Kazi ya Monusco na EADF ni kulinda amani tu na sio vinginevyo. Ndio maana leo hii watu wanashangaa kenya imetuma wanajeshi wake ila hawajui huko zaire kuna wanajeshi zaidi ya 18,000 wa Monusco kutoka nchi mbali mbali ikiwemo marekani china na india. Na hao M23 hawawezi kuisha leo wala milele kwasababu watu wanatajirika kupitia wao. Wengi wanamlaumu kagame kwamba anawapa silaha ila sio kweli bali kuna tuhuma nyingi sana za exchanges za bunduki kwa dhahabu, bunduki kwa ndovu au pembe na bunduki kwa almasi, ambazo zinafanywa na monusco ndani ya Zaire. Tanzania tunawanajeshi wetu zaidi ya 900 huko Zaire kwahyo lazima ujiulize inakuwaje wanajeshi kibao alafu wanashindwa na M23 ukitafakari vizuri utaelewa kuna biashara kubwa sana hapo Zaire.