Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ili kukabiliana na changamoto mpya

Rais Xi Jinping asisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika ili kukabiliana na changamoto mpya

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
微信图片_20220224143546.jpg

Wiki hii rais Xi Jinping wa China ameandika bara ya pongezi kwa sherehe za uzinduzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kilichoko mjini Kibaha, mkoani Pwani, Tanzania. Chuo Kicho kilianzishwa na vyama sita vilivyoshiriki kwenye ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ambavyo ni Chama cha Mapinduzi cha Tanzania, Chama ch African National Congress cha Afrika Kusini, Chama cha Ukombozi cha Msumbiji FRELIMO, Chama cha ukombozi wa Angola MPLA, chama cha ukombozi wa Namibia SWAPO na chama cha ukombozi wa Zimbabwe ZANU-PF.

Kwa watu wanaofuatilia mambo ya uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, hatua hii ya kuzinduliwa kwa chuo hicho si jambo geni, bali ni mwendelezo wa uhusiano ulioanza muda mrefu uliopita, na kukamilika kwa ujenzi wa chuo ambacho mipango yake ilikuwepo tangu muda mrefu uliopita. Kwa wasio na uelewa wa kutosha kuhusu uhusiano kati ya China na nchi za Afrika, kufunguliwa kwa chuo hicho ni ushahidi kuwa ushirikiano wa leo kati ya China na nchi za Afrika umetoka mbali sana, tofauti na jinsi baadhi ya watu wanavyofikiria kuwa umeanza baada ya China kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi au baada ya nchi za Afrika kuwa na mazingira ya kuvutia wawekezaji kutoka China.

Bango kubwa lililowekwa kwenye viwanja vya chuo hicho, linaonyesha picha kubwa za Rais Xi Jinping wa China na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, kwa sababu wawili hawa kwa sasa ndio wameshika hatamu za kuendeleza uhusiano huu, na msingi wa ushirikiano kati ya China na Tanzania. Lakini pia kuna picha nyingine saba za aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha China Mao Zedong, na viongozi waasisi wa vyama vya ANC, CCM, FRELIMO, MPLA, SWAPO, ZANU-PF, waliokuwa viongozi wa vyama kupigania ukombozi wa nchi za Afrika. Picha hizo zinakumbusha kuwa ujenzi wa chuo hicho siyo tu ni alama na matokeo ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya pande mbili za China na nchi vilivyoko vyama hivyo, bali pia msingi wa uhusiano wa karibu uliopo kati ya China na nchi ambazo vyama hivyo vilipigania ukombozi.

Kwenye hotuba iliyotolewa na Rais Samia Suluhu kwenye ufunguzi wa chuo hicho, alikumbusha jinsi chama cha kikomunisti cha China kilivyounga mkono juhudi za vyama hivyo katika mapambano ya kujiletea ukombozi, na hata kusema ujenzi wa chuo hicho ni msaada kutoka China wenye lengo la kuendeleza mahusiano ya karibu kati ya Chama cha Kikomunisti cha China na vyama vya nchi za Afrika.

Hali halisi ya sasa ni kwamba mazingira ya dunia yamebadilika, China ya sasa na nchi za Afrika ni tofauti kabisa na zilivyokuwa kwenye miaka ya sitini na sabini. Ndio maana Rais Samia Suluhu alizungumzia jambo moja la muhimu, ambalo ni kuhakikisha falsafa zilizoonyeshwa na waasisi wakati wa ukombozi, zipewe mtizamo wa kisasa. Alifafanua kuwa falsafa hiyo ihimizwe kwenye kujenga nchi, na kuhimiza uchumi na maendeleo.

Alichosema Rais Samia kinashabihiana kabisa na alichosema Rais Xi Jinping kwenye barua ya pongezi kuhusu kufunguliwa kwa chuo hicho. Rais Xi amesema kwenye barua hiyo kuwa kwa sasa dunia inapita kwenye mabadiliko ambayo hayajawahi kuonekana katika karne moja, China na Afrika zinahitaji kuimarisha mshikamano na ushirikiano zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili kukabiliana na hatari na changamoto, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kuboresha ustawi wa watu. Rais Xi amesisistiza umuhimu wa shule hiyo kutoa jukwaa kwa vyama hivyo sita kuongeza uwezo wao wa kiutawala na kuongoza vyema nchi zao,ili kupata maendeleo na kuwanufaisha watu wao.
 
Putin na Xi Jinping ni viongozi wanajielewa sana.
 
Kwa iyo makada wa ccm wanaenda kupatiwa elimu ya uongozi yenye kuleta maendeleo na kuacha kupenda rushwa?. Nauliza
 
Hawa ni matapeli, wanafanya ushirikiano na vyama vinavyotawala visivyojielewa ili viziibie nchi masikini, mfanyabiashara hawezi kuwa rafiki wa masikini hata dakika moja.
 
Back
Top Bottom