye Makambi maalum, maana nao ni binadam na wanahitaji kulindwa, sasa kwanini ulinde magaidi kama si wewe unaewatuma kuiba madini?
 
This time Mimi natamani wasikimbilie popote pale zipigwe mpk mwisho tuone itakavyokua tu.
 
Kagame awe makini tu kwenye safari yake ya Burundi aweke maanani yaliyomkuta Rwagasore hawa Wakongo pia hawaaminiki.
Huyu Kagame ndiye mmiliki wa Rwanda kama Ccm inavyoimiliki Tz.
 
Huyu Kagame ndiye mmiliki wa Rwanda kama Ccm inavyoimiliki Tz.
Anastahili,wakati Watu wake wanauwawa kwa maelfu ni yeye peke yake na RPF ndio walikomesha Mauwaji, hata Ufaransa ilikasirika na kutuma Vikosi ili mauaji yaendelee, lakini Mungu ni mkubwa walipigwa ganzi na Mungu.

Kagame anastahili kukaa mpaka atakapo andaa mrithi wake.

Anastahili pongezi sana huyo Jamaa.

Sisi tulimtuma Kinana kwenda kung'aa macho pale Rusumo na kujifanya anasikitika.
 
Uhuru nae hivyo hivyo alituma KDF kule Somalia, Matokeo yake Alshabaab wakaja kushambulia Kenya eg. ( West Gatte attack) Ruto nae anaenda kufanya jaribio ambalo kwa haraka haraka ni vigumu hicho kikosi kufanikiwa dhidi ya M23, Serikali za DRCKongo zimepambana na hhili kundi kwa muda mpaka sasa na halionekani kurudi nyuma, kila siku wanasumbua raia katika majimbo kadhaa na kuteka miji, KDF wanaenda kufanya nini kipya humo msituni?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mbaya zaidi m23 wanaujua huo msitu vizuri kuliko hao KDF yaani nawaonea huruma watadakwa kama vindege huko msituni
 
Nimesoma pahala KDF walichakazwa huko El Ade Somalia mpaka wakachanganyikiwa na kuanza kutwangana risasi wao kwa wao😆😆
 
Majeshi ya nchi zifuatazo yako Congo huko miaka na miaka na hayajaweza kuleta amani(Pakistan, India, Bangladesh, Brazil, Ukraine, Paraguay,SouthAfrica, Senegal, Egypty, Malawi, Niger, Morocco,Tanzania.

Sasa ngoja tuone Jeshi la Kenya litaweza kuleta utofauti wa Aina gani.

Hayo majeshi ni vikosi vya kulinda amani chini ya MONUSCO, vikosi hivyo haviruhusiwi kupigana vita na waasi, lakini vikosi vya EACRF wao wanaenda direct kupigana na waasi hivo hizo ni mission mbili tofauti, yaani TPDF ikipeleka kikosi kingine ndio kitakua vitani na sio kile kilichopo kule chini ya MONUSCO, ni kama kipindi kile SADCRF ilivyokwenda kumtandika M23 haikuhusiana na mission ya MONUSCO
 
Kazi ya FIB Ni Nini Kwny MONUSCO?
 
Back
Top Bottom